Ni misingi ipi ya CHADEMA iliyowekwa pembeni katika hayo maridhiano? Huoni kwamba ni mapema sana ku-speculate hayo? Hatujasikia mabadiliko yoyote ya msimamo wa CHADEMA katika mambo makuu ya kisiasa, kiuchumi, kijamii ikiwemo utawala bora, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, “Covid-19”, n.k.
Ni ushauri mzuri kujipa muda tujionee ukweli wa maridhiano hayo kama tunajali mustakabali wa taifa.
Kwa wanaopenda msimamo wa late JPM wa kuviangamiza vyama vya upinzani haishangazi wao kutamani CHADEMA wawe na direct and total confrontational approach itakayowezesha vyombo vya dola kuangamiza viongozi, makada, wafuasi na chama kizima - literally. Enzi za Hitler ilijulikana kama Final Solution.