Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

kuwa sehemu ya CCM iliyowakandamiza wakati wote huu. Badala ya kuwakandamiza kwa maumivu, sasa inawakandamiza kwa kuwaondoa kwenye lengo lao kuu la kushika madaraka ya nchi.
Inawakandamiza kwa kuwapatia katiba mpya na tume huru?? Inawakandamiza kwa kuruhusu mikutano ya kubomoa ngome za CCM? Inawakandamiza kwa kuachia wafungwa wa kisiasa?
 
Ni jambo la kawaida sana vyama kuungana vinapopigania maslahi ya taifa... ikumbukwe utawala uliopita ulivuruga kabisa umoja wa kitaifa uliojengwa tangu 1961. CCM na CHADEMA ni wahanga wakubwa wa ushenzi uliofanywa kwa miaka mitano ya mwendazake. Ilifikia hatua aliyekuwa mkuu wa mkoa Gambo aliwaweka rumande waliokuwa wanaenda kutoa rambirambi kwenye msiba wa watoto wa Lucky Vicent School.. waliofanya maombi kwa ajili ya Lissu nao waliingia matatani.. hata ndani ya CCM watu walioshinda kura za maoni majina yao yalikatwa kibabe. Ilifika mahali chuki ilienea kila upande.. Hata wanaCCM waliogopa kabisa kujichanganya na CHADEMA kwa kumhofia yule fedhuli na wapambe wake. Kinachopiganiwa kwa sasa ni kujenga umoja wa kitaifa na kuondoa zile chuki.

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia vinaanza iliwakuta wachina wakiwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.. chama cha Kuomintang (KMT) kilikuwa kikipigana na kile cha kikomunisti (CCP), ikabidi wasitishe vita yao na kuungana kumpiga mjapani aliyekuwa kawavamia. Walipigana na mjapani kuanzia 1937 hadi 1945. Baada ya vita ya pili kwisha wachina wakarudi kwenye vita yao ya wenyewe kwa wenyewe hadi 1949 ambapo CCP walishinda. Kwa hiyo kinachoendelea kwa sasa ni kawaida kabisa kutokea. Siasa za nchi zitaendelea kama kawaida. Pia sio lazima CCM au CHADEMA ndo viongoze kwa maisha yote. Kinaweza kutokea chama kingine chenye nguvu mambo yakabadilika.
 
Nevermind, let it be abysmal, that is of the least worry to me.
But as we have agreed between us, let time speak for itself.
We keep reiterating this statement but you still make conclusions based on daily events? Just give it time and you'll realize how Samia and Mbowe are transforming the political dynamics in Tanzania.
 
Weird analysis!! Embu tuongee ukweli hivi kwa jinsi Samia alivyoji potray kuwa fair politically, je ukitokea uchaguzi Leo Mbowe hatorudi bungeni?? Yaani kwanini kipindi Cha Samia ambapo Mbowe yupo huru kufanya chochote ndio ategemee cheo CCM??

Kipindi Cha JPM Kuna mpinzani alikua na uhakika wa kushinda Jimbo au kata? So Ile ilikua ni motisha tosha kwa wapinzani kuhamia CCM Ili kusecure political future. Na ukweli wapinzani wengi mnoo walihamia CCM sio sababu ya kununuliwa Bali kuokoa political career.

Sasa kwa kuangalia hizo scenario mbili, je kwanini Lissu au Mbowe wasihamie CCM ya 2020 ambayo Kulikua hakuna hope ya upinzani kupata uongozi ILA wahamie CCM ya 2023 ambapo upinzani una matumaini ya kubeba sio tu majimbo zaidi ya 100 Bali Dola kabisa???
Nadhani tumekwishakubaliana mahala, kati yako na mimi, kwamba lengo kuu sasa linaloihusu CHADEMA ni kupata "win-win', wapoteze baadhi ya mambo na waweze kuwa serikalini au Bungeni. Hili nilikwishalielewa toka kwako, kwa hiyo ssiyo swali ninalohofia wewe kuwa nalo.

On the otherhand, mimi nasema juhudi zote kubwa walizofanya CHADEMA kabla, na wakati wa Magufuli ambazo zilionyesha kwamba sasa wanaelekea kwenye lengo lao kuu la kushika mamlaka, kwa ajabu kabisa linawaponyoka mikononi kwenye dakika za majeruhi!
 
We keep reiterating this statement but you still make conclusions based on daily events? Just give it time and you'll realize how Samia and Mbowe are transforming the political dynamics in Tanzania.
That was between you and me, it didn't involve the rest of the audience in this forum.
 
Negotiation zote duniani zinalenga win-win, hivi unadhani CCM na yenyewe Haina demands? Inakubali demands za Chadema pekee??
wapoteze baadhi ya mambo na waweze kuwa serikalini au Bungeni
Wapi wamesema wanataka kuwa serikalini? Why unalazimisha hili suala? Wanachotaka ni katiba mpya Ili CCM na Chadema 2025 iwe Kila mtu ashinde kwa haki so win-win Wala sio vyeo vya uRC na uDC!!
the otherhand, mimi nasema juhudi zote kubwa walizofanya CHADEMA kabla, na wakati wa Magufuli ambazo zilionyesha kwamba sasa wanaelekea kwenye lengo lao kuu la kushika mamlaka, kwa ajabu kabisa linawaponyoka mikononi kwenye dakika za majeruhi
Madaraka utayashika Kwa katiba ipi hiyo?
 
Negotiation zote duniani zinalenga win-win, hivi unadhani CCM na yenyewe Haina demands? Inakubali demands za Chadema pekee??
Huwezi kuniambia kwamba hakuna yasiyokuwa 'negotiated.'
Negotiation zote duniani zinalenga win-win, hivi unadhani CCM na yenyewe Haina demands? Inakubali demands za Chadema pekee??

Wapi wamesema wanataka kuwa serikalini? Why unalazimisha hili suala? Wanachotaka ni katiba mpya Ili CCM na Chadema 2025 iwe Kila mtu ashinde kwa haki so win-win Wala sio vyeo vya uRC na uDC!!

Madaraka utayashika Kwa katiba ipi hiyo?
Naona unapenda sana wakati mwingine hiyo lugha ya "unalazimisha". Mimi sijakulazimisha popote.

Kwa Katiba hiyo hiyo iliyopo sasa. Unataka kuniambia kwa vile hapatakuwepo na Katiba Mpya, ndiyo iwe sababu ya CHADEMA kutolenga kuunda serikali?
Na 'obviously' hakuna katiba mpya kabla ya 2025, kwa hiyo tafsiri yako hapa tayari ni kwamba CHADEMA waachane na lengo la kushika madaraka?
 
Maridhiano haya ni ubunifu wa CHADEMA na CCM ndio mtekelezaji.. Wengi wana wasiwasi kama huu wako, lakini CHADEMA ni chama chenye think tank kubwa sana na wasomi wenye weledi na maono ya kutosha sana

Kwa hatua hii ya kwanza tayari CHADEMA imeshatia mguu mmoja ndani ama kimjinimjini imeshaingiza kichwa ni hatua moja kubwa sana kwakuwa sasa CHADEMA itafanya siasa zake kwa uhuru bila woga wa kukamatwa. Kutekwa, kubambikiwa kesi. Kujeruhiwa na kudhulumiwa haki zake nyingi za msingi

Hatua ya pili na ya tatu zinakuja na mpaka 2025 CHADEMA itakuwa imeshamaliza kazi
Kuna vimatukio vidogo vidogo vinajengewa hoja nyepesi lakini CHADEMA haishughuliki navyo kwakuwa ilaeweza vipo kwa ajili ya kuwatoa kwenye reli na pia vinaletwa na wale wote waliochukizwa na haya maridhiano
Hivi ndio Maalim alivyokuwa anajiambia wakati anafanya maridhiano na CCM. Kilichofuata Jecha akafanya yake. Wapinzani hawatapewa hii nchi kwa kura wala maridhiano bali kwa ushawishi na nguvu ya umma. Ninaposema ushawishi ni pale unapoita maandamo na watu wakaja hata kama jeshi nzima limetandazwa nchi nzima. Kwasasa CDM haina ushawishi kama unavyodhani hamna kiongozi pale anaweza kuweka mgomo nusu ya nchi ikatekeleza agizo lake sasa nyie kaeni hapo jidanganyeni.
 
Dah!
Inalazimu wakati mwingine kukubaliana na hoja kama hizi.
Hivi ni sababu gani hasa CHADEMA wanapoteza ushawishi wa aina hiyo unaouelezea hapa?
Ni lazima patakuwepo na sababu maalum inayofanya wanachi wakose imani hiyo.

Na inawezekana kabisa, ni kutokana na utambuzi huo, ndiyo maana sasa CHADEMA wanataka wapate nafasi hii ya kupandia kwa Samia, ili na wao wawemo serikalini.

Na hii hali itazidi kuwa ngumu zaidi kwa CHADEMA hapo hata wanachama wao na mashabiki wa chama hicho watakapogundua kwamba viongozi wao wamekwishakengeuka. Hata wao wataanza kutelekeza chama.

Umegusia jambo muhimu sana hapa.
 
Nadhani wewe umekwishajiondoa kwenye kushiriki majadiliano kwa uelewa unachoshiriki. Imebaki tu kuingiza vimaneno tu.
Kwa hiyo ninakuweka pembeni hadi hapo utakapotuliza akili ujadili kwa utulivu wa akili na kuachana na mihemko.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] haya ndio madhara ya kuja na mada isiyo na locus standi, haina misingi ya kusimamia, umeleta hisia unazotaka zijadiliwe kama facts, ni kama vile ulilala usiku ukaota hii mada kisha ukaja nayo hapa bila kutafakari chochote kabla hujaandika.
 
Sijaona kipya cha kujibu, ila sasa ni kuzungushana tu.
Sema tu kiufupi hauna majibu, umeleta mada iliyojaa hisia, baada ya kuona nakubana umeamua kukimbia kijanja.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] haya ndio madhara ya kuja na mada isiyo na locus standi, haina misingi ya kusimamia, umeleta hisia unazotaka zijadiliwe kama facts, ni kama vile ulilala usiku ukaota hii mada kisha ukaja nayo hapa bila kutafakari chochote kabla hujaandika.
Sihitaji kujibu chochote hapa., kwa sababu hakuna cha kujibu.
 
Sema tu kiufupi hauna majibu, umeleta mada iliyojaa hisia, baada ya kuona nakubana umeamua kukimbia kijanja.
Sioni chochote "ulichobana", pengine hicho kimo akilini mwako tu!
 
Ni misingi ipi ya CHADEMA iliyowekwa pembeni katika hayo maridhiano? Huoni kwamba ni mapema sana ku-speculate hayo? Hatujasikia mabadiliko yoyote ya msimamo wa CHADEMA katika mambo makuu ya kisiasa, kiuchumi, kijamii ikiwemo utawala bora, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, “Covid-19”, n.k.

Ni ushauri mzuri kujipa muda tujionee ukweli wa maridhiano hayo kama tunajali mustakabali wa taifa.

Kwa wanaopenda msimamo wa late JPM wa kuviangamiza vyama vya upinzani haishangazi wao kutamani CHADEMA wawe na direct and total confrontational approach itakayowezesha vyombo vya dola kuangamiza viongozi, makada, wafuasi na chama kizima - literally. Enzi za Hitler ilijulikana kama Final Solution.
Huu ndio msingi wa hoja zake - Speculation.
 
Sioni chochote "ulichobana", pengine hicho kimo akilini mwako tu!
Wacha kujitoa akili makusudi na speculation zako!

Unachekesha unapowalaumu Chadema, halafu sehemu nyingine nikikusoma unaandika wacha muda uamue, mbona upo kama popo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nani Hana uhakika? Kwani hauoni tofauti kati ya siasa za JPM na Sasa? Umesikia Leo kwamba hakuna mpinzani atakamatwa maana hayo mambo zamani hayakuwepo. Ilikua mkutano wa Chadema lazima uzuiwe na Polisi.
Mbowe amekamatwa chini ya utawala upi ?
Kipindi Cha JPM Kuna mpinzani alikua na uhakika wa kushinda Jimbo au kata? So Ile ilikua ni motisha tosha kwa wapinzani kuhamia CCM Ili kusecure political future. Na ukweli wapinzani wengi mnoo walihamia CCM sio sababu ya kununuliwa Bali kuokoa political career.
Unafahamu bado waamuzi wa uchaguzi na matokeo ya uchaguzi Tanzania ni CCM kwa msaada wa vyombo vya dola.

Kwahiyo chaguzi za 2024 na 2025 mtashiriki ?
Sasa kwa kuangalia hizo scenario mbili, je kwanini Lissu au Mbowe wasihamie CCM ya 2020 ambayo Kulikua hakuna hope ya upinzani kupata uongozi ILA wahamie CCM ya 2023 ambapo upinzani una matumaini ya kubeba sio tu majimbo zaidi ya 100 Bali Dola kabisa???
Sijasema mbowe na Lissu wana hamia CCM 2023.

Narudia tena kwa hiyo chaguzi za 2024 na 2025 mtashiriki ?

Swali langu la katiba bado hujajibu .
 
Nani Hana uhakika? Kwani hauoni tofauti kati ya siasa za JPM na Sasa? Umesikia Leo kwamba hakuna mpinzani atakamatwa maana hayo mambo zamani hayakuwepo. Ilikua mkutano wa Chadema lazima uzuiwe na Polisi.

Kuhusu lini? Rais keshasema ataunda tume hivi karibuni Sasa si usubiri ikiundwa ndio uone kama katiba haitapatikana.

Ni either mjiunge na maridhiano au mtakufa kwa chuki tu maana there's no way tutarudi kwenye siasa za JPM. Nchi imeshakombolewa badilisheni mindset.
Uzuri au ubaya wa CCM bwana wanakupa Nyerere baadae wana kupa Mwinyi wanakupa tena Mkappa baadae wanakupa Jakaya wanakupa tena Magufuli baadae wanakupa Samia mwendo ni huo huo usiposoma nyendo zao vizuri lazima uumie.
 
Haya sio maridhiano bali hali ya mmoja wa washindani kukubali kushindwa na kuungana na washindani wake.......

Kwa macho ya kawaida inaonekana ni jambo jema lakini kwenye ulingo wa kisiasa ni kwamba CHADEMA inajichimbia kaburi lake.... kutokana na misingi ya kisiasa ya CHADEMA........

Bado nchi yetu Ina uhitaji wa siasa za CHADEMA kutokana na upuuzi na uozo wa serikali dhalimu......

Mimi kwa mtazamo wangu ni maridhiano haya hayakuzingatia maoni na utashi wa wananchi mbele ya safari.......
 
Wengi wanaweza kuibeza chadema kwa uwamuzi iliyochukuwa ,zaidi viongozi wao waandamizi kama Mbowe kwamba wamekubali ku compromise lakini ilikuwa hamna namna hii ndio njia peke kwa nchi kama Tanzania , mbinu inayoweza zaa matunda ,why? Viongozi walitoa maelekezo kufanyike maandamano kupinga uvunjwaji wa katiba unaofanywa na chama tawala waziwazi lakini watu ni waoga, na hakuna mfano Matokeo yake watu kama Mbowe na wengine wakafunguliwa mashtaka ya uongo, lengo likiwa na kuwatisha na ni kweli watu wote wanaodai ni wapenda mabadiliko wakatishika .Sasa kwa mazingira haya ya hapa Tanzania ni ngumu kupata reforms kwa kutumia people's power kama tunavyoona mataifa mengine sababu mataifa mengine wanachama wakiamua lao linakuwa lao wote sio pale viongozi wanapokuwa wamekamatwa bási na movements zote za kudai mabadiliko zinakuwa zimekoma.Mbowe na wezake wameamua kuja na initiatives nyingine ya kudai mabadiliko kulinga na mazingira na nature ya mtazania jinsi alivyo na ikiwa ni tofauti na jinsi ijulikanavo duniani kwa vyama vya upizani kutoku negotiate na chama tawala .Kamwe mabadiliko hayawezi kuja kwa kutegemea viongozi peke kwamba wao ndio wawe front alafu wa wanachama mpo kwenye sofa na smart phone mnalalama badala yake mnabidi strategy, no way out.
 
Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia vinaanza iliwakuta wachina wakiwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.. chama cha Kuomintang (KMT) kilikuwa kikipigana na kile cha kikomunisti (CCP), ikabidi wasitishe vita yao na kuungana kumpiga mjapani aliyekuwa kawavamia. Walipigana na mjapani kuanzia 1937 hadi 1945. Baada ya vita ya pili kwisha wachina wakarudi kwenye vita yao ya wenyewe kwa wenyewe hadi 1949 ambapo CCP walishinda.
Mapambano ya wakomunisti hayapaswi kufananishwa na hawa Chadema ni mbingu na ardhi.

Si sahihi kuwa vunjia heshima wakomunisti walio pambana kwa jasho na damu ili kukomboa nchi bila sarakasi za maridhiano ukifananisha struggling zao na hawa Chadema.
 
Back
Top Bottom