Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Mara nyingi sisi hupenda kuiga au kujilinganisha na hawa wenye demokrasia yao waliyoitengeneza kwa muda mrefu.

Sasa nauliza, hizi mbinu za CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe inakidhi kweli mlinganisho wowote na wayafanyayo Democratic Party na Republican wa Marekani au Chama cha Labour na Conservative vya Uingereza; au hata vile vilivyoko Ujeruman kwa namna yoyte ilei?

Nionavyo mimi, haya majadiliano na maridhiano ni njia tu za kutafuta ulaji kwa raha toka kila upande, bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake.

Ninaelewa, kuna mambo ambayo huwaleta pamoja hao wakubwa wa dunia, na yote ni yale yanayohusu siasa za nje, hasa wanapopambania maslahi ya nchi zao dhidi ya mataifa wanayoyaona kuwa hatarishi kwa maslahi yao.

Haiwezi hata siku moja ikatokea watu wa Democratic Party wakawaalika wenzao wa Republican kusherehekea shughuli zao za kichama. Hali ni hiyo hiyo na Labor party na Conservatives; na hata kule Canada, Australia, hata Japan, Korea Kusini na kwingineko.
Hii haina maana kwamba hawapendani kama ndugu, au kwamba kuna uhasama kati ya vyama vyao, lakini ndivyo ilivyo ni kama utamaduni kwao.

Sasa sisi tunaiga kitu gani, kama siyo njia tu za kuhalalisha kugawiana mafao ya jasho la wananchi.
Hayo yanadondokea katika Mila na Desturi??

Kimsingi, mila na desturi za siasa zetu hazina ulinganisho;we are a rare species, if I may- na nchi yeyote Duniani, bali tunaigwa.

Siasa zetu ni Unique.

Naona uko sahihi Mkuu.
 
Watu wanaimba tu "maridhiano" lakini ni viongozi wao tu ndiyo wanajua wameridhiana kitu gani.

Kwa nini imekuwa siri kutoka nje na kuutangazia umma walichokubaliana?

Hata hili la kupokea ruzuku isingekuwa ACT kuliibua lilikuwa siri.
 
Haya sio maridhiano bali hali ya mmoja wa washindani kukubali kushindwa na kuungana na washindani wake.......

Kwa macho ya kawaida inaonekana ni jambo jema lakini kwenye ulingo wa kisiasa ni kwamba CHADEMA inajichimbia kaburi lake.... kutokana na misingi ya kisiasa ya CHADEMA........

Bado nchi yetu Ina uhitaji wa siasa za CHADEMA kutokana na upuuzi na uozo wa serikali dhalimu......

Mimi kwa mtazamo wangu ni maridhiano haya hayakuzingatia maoni na utashi wa wananchi mbele ya safari.......
Chadema inajichimbia kaburi lake, how? umeona nini kilichoshusha nguvu ya Chadema kwasababu ya maridhiano mpaka sasa kule field?

Hisia tu.
 
Na 'obviously' hakuna katiba mpya kabla ya 2025,
Na hapa ndio shida inaanza, nani kakwambia hakuna katiba mpya before 2025? Hii 2023 Bado Ina miezi 8 hapo Bado miaka 2 mingine hivi kweli tukose katiba for 2.8 years?

Tuache pessimism
 
Mapambano ya wakomunisti hayapaswi kufananishwa na hawa Chadema ni mbingu na ardhi.

Si sahihi kuwa vunjia heshima wakomunisti walio pambana kwa jasho na damu ili kukomboa nchi bila sarakasi za maridhiano ukifananisha struggling zao na hawa Chadema.
Sasa kama hao kina Chiang Kai Shek na Mao Tse Tung waliungana ndio sembuse Mbowe na Samia kukaa meza Moja kukubaliana masuala muhimu ya taifa?

Siasa sio uadui mkuu
 
Chadema inajichimbia kaburi lake, how? umeona nini kilichoshusha nguvu ya Chadema kwasababu ya maridhiano mpaka sasa kule field?

Hisia tu.
Huo ni mtazamo wangu tu ndugu.... inaweza kuwa tofauti na ninavyoona.....
 
Sasa kama hao kina Chiang Kai Shek na Mao Tse Tung waliungana ndio sembuse Mbowe na Samia kukaa meza Moja kukubaliana masuala muhimu ya taifa?

Siasa sio uadui mkuu
Unafahamu hivyo vyama viliungana kwa sababu gani ?

Kwa hiyo na nyie Chadema mmeungana na CCM huku adui yenu akiwa nani ?
 
Kinachoendelea ni wanasiasa kuungana kuwakandamiza wananchi.

Tukatae huu usanii unaoendelea maana sisi ndio tunaopoteza zaidi.

Kwani hakuna wa kuzungumzia hali ngumu za wananchi katika mazingira haya ambayo wote ni kitu kimoja.
Wee shindwa Pepopunda na hao walinda legacy wenzako!! Yaan mlishazoea kula nyama za watu ,kuua kutesa na kuteka wapinzani, sasa haya yanayoendelea ni chukizo kwenu!! Yaan nyie na genge lenu mnataman siasa kama zile zenu za kutekana, shubaamit!!!
 
Mara nyingi sisi hupenda kuiga au kujilinganisha na hawa wenye demokrasia yao waliyoitengeneza kwa muda mrefu.

Sasa nauliza, hizi mbinu za CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe inakidhi kweli mlinganisho wowote na wayafanyayo Democratic Party na Republican wa Marekani au Chama cha Labour na Conservative vya Uingereza; au hata vile vilivyoko Ujeruman kwa namna yoyte ilei?

Nionavyo mimi, haya majadiliano na maridhiano ni njia tu za kutafuta ulaji kwa raha toka kila upande, bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake.

Ninaelewa, kuna mambo ambayo huwaleta pamoja hao wakubwa wa dunia, na yote ni yale yanayohusu siasa za nje, hasa wanapopambania maslahi ya nchi zao dhidi ya mataifa wanayoyaona kuwa hatarishi kwa maslahi yao.

Haiwezi hata siku moja ikatokea watu wa Democratic Party wakawaalika wenzao wa Republican kusherehekea shughuli zao za kichama. Hali ni hiyo hiyo na Labor party na Conservatives; na hata kule Canada, Australia, hata Japan, Korea Kusini na kwingineko.
Hii haina maana kwamba hawapendani kama ndugu, au kwamba kuna uhasama kati ya vyama vyao, lakini ndivyo ilivyo ni kama utamaduni kwao.

Sasa sisi tunaiga kitu gani, kama siyo njia tu za kuhalalisha kugawiana mafao ya jasho la wananchi.
BASI IGA NA USHOGA UWAFUNDISHE NA WANAO
 
Wee shindwa Pepopunda na hao walinda legacy wenzako!! Yaan mlishazoea kula nyama za watu ,kuua kutesa na kuteka wapinzani, sasa haya yanayoendelea ni chukizo kwenu!! Yaan nyie na genge lenu mnataman siasa kama zile zenu za kutekana, shubaamit!!!
Sio lazima kila kitu uchangie mambo mengine yapo juu ya uwezo wako wa kufikiri.

Achie waliokuzidi wachangie.
 
Sio lazima kila kitu uchangie mambo mengine yapo juu ya uwezo wako wa kufikiri.

Achie waliokuzidi wachangie.
Unajua stroke hakuna kitu kibaya kama hujui kua hujui!! Sasa kama kwel unayo akili ungeweka facts.. je viongoz wa kisiasa na chama tawala wameungana kuwaumiza wananchi kvp? Pili.. umesema ni wasanii well lielezee jukwaa hili kwa evidence huo usanii wao, tatu.. umewalaumu hawazungumzii matatizo ya wananchi well, kwa akili yako unadhan hapo walipoanza na hilo ndipo tayar washamaliza sera zao na mikutano wamekamilisha? Kwann ulazimishe waanze na kile unataka? Hata vyama vya siasa vina schedule zao za kisera!!! All in all jambo hili la maridhiano limekua kero kwa wengi san ndan ya upinzani na ndan ya CCM!!
 
La kuwa sehemu ya CCM iliyowakandamiza wakati wote huu. Badala ya kuwakandamiza kwa maumivu, sasa inawakandamiza kwa kuwaondoa kwenye lengo lao kuu la kushika madaraka ya nchi.

Nimekusoma vizuri kabisa na kukuelewa, nami nikueleza kwamba, inawezekana kabisa CHADEMA ilipata heshima kubwa wakati wa Magufuli kuliko wakati mwingine wowote. Hii turufu waliyokwishaipata, sasa inaonekana kama wanataka kuipoteza kimzahamzaha tu chini ya Samia.

Siwezi kamwe kum'underestimate' Kinana; na anakuwa hatari zaidi anapounganishwa na Samia. Hawa hawatumii njia za maumivu, wao wanatumia njia za laini tu kummaliza mpinzani wao.
It's too late ndugu Kalamu kwa hicho kilicho kwenye fikra zako kufanyika au kutokea. Historia ya CHADEMA ilikotoka na ilipo ni reference nzuri na ya wazi kabisa..!

By the way, sijakuambia um - underestimate Kinana. Lakini nimesisitiza sana kuwa, nyakati na majira zinabadilika. Vivyo hivyo mazingira, mikakati na mbinu za kufanya siasa zinabadilika kulingana na nyakati..

Na kwa hiyo, vivyo hivyo kama ambavyo hum - underestimate Kinana na CCM yake, kwa akili hiyo hiyo usijaribu kuu - underestimate upinzani hususani CHADEMA kwa mbinu na mikakati yao ya kufanya siasa sasa..!

Mimi naiona CHADEMA iliyokomaa na iliyo tayari kuiporomosha chini CCM na kushika dola kwa namna hiihii ambayo ninyi wengine mnaona kama wameingizwa chaka vile..!!!

Hiyo ndiyo hoja yangu..
 
Huo ni mtazamo wangu tu ndugu.... inaweza kuwa tofauti na ninavyoona.....
Kama inaweza kuwa tofauti na vile unavyoona, basi bora muweke akiba hizi lawama zenu mpaka pale zitakapokuja thibitika, kwasasa muache hizi ramli.
 
Mapambano ya wakomunisti hayapaswi kufananishwa na hawa Chadema ni mbingu na ardhi.

Si sahihi kuwa vunjia heshima wakomunisti walio pambana kwa jasho na damu ili kukomboa nchi bila sarakasi za maridhiano ukifananisha struggling zao na hawa Chadema.
Wewe ni mzito kuelewa.. unajua maana ya UMOJA WA KITAIFA?
 
Wacha kujitoa akili makusudi na speculation zako!

Unachekesha unapowalaumu Chadema, halafu sehemu nyingine nikikusoma unaandika wacha muda uamue, mbona upo kama popo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nilijuwa toka ulipobababaika kule mwanzo na hoja ya "visheria"kwamba hutakuwa na akili tulivu tena katika kujadili chochote, kwa hiyo nikakudharau tokea hapo.

Endelea kuhangaika mwenyewe upendavyo.
 
Wengi wanaweza kuibeza chadema kwa uwamuzi iliyochukuwa ,zaidi viongozi wao waandamizi kama Mbowe kwamba wamekubali ku compromise lakini ilikuwa hamna namna hii ndio njia peke kwa nchi kama Tanzania , mbinu inayoweza zaa matunda ,why? Viongozi walitoa maelekezo kufanyike maandamano kupinga uvunjwaji wa katiba unaofanywa na chama tawala waziwazi lakini watu ni waoga, na hakuna mfano Matokeo yake watu kama Mbowe na wengine wakafunguliwa mashtaka ya uongo, lengo likiwa na kuwatisha na ni kweli watu wote wanaodai ni wapenda mabadiliko wakatishika .Sasa kwa mazingira haya ya hapa Tanzania ni ngumu kupata reforms kwa kutumia people's power kama tunavyoona mataifa mengine sababu mataifa mengine wanachama wakiamua lao linakuwa lao wote sio pale viongozi wanapokuwa wamekamatwa bási na movements zote za kudai mabadiliko zinakuwa zimekoma.Mbowe na wezake wameamua kuja na initiatives nyingine ya kudai mabadiliko kulinga na mazingira na nature ya mtazania jinsi alivyo na ikiwa ni tofauti na jinsi ijulikanavo duniani kwa vyama vya upizani kutoku negotiate na chama tawala .Kamwe mabadiliko hayawezi kuja kwa kutegemea viongozi peke kwamba wao ndio wawe front alafu wa wanachama mpo kwenye sofa na smart phone mnalalama badala yake mnabidi strategy, no way out.
Mkuu 'Srkaka', nimekusoma kwa uangalifu ili nikuelewe vizuri. Nimekuelewa hoja yako.

Lakini, bado hoja haielezi kwa nini CHADEMA hawana ushawishi wa kutosha kuwaamsha wananchi wafanye kama unavyosema kwenye andiko lako.
Swala la waTanzania kuwa "waoga", siyo kweli. Tumeona jinsi walivyosimama kidete kumkabili Nduli, katika hali ngumu sana; na jinsi walivyokuwa mbele kabisa kutetea upatikanaji wa uhuru wa wenzetu waliokuwa bado chini ya ukoloni.

Kwa hiyo, waTanzania siyo watu tofauti na hao wengine wa mataifa mengine.

Jambo unalotakiwa kukifahamu ni kuwa waTanzania siyo watu wa papara na kufuata tu mkumbo, lakini ni watu ukiwaeleza na wakikubali unayowaeleza na kukuamini, basi ujue umekoga roho zao na watashiriki katika mambo utakayotaka wayashiriki.

Ni kwa bahati mbaya sana, CHADEMA hawajawa na ushawishi huo kwa aTanzania. Siwezi kueleza sababu hasa ni zipi, lakini ukweli ndio huo kwamba wengi wa raia wetu bado hawawaamini viongozi wa CHADEMA, kwa hiyo hawawezi kushiriki kwenye mapambano hayo ya CHADEMA, hata kama baadhi yetu tungependa iwe hivyo ili CCM wapate nafasi ya kupumzika na kujitafakari.
 
Na hapa ndio shida inaanza, nani kakwambia hakuna katiba mpya before 2025? Hii 2023 Bado Ina miezi 8 hapo Bado miaka 2 mingine hivi kweli tukose katiba for 2.8 years?

Tuache pessimism
Again, ningekuwa na hela za kutoa sadaka; nisingesita hata kidogo kutoa sadaka juu ya hili jambo la Katiba Mpya 2025.
Na kwa usahihi, Katiba Mpya inastahiri kuwepo kabla ya 2024 kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 
Back
Top Bottom