TASK FORCE
JF-Expert Member
- Apr 7, 2017
- 2,465
- 3,459
mkuu watu hawaeleweki wanataka nini??! Ndiomaana Mungu alitutia adabu kwa kutuletea dikteta yule,Umeliweka vizuri Sana. Watanzania kuna nyakati hatujijui tunataka nini kwa kweli. Mungu anaipenda nchi yetu, ameonyesha namna ambavyo nchi yetu inaweza kupoteza utulivu kwa kuruhusu yule DIKTETA kututawala kwa miaka 5 na siku 114 kisha akaitoa roho yake. Ametupa Rais mtulivu, msikivu, mfuata utawala wa Sheria na anayemwogopa Mungu kwa matendo na siyo kwa mdomo kama Mwendazake.
Siku ni chini ya 100 toka amechukua nchi na kazi yake tunaiona kuanzia Uhuru wa kujieleza na kukosoa, mikutano ya ndani. ya vyama vya siasa, ajira za waalimi na watumishi wa afya, TRA kuacha dhuluma kwa wafanya biashara, kufutwa kwa kesi za kubambikiza, ujio wa wawekezaji, utayari wa kupambana na COVID 19 na kufunguka kwa dunia ya kidiplomasia.
Hakuna anayejua To Do List ya Rais SSH ina items gani japo mimi naamini la KATIBA MPYA lipo ni suala la wakati. Cha ajabu WAKOSOAJI wa Rais SSH wanamuona hajafanya kitu. Yaani watakapoona Katiba MPYA ndiyo watakubali.
Pengine niwakumbushe, kupata Katiba nzuri ni kitu kimoja na kuheshimu Katiba ni kitu kingine. Katiba hii mbovu ya sasa yule Mwendazake alikuwa anaivunja anavyotaka. Tumpongeze kwanza huyu Samia ambaye anaiheshimu pamoja na mapungufu yake.
Sasa mama Dawa yake Kama mijitu itaendelea kupinga pinga kila kitu iviivi, Bora awabane kila idara tu kmmmae, maana hatuna fadhila sisi