Tofauti ya wapiga kura wa mitandaoni na wale wa box la kura ni;
1. Wa mitandaoni vipaumbele vyao ni kuwa na magari mazuri, nyumba nzuri na kusomesha watoto wao shule za gharama.
2. Wale wa box la kura ambao ndio wengi ni kuwa na uhakika wa maji, umeme, huduma za afya, uhakika wa masoko ya mazao, pamoja na uhakika wa watoto wao kusoma.
3. Wa mitandaoni vipaumbele vingine ni kuwa na mianya ya kupiga dili,kupiga rushwa, kupata kipato kisicho halali pamoja na kulipwa mishahara mikubwa kuliko ufanisi wao.
4. Wa box la kura vipaumbele ni kuzibwa mianya ya rushwa, kutoibiwa mazao yao na vyama vya ushirika, kuondolewa tozo zisizo za lazima za mazao na mifugo, uhakika wa amani na usalama.