Mansa Musa, Mfalme tajiri sana wa Mali, alivyokuwa katika safari yake kwenda kuhiji Mecca, mwaka 1324 alifika Cairo Misri. Mwaka huo alitoa sadaka ya dhahabu nyingi sana Cairo, mpaka akashusha bei ya dhahabu.
Katika msafara wake huo, muandishi mmoja wa habari na historia maarufu wa Misri, alimuuliza. Mfalme, ulipataje kuwa Mfalme?
Mansa Musa akamjibu. Akamwambia kwamba, kabla yangu alikuwapo mflame mwingine, aliyeitwa Abubakar II. Abubakar alipenda sana kuchunguza vyanzo vya mambo. Mfalme Abubakar akasema, kama vile mto huu (Niger) ulivyo na ng'ambo ya pili yenye nchi kavu, vivyo hivyo hata bahari (Atlantic) ina ng'ambo ya pili yenye nchi kavu.
Mfalme Abubakar akajaza mamia ya mashua vyakula na maji, na vijakazi mbalimbali, waende kutazama kama upande wa pili wa bahari kuna nchi kavu.
Wale watu wakaenda, mashua ya mwisho ikarudi kutoa habari, kwamba walifika sehemu baharini kuna mawimbi makubwa kama maghorofa.
Mfalme Abubakar alivyosikia hivyo, akasema safari hii nitaenda mwenyewe nijionee. Akapanga vijakazi wake, mamia ya mashua, vyakula na maji. Akamuweka Mansa Musa kuwa mfalme wa muda wakati yeye yupo safarini.Akaenda baharini. Baada ya hapo hakuonekana tena.
Watu wa Mali walichukulia jambo lile kama la aibu sana. Kwamba Mflame wao amewatelekeza. Wakaenda kwenye vitabu vinavyoweka rekodi za Wafalme wa Mali, wakalifuta jina la Mansa Abubakar II.
Kisa hiki kinatufundisha nini?
A king abdicating his duties is a serious thing. Serious enough to be stricken off the records in the ancient Mali rosters.
Mbunge anapoomba kura, anaomba kupewa heshima kubwa sana. Akijiuzulu bila sababu ya msingi wajibu huu, amejionesha kuwa hafai uongozi wa umma.
Kwa sasa, sitaki kumpangia rais nani wa kumteua, kwa sababu ni haki yake ya kikatiba na kisheria.
Ila, nahoji ufanisi wa kuteua watu ambao walishajiuzulu uongozi wa umma bila sababu muhimu. Na zaidi, nahoji kama hivi vyeo inawezekana vikajazwa vizuri kwa watu kugombea badala ya kuteuliwa.
Na zaidi, kama kuna mbunge kachaguliwa na watu, mkuu wa wilaya anahitajika kufanya nini?