Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Hivi ndivyo watu walivyochambua na kupinga uteuzi wa Joshua Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya.

View attachment 1825048

View attachment 1825050
Kama ndani ya maccm kuna wanaomtetea yule jambazi na muuaji basi chama hicho hakistahili kuwepo madarakani kwani sasa ni genge la majambazi na wauaji ambao wako tayari kufanya maovu ya kila aina ili kujikusanyia utajiri haramu na kuua ili kuendelea kung’ang’ania madaraka.
Huyo Jiwe ndio hopeless kabisa.

Hatuhitaji kubembeleza mtu kutimiza wajibu wake kwani hii kazi waliomba wenyewe na wanalipwa vizuri sana kufanya hii kazi hivyo ni wajibu wao kufanya wanachotakiwa kukifanya.

Hizo ni kodi zetu hatuwezi kukaa kimya kuona zinatumika vibaya.
Some of the few hopeless arguments!
Ukishindwa kulima korosho huwezi kuwa mvuvi? Ukishindwa kufuga kuku huwezi kuwa muuza maji. Yaani akishindwa kazi ya ubunge hawezi kuwa mkuu wa wilaya. Is there any synonymity between the two?
Again, hopeless!
 
Kashasema Katiba si kipaumbele chake kwa sasa mkuu.

Ila asinukukuliwe kimakosa. Mama mswahili yule. Alisema hivi:

"Hili la katiba mpya tupeane muda kwanza."

Kauli hii ni tofauti na aliye kwenda zake. Kwani yule ndiyo rasmi alitamka kuwa la katiba yeye hakuahidi.

Hata hivyo Mama asituchukulie poa.
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
Hata akija malaika akatawala kupitia CCM kwa katiba hii bado hatotoshea hicho cheo
 
Rais Samia Suluhu Hassan alipata kutuambia awamu hii anatekeleza yote aliyokua yamepangwa kutekelezwa na JPM yeye akiwa makumu, pamija na kuboresha kunakohitajika

Sijui kwanini kuna watu hawamuelewi






Chuma JPM alinoa chuma SSH

Alale salama kipenzi chetu John Pombe Magufuli

Mungu ibariki Tanzania, Mungu tulindie Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan

Dada yangu,
Yaonyesha kuwa bado unayo mapenzi makubwa kwa Mwendazake, kwa upande mmoja hilo laweza lisiwe kosa.
Lakini KOSA ni kuwa wa kushangilia na kushabikia kila kitokacho kwake hata pale ilipokuwa dhahiri kuwa KAKOSEA.
Maadam madhara yake yalikwishaonekana, basi kama twataka kweli kupiga hatua, kama Taifa, itakuwa sio busara kujivunia kuendelea kuyafanya makosa yaleyale.
 
Sidhani kama iliwahi kutokea ulinzi wa Rais wa Tanzania ukawa tatizo,tatizo ni pale tunapomlinda na asitekeleze kile wananchi wanataka akafanye naye akatenda atakayo yeye au chama chake.

Ulinzi huo vipi🙄
 
Sidhani kama mama anajifanyia mwenyewe. Kuna wajinga wanampangia huyu anafaa na huyu hafai, mf huyo nassari. Mama asiwasikilize hao.


Na katiba mpya iliyoachwa na kikwete kwa mwendazake aipitishe.
 
Ndugu,
Nyerere aliwahi kumteua na kumtangaza Chediel Mgonja kuwa RC. Waziri Mkuu Sokoine na Waziri wa Sheria Warioba wakamwendea na kumshauri kwani alikuwa amevuliwa ubunge wake na Mahakama kutokana na kutoa rushwa. Pamoja na Nyerere kuonekana kuwa alimpenda sana Mgonja alitengua uteuzi huo ndani ya siku mbili.
Inavyoonekana ni kuwa, Mama yuko peke yake katika juhudi za kufuta nyayo za UDHALIMU. Wengi wa aliyonao hawamsaidii; kwani sio wakweli ILA ni wachumia tumbo waliyokwisha zoea na kunogewa kuishi kwa kujichekesha na kujipendekeza, muda wote kwa lolote. Hawana ujasiri wa kukosoa wala kutoa hoja za kurekebisha penye madosari hata ya wazi.
Hiyo ndio LEGACY aliyoiacha Mwendazake HASA kwa wenye unyonge wa moyo.
Mungu ataendelea kuwalinda wanaothamini HAKI.
AMEN
AMEN
 
Umeliweka vizuri Sana. Watanzania kuna nyakati hatujijui tunataka nini kwa kweli. Mungu anaipenda nchi yetu, ameonyesha namna ambavyo nchi yetu inaweza kupoteza utulivu kwa kuruhusu yule DIKTETA kututawala kwa miaka 5 na siku 114 kisha akaitoa roho yake. Ametupa Rais mtulivu, msikivu, mfuata utawala wa Sheria na anayemwogopa Mungu kwa matendo na siyo kwa mdomo kama Mwendazake.

Siku ni chini ya 100 toka amechukua nchi na kazi yake tunaiona kuanzia Uhuru wa kujieleza na kukosoa, mikutano ya ndani. ya vyama vya siasa, ajira za waalimi na watumishi wa afya, TRA kuacha dhuluma kwa wafanya biashara, kufutwa kwa kesi za kubambikiza, ujio wa wawekezaji, utayari wa kupambana na COVID 19 na kufunguka kwa dunia ya kidiplomasia.

Hakuna anayejua To Do List ya Rais SSH ina items gani japo mimi naamini la KATIBA MPYA lipo ni suala la wakati. Cha ajabu WAKOSOAJI wa Rais SSH wanamuona hajafanya kitu. Yaani watakapoona Katiba MPYA ndiyo watakubali.

Pengine niwakumbushe, kupata Katiba nzuri ni kitu kimoja na kuheshimu Katiba ni kitu kingine. Katiba hii mbovu ya sasa yule Mwendazake alikuwa anaivunja anavyotaka. Tumpongeze kwanza huyu Samia ambaye anaiheshimu pamoja na mapungufu yake.
Well said bro.

Na binaadam sote tuna mioyo na sio malaika. Hata Sisi tunataka katiba mpya na bora, upo uzi wangu humu nimelizungumzia hili. Lakini hatuwezi kudai katiba kwa jeuri na maneno yasiyo staha. Mpaka sasa Mheshimiwa rais amefanya so much already, inapotokea wapumbavu wachache wanakejeli juhudi hizi wanaweza wakamfanya Mama akafikiria tofauti.

Ndio maana nkawaambia, Mama anaweza asilishughulikie na HAKUNA tena HAKUNA chochote tutakachomfanya.
 
Back
Top Bottom