Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Huyu Mama ni tatizo na ameamua kurithi na kuyaenzi baadhi ya mambo ya yasiyofaa ya Mwendazake yaliyotuharibia hii nchi.

Kwa kifupi, hatoshi na bora muda wake uishe aondoke.

Hata Katiba Mpya sidhani kama itakuwa ni moja ya vipaumbele vyake kwani inaonekana ameanza kufurahia hii katiba mbovu inayompa mamlaka makubwa ya kufanya atakavyo.
😀 😀 😀 Ninyi si ndio mlikuwa mnamsifu kwa pambio na vigelegele kuwa ameanza vizuri leo hafai tena?.Acheni uzandiki.
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
Huyu atamaliza miaka 4 bila kufanya cha maana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa style hii upinzani tusahau kuchukua nchi maana tunakaa kumshangilia Rais wa CCM badala ya kujenga kwetu.
😀 😀 Eti kuchukua nchi,nchi ipi?. Labda nchi ya machame nkuu kati ndio mkachukue ila sio mama Tanzania. Mchukue nchi kwa upinzani huu utopolo, hilo jambo ni njozi za mchana.
 
Ishu si hao hawana shukrani mimi sina chama cha siasa lakini mtu akiacha ubunge kwa kutokuudhuria vikao vya bunge unampaje nafasi ya ukuu wa wilaya Mama anaweza kuwa vizuri lakini anapokosea usiweke upofu kisa ni Mama wanaomsaidia teuzi wanazingua sana hii ni kweli
Hili ni suala pana mkuu. Kila mtu atalizungumzia kinamna yake. Chadema ndio wapo mitandaoni kupigia kelele huu uteuzi wa Nassari.

Je mtu akifeli biashara ya Mihogo ndio hafai kuajiriwa kuwa afisa Tarafa??
Lakini wao Chadema alipokuwa akifanya mambo hayo hawakumuona?? Je walimchukulia hatua gani???
 
😀 😀 Eti kuchukua nchi,nchi ipi?. Labda nchi ya machame nkuu kati ndio mkachukue ila sio mama Tanzania. Mchukue nchi kwa upinzani huu utopolo, hilo jambo ni njozi za mchana.
Matokeo ya Kisiasa yanataka Moyo Sana vijana wa CCM tulieni au hamieni Upinzani..... Nchi ni Yetu Sote, tupunguze kuchukiana na Kuumizana kimwili!!

Moses Machali, DC
David Kafulila, RC
Mwita Waitara, Naibu Waziri
Joshua Nassari, DC
Fakii Lulandala, DC
Julius Mtatiro, DC
Albert Msando, DC
David Silinde, Naibu Waziri,
Vincent Mashinji, DC
Mwambe, MB
Gekuli, Naibu Waziri
Juliana Shonza, MB
Patrobasi Katambi, N/W
Lijua Likali, DC
Covid 19
UVCCM mnajifunza nini toka kwa Vijana waliojengwa na CHADEMA wakaiponda CCM, Wamechukuliwa kuisaidia CCM📝

Sasa endelea kusema upinzani utopolo mjinga mkubwa wewe. Laiti ingekuwa utopolo si mngechukuliwa nyie waimba mapambio na kujamba mitandaoni na kwenye mikutano ya siasa? Mbona viongozi mnakosa mnachukua ambao tumewalea na kuwakuza kisiasa sisi? Amka sio unaongea tu.
 
Ooh basi fahamu mie sio MATAGA na simuelewi kabisa huyu mama only the difference ni kwamba yeye sio katili
Kwa nini humuelewi?,hayuko hapo kusaidia upinzani,anajua kwa kuwapa kina juakali nafasi,2025 cdm wengi watavutika kwenda ccm,,siasa ni strategy,,unadhani angewaacha nani mwanachadema atatamani kwenda ccm tena?
 
Siyo kweli, hiyo ni dhana tu! Lakini pia Wachaga ni wachapa kazi sana, mfano Reginald Meghi, na kama ukifanikiwa kufika Arusha na Kilimanjaro, utakubaliana na mimi! Kuna Wachaga wengi CHADEMA, lakini makabila mengine wapo pia, hata Wasukuma! Na pia, muhimu sana, kuna Wachaga wengi sana ccm!
Hili la uchapakazi sikatai, maana niko huku pia

Ila haibadilishi uhalisia kwamba mna ka ubinafsi, kujihisi bora kuliko wengine n. K, wakati hao mnaowaona duni wanawahifadhi huko kwao bila kuchunguza mnatoka wapi.
 
Huwezi kupata Urais bila kupitia chama cha siasa,,so lazima mazingira wezeshi yawekwe
Vyovyote iwavyo, akishapatikana anasimamia na kuapa kuwatumikia watanzania wote bila kujali vyama vyao mkuu
 
Wewe unaona uteuzi wa nassar ni sawa?
Maoni yangu doesn't matter mkuu especially baada ya kuwa mtu ameshateuliwa.

Mama ndio anajua Mheshimiwa Joshua Nassari atamsaidia vipi.

Ndio maana tunasisitiza kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
 
We pumbavu kweli eti sabaya wamemtengenezea makosa!kwani cdm Ni Dpp?
Mkuu kumsikia tuSabaya umepanick 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Hivi DPP akiamua kumuachia kwamba hana hatia si mtakufa nyinyi duh

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mansa Musa, Mfalme tajiri sana wa Mali, alivyokuwa katika safari yake kwenda kuhiji Mecca, mwaka 1324 alifika Cairo Misri. Mwaka huo alitoa sadaka ya dhahabu nyingi sana Cairo, mpaka akashusha bei ya dhahabu.

Katika msafara wake huo, muandishi mmoja wa habari na historia maarufu wa Misri, alimuuliza. Mfalme, ulipataje kuwa Mfalme?

Mansa Musa akamjibu. Akamwambia kwamba, kabla yangu alikuwapo mflame mwingine, aliyeitwa Abubakar II. Abubakar alipenda sana kuchunguza vyanzo vya mambo. Mfalme Abubakar akasema, kama vile mto huu (Niger) ulivyo na ng'ambo ya pili yenye nchi kavu, vivyo hivyo hata bahari (Atlantic) ina ng'ambo ya pili yenye nchi kavu.

Mfalme Abubakar akajaza mamia ya mashua vyakula na maji, na vijakazi mbalimbali, waende kutazama kama upande wa pili wa bahari kuna nchi kavu.

Wale watu wakaenda, mashua ya mwisho ikarudi kutoa habari, kwamba walifika sehemu baharini kuna mawimbi makubwa kama maghorofa.

Mfalme Abubakar alivyosikia hivyo, akasema safari hii nitaenda mwenyewe nijionee. Akapanga vijakazi wake, mamia ya mashua, vyakula na maji. Akamuweka Mansa Musa kuwa mfalme wa muda wakati yeye yupo safarini.Akaenda baharini. Baada ya hapo hakuonekana tena.

Watu wa Mali walichukulia jambo lile kama la aibu sana. Kwamba Mflame wao amewatelekeza. Wakaenda kwenye vitabu vinavyoweka rekodi za Wafalme wa Mali, wakalifuta jina la Mansa Abubakar II.

Kisa hiki kinatufundisha nini?

A king abdicating his duties is a serious thing. Serious enough to be stricken off the records in the ancient Mali rosters.

Mbunge anapoomba kura, anaomba kupewa heshima kubwa sana. Akijiuzulu bila sababu ya msingi wajibu huu, amejionesha kuwa hafai uongozi wa umma.

Kwa sasa, sitaki kumpangia rais nani wa kumteua, kwa sababu ni haki yake ya kikatiba na kisheria.

Ila, nahoji ufanisi wa kuteua watu ambao walishajiuzulu uongozi wa umma bila sababu muhimu. Na zaidi, nahoji kama hivi vyeo inawezekana vikajazwa vizuri kwa watu kugombea badala ya kuteuliwa.

Na zaidi, kama kuna mbunge kachaguliwa na watu, mkuu wa wilaya anahitajika kufanya nini?
huu jamaa anaitwa relief asome hapa ishu si kumpangia raisi ishu ni je raisi kwanini anachukua aina hii ya watu kama nassari na kufanya nao kazi

mfano mimi binafsi yangu mtu akimsifu magufuli kinamna yeyote namuona hafai sababu magufuli anakuwa vipi msafi na huku alimteua sabaya kuwa mkuu wa wilaya na kuamua kufanya kazi naye
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
I have spent time reviewing your presentations and comments, you often have a point. But it would have hold much sense if it was not competitive politics.
CCM shall never, never be a constructive engagement (allie) partner to Chadema.

You are politically an enemy to CCM, your friend is an enemy to CCM, your irritant is a refreshment to CCM.

Never expect CCM to listen to you on any issue unless it gives mileage to CCM. CCM will always do things which must irritate Chadema or rather opposition.

This is competitive politics, the reverse is true. Chadema ought to do the same. Parties are not working to complementing the other but competing.
 
Back
Top Bottom