Ni chaka gani waliloingizwa hawa CHADEMA?
Na ni kwamba unahisi wameingizwa chaka au una uhakika kuwa wameingizwa huko? Kama una uhakika eleza ni Kwa namna gani...
By the way, kwanini usiamini kuwa Rais Samia na CCM yake ndiyo haswaaa wameingizwa chaka na CHADEMA?
Ndugu
Kalamu usiishi jana. Ishi Kwa kuingalia leo na sasa..
Nisome vizuri
Kalamu, kwamba, mimi naamini na kujua kuwa CCM na Samia ndiyo haswaaa wameshanyoosha maneno...
Sababu ni hizi zifuatazo:
1. Kinana unayefikiri ni mwana mikakati hodari, alikuwa katibu wa CCM karibu kipindi chote Cha urais wa JK.
Huyu huyu Kinana na JK wake alishindwa sawia kuiua CHADEMA na badala yake walipofanikiwa kumuingiza yule dhalimu mdarakani, moto ukawawakia na wao pia. Hawakuamini..!!
2. Kama CHADEMA ingekuwa ya kufa, ingeweza kuuwawa wakati wa miaka karibu saba (2015 - 2021) ya utawala wa CCM ya John P. Magufuli aliyedhamiria kufanya hivyo Kwa njia za mkono wa chuma na kuvunja sheria na katiba.
CHADEMA chini ya Mbowe freeman, haikufa wala kuugua...!!