Hebu kwanza jibu nilichokuuliza mwanzo, usijibu swali kwa kuuliza swali lingine, hiyo kwangu inaonesha hujui mantiki ya kile unachosimamia.
Naona unaendelea tu kuzungumzia mambo yasiyo na standard, unapenda sana kujadili hisia ndio maana neno sheria limekukera, nani aliesema tuwaige wazungu kila wanachofanya? una hoja nyepesi unazoziamini ni nzito, hatubanwi na yeyote kuiga kila wanachofanya wazungu- fact.
Nimetumia neno sheria kwasababu hiyo ndio standard ya kujua kama mtu/taasisi fulani imekosea au vinginevyo, sijui kwanini matumizi ya hilo neno yakukere! itakuwa ni kwasababu unajua hauna majibu ya kile ulichoulizwa.
Nakuuliza tena, hiyo asali unayolalamika Chadema wamelambishwa [ kupokea ruzuku] au kama huzungumzii ruzuku kwenye asali yako useme, ipo kisheria au haipo kisheria?
Usitake kubadili maana ya kile nilichokuuliza bila sababu, mimi sijawaambia CCM wasifuate sheria popote, sasa unaponiambia mbona wao huwa hawafuati sheria, maana yake unataka na Chadema wavunje sheria!
Unaposema nachojaribu ku-spin hakiwezekani, huo ni mtazamo wako, sikulazimishi uamini tofauti, lakini pia, nawe usilazimishe wengine waamini kile unachoamini wewe, kama umeamua kuimba "asali" bila ushahidi, endelea kuimba mapambio yako ...