Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Dah,hii nchi kweli ngumu!!!!
Sijui mtu afanyaje ili kuwafurahisha aisee , mama ameeleza namna kwenye uongozi wake kuwa hatotaka Kodi ya dhulma, hatotaka kumuonea mtu, na ametoa uhuru wa kukosoa na pia kufungulia vyombo vya habari ambavyo vilifungiwa, ayo yote ni yale ambayo enzi za dikteta yalikosekana,
Leo Chadema inazunguka mikoani kufanya mikutano ya ndani,hatujasikia hata purukushani za kuvamiwa na polisi, na mengineyo mengi,

Sasa mnataka mtu wa namna gani!?? Na mama ana siku mia tu tayari mshaanza kusema hafai
Watanzania kulalamika ndio jadi yetu, ni udhaifu wetu.
 
Wewe dogo ni mlalamishi sana
Una ufinyu wa akili wewe! Huyo msaliti Ayatollah Zitto aliyefukuzwa Chadema kwa kuchukua mikakati ya chama uchaguzi wa 2010 na kuipeleka ccm unaweza kumuita mpinzani?
Huyo aliyekuwa busy kuongea na Rostam miezi michache kabla ya uchaguzi wa 2010 akitoa siri za mipango ya chama kisha alipoulizwa namba yake ya simu ilikuwa inaongea na namba ya Rostam walikuwa wanaongea nini? Akabaki kung’ang’ania macho!?
Akaulizwa hii ni namba yako au si namba yako? Jibu lake ni namba yangu lakini sijaitumia miezi mingi sana. Swali sasa hiyo simu umempa mtu mwingine? Hapana. Je, imejipiga yenyewe kwenda kwa Rostam? Hapana. Sasa mlikuwa mnaongea na Rostam kitu gani miezi miwili kabla ya uchaguzi!!!?
KIMYAAAAAA! Usiandike ujinga wako humu kuhusu ACT Wazalendo AKA ACT Wasaliti.
 
Mkuu Uttoh2002, unafikiri Mshana ni ccm?! Tuna tatizo kubwa JF, kuna wakati tuna paswa kufikiri nje ya mabox ya ccm vs CHADEMA, kwa masilahi mapana ya nchi yetu!

Mimi I don’t care about CCM au chadema au ujinga wowote, jibu hizo bulletins hapo! Maana na wewe umeacha hizo bulletins umeenda kwenye vyama!
 
Lakini si aliwahi kuwa mbunge vipindi viwili? Kwenda kula.bata huko nje huenda ulikuwa mpango mkakati ili atimuliwe aingie upande wapili, {mawazo yangu lakini}

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Nyinyi huwa hamna jema wala shukran.

Jiwe ndio aliwajua vyema na ndio maana akawafanyia alivyowafanyia. JK aliwaeka karibu na kuamini kwamba Tanzania ni yetu sote lakini shukran yenu ni matusi kwake.

Hata mfanyiwe nini nyinyi hamtokaa mshukuru kwamba angalau mmepata rais anaeskiliza maoni na kujali kwamba sote ni Watanzania. Mmekalia lawama juu ya lawama juu ya lawama.

Muwe na staha na busara na muache huu ujinga wenu dhidi ya rais.

Yaani tatizo ni kuteuliwa Nassari???? Huku hampo na kule hampo
Kinachojadiliwa ni jinsi ambavyo CCM ilivyokosa watu hadi kufikia hatua ya kuteua wakuu wa wilaya wapinzani mliowabeza few days ago?
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
Mama kama kuna aliowateua basi labda ni watano tu , mkeka ameletewa tu mezani , nina hakika 95% ya wateule hawajui .

Sasa ni nani kampa majina ?
 
Umesema yote it’s beyond me kwenye,kuwaelewa hawa viazi.

Wafuasi wa CDM ovyo kweli kweli; we need to asses their to asses their mental ability.
Ni ukosefu tu wa akili ndio unawasumbua hawa watu.

Huu uteuzi umewauma sana! Walitamani kuona kina Lijuakali wanaendelea kusota.

Lakini kina Nayarandu walipohamia kwao walipewa vyeo fasta fasta na wakashangilia na kuita hiyo ndio democrasia.

Mbowe anaendelea kukaa pale kwa ujinga wa wafuasi wake.
 
Hamna lolote mkuu, hamnaga hoja wala agenda iliyo na malengo ya kitaifa. Nyinyi ni kupinga tu kila lifanywalo.

Hamuwezi kukaa kimya mbona kipindi cha jiwe mliufyata?? Shukuruni kwamba Marais waislam wana hekma na busara.

Kwa kutumia hizo hizo kodi zenu jiwe alifanya anavyotaka na mliufyata kimyaaaa hakuna cha kodi zenu wala nini.

Muwe na staha na busara na muache huu ujinga wenu dhidi ya Rais.
Well said Mkuu
 
Labda tukisema upinzani wa nchi hii tunakosea. Mbona @ACT Wazale@ACT ni wapinzania lakini wanakosoa, kushauri na kushiriki kwa staha???

Hiki kikundi cha watu lengo lake ni kuingia tu madarakani hata kwa ghiliba, fujo, au hata kwa damu.

Hawana jema hawa, tulipiga kelele weeee kwamba vijana washirikishwe, Leo vijana wanashirikishwa bado wanapiga kelele only because hawateuliwi wao. Yaani wao lazima wateuliwe wao tu.

Watakwambia kuhubiri na kuzunguka nchi nzima sio hisani, lakini kwa miaka mitano waliufyata hawa.

Time yao inakuja na ikifika hatutotaka kuskia malalamiko.
Ajabu sana. Vijana tulipiga kelele sana kwanba wazee waliochoka wanateuliwa vyeo mbalmbal huku vijana wakiachwa. Vijana wameteuliwa tena tunalia tunasema hawana uzoefu wateuliwe wazee.
Wapinzan wamepewa uhuru wa kufanya wakitakacho lkn sasa hawamtak aliewapa uhuru.

Nasema hivi mama fuata Magufuli style hawa watu wapigwe pin mikutano mpaka uchaguzi mkuu. Ukiwachekea hawa watu utajikuta wamekupiga na viatu wakidai ni uhuru wao.

Nilimchukia jiwe kwa kuwanyima uhuru lkn nasema am sorry Jiwe, hawa watu uliwajua sana. Uliwabana p**u na hakuna kitu walikufanya. Ulitumia kodi zao kuwapelekea moto nao wakaufyata mpka sasa ndo wameinua vichwa.

Believe me, wapinzani wakivhukua nchi hakuna kitu watafanya. Hata hilo la katiba mpya wataachana nalo. Na hawa nk wafalme wapendao kutukuzwa wala hawatak kupingwa.
 
Rais Samia Suluhu Hassan alipata kutuambia awamu hii anatekeleza yote aliyokua yamepangwa kutekelezwa na JPM yeye akiwa makumu, pamija na kuboresha kunakohitajika

Sijui kwanini kuna watu hawamuelewi






Chuma JPM alinoa chuma SSH

Alale salama kipenzi chetu John Pombe Magufuli

Mungu ibariki Tanzania, Mungu tulindie Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan

Sidhani kama iliwahi kutokea ulinzi wa Rais wa Tanzania ukawa tatizo,tatizo ni pale tunapomlinda na asitekeleze kile wananchi wanataka akafanye naye akatenda atakayo yeye au chama chake.
 
Ajabu sana. Vijana tulipiga kelele sana kwanba wazee waliochoka wanateuliwa vyeo mbalmbal huku vijana wakiachwa. Vijana wameteuliwa tena tunalia tunasema hawana uzoefu wateuliwe wazee.
Wapinzan wamepewa uhuru wa kufanya wakitakacho lkn sasa hawamtak aliewapa uhuru.

Nasema hivi mama fuata Magufuli style hawa watu wapigwe pin mikutano mpaka uchaguzi mkuu. Ukiwachekea hawa watu utajikuta wamekupiga na viatu wakidai ni uhuru wao.

Nilimchukia jiwe kwa kuwanyima uhuru lkn nasema am sorry Jiwe, hawa watu uliwajua sana. Uliwabana p**u na hakuna kitu walikufanya. Ulitumia kodi zao kuwapelekea moto nao wakaufyata mpka sasa ndo wameinua vichwa.

Believe me, wapinzani wakivhukua nchi hakuna kitu watafanya. Hata hilo la katiba mpya wataachana nalo. Na hawa nk wafalme wapendao kutukuzwa wala hawatak kupingwa.
Nakubaliana nawe mkuu.

Hawa watu nina mashaka na agenda zao.
 
Nyinyi huwa hamna jema wala shukran.

Jiwe ndio aliwajua vyema na ndio maana akawafanyia alivyowafanyia. JK aliwaeka karibu na kuamini kwamba Tanzania ni yetu sote lakini shukran yenu ni matusi kwake.

Hata mfanyiwe nini nyinyi hamtokaa mshukuru kwamba angalau mmepata rais anaeskiliza maoni na kujali kwamba sote ni Watanzania. Mmekalia lawama juu ya lawama juu ya lawama.

Muwe na staha na busara na muache huu ujinga wenu dhidi ya rais.

Yaani tatizo ni kuteuliwa Nassari???? Huku hampo na kule hampo
Ndugu,
Nyerere aliwahi kumteua na kumtangaza Chediel Mgonja kuwa RC. Waziri Mkuu Sokoine na Waziri wa Sheria Warioba wakamwendea na kumshauri kwani alikuwa amevuliwa ubunge wake na Mahakama kutokana na kutoa rushwa. Pamoja na Nyerere kuonekana kuwa alimpenda sana Mgonja alitengua uteuzi huo ndani ya siku mbili.
Inavyoonekana ni kuwa, Mama yuko peke yake katika juhudi za kufuta nyayo za UDHALIMU. Wengi wa aliyonao hawamsaidii; kwani sio wakweli ILA ni wachumia tumbo waliyokwisha zoea na kunogewa kuishi kwa kujichekesha na kujipendekeza, muda wote kwa lolote. Hawana ujasiri wa kukosoa wala kutoa hoja za kurekebisha penye madosari hata ya wazi.
Hiyo ndio LEGACY aliyoiacha Mwendazake HASA kwa wenye unyonge wa moyo.
Mungu ataendelea kuwalinda wanaothamini HAKI.
AMEN
 
Na mkiendelea hivi hiyo habari ya mikutano na the so called wapinzani wa kweli itapotelea hewani. Haina hata haja ya kuwakaribisha.

Sisi tutamkumbusha aachane na hizo habari maana Mheshimiwa Kikwete alifanya hivyo na hakuna tija yoyote iliyopatikana law kukutana na hao wanaojiita wapinzani wa kweli. Zaidi zaidi walikwenda tu kunywa chai ikulu na kuongeza gharama zisizo za msingi.

Kwa tabia zenu hizi Wallahi haya mambo ya katiba mpya na tume huru pia yanaweza yakapeperuka na to be honest my friend hamna mtakaloweza kumfanya mama. Ni hisani na busara zake tu. Ni mapenzi yake kwa taifa lake tu, hivyo musitake kumvuruga.

Eti anatoka mtu na kusema hatuwezi kumbembeleza na tutapaza sauti. You are not being realistic.

Muwe na staha wakuu
Umeliweka vizuri Sana. Watanzania kuna nyakati hatujijui tunataka nini kwa kweli. Mungu anaipenda nchi yetu, ameonyesha namna ambavyo nchi yetu inaweza kupoteza utulivu kwa kuruhusu yule DIKTETA kututawala kwa miaka 5 na siku 114 kisha akaitoa roho yake. Ametupa Rais mtulivu, msikivu, mfuata utawala wa Sheria na anayemwogopa Mungu kwa matendo na siyo kwa mdomo kama Mwendazake.

Siku ni chini ya 100 toka amechukua nchi na kazi yake tunaiona kuanzia Uhuru wa kujieleza na kukosoa, mikutano ya ndani. ya vyama vya siasa, ajira za waalimi na watumishi wa afya, TRA kuacha dhuluma kwa wafanya biashara, kufutwa kwa kesi za kubambikiza, ujio wa wawekezaji, utayari wa kupambana na COVID 19 na kufunguka kwa dunia ya kidiplomasia.

Hakuna anayejua To Do List ya Rais SSH ina items gani japo mimi naamini la KATIBA MPYA lipo ni suala la wakati. Cha ajabu WAKOSOAJI wa Rais SSH wanamuona hajafanya kitu. Yaani watakapoona Katiba MPYA ndiyo watakubali.

Pengine niwakumbushe, kupata Katiba nzuri ni kitu kimoja na kuheshimu Katiba ni kitu kingine. Katiba hii mbovu ya sasa yule Mwendazake alikuwa anaivunja anavyotaka. Tumpongeze kwanza huyu Samia ambaye anaiheshimu pamoja na mapungufu yake.
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.

Bro wangu tumekuwa wote muda mrefu sana hapa JF. Lkn kitu ambacho nimegundua ni kuwa viongozi wote ambao wamepita tukiwa wote hapa JF umekuwa ukiwapinga. Kuanzia Kikwete, JPM mpaka SSH, wote unawapinga. Je umepata kujiuliza nini tatizo? Mfumo au mtu mwenyewe binafsi?
Nionavyo mimi tuangalie uwezo wao, na si mapungufu yao. Kwa maana viongozi wetu hawa ni binadamu kama wewe. Hawatokei MBINGUNI kama malaika. Kwa hiyo tusiwe na mtazamo wa kuwachambua tu, kana kwamba sisi tunaweza kufanya kila jambo bila makosa.
 
Back
Top Bottom