Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Watanzania kulalamika ndio jadi yetu, ni udhaifu wetu.
 
Wewe dogo ni mlalamishi sana
 
Mkuu Uttoh2002, unafikiri Mshana ni ccm?! Tuna tatizo kubwa JF, kuna wakati tuna paswa kufikiri nje ya mabox ya ccm vs CHADEMA, kwa masilahi mapana ya nchi yetu!

Mimi I don’t care about CCM au chadema au ujinga wowote, jibu hizo bulletins hapo! Maana na wewe umeacha hizo bulletins umeenda kwenye vyama!
 
Lakini si aliwahi kuwa mbunge vipindi viwili? Kwenda kula.bata huko nje huenda ulikuwa mpango mkakati ili atimuliwe aingie upande wapili, {mawazo yangu lakini}

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kinachojadiliwa ni jinsi ambavyo CCM ilivyokosa watu hadi kufikia hatua ya kuteua wakuu wa wilaya wapinzani mliowabeza few days ago?
 
Mama kama kuna aliowateua basi labda ni watano tu , mkeka ameletewa tu mezani , nina hakika 95% ya wateule hawajui .

Sasa ni nani kampa majina ?
 
Umesema yote it’s beyond me kwenye,kuwaelewa hawa viazi.

Wafuasi wa CDM ovyo kweli kweli; we need to asses their to asses their mental ability.
Ni ukosefu tu wa akili ndio unawasumbua hawa watu.

Huu uteuzi umewauma sana! Walitamani kuona kina Lijuakali wanaendelea kusota.

Lakini kina Nayarandu walipohamia kwao walipewa vyeo fasta fasta na wakashangilia na kuita hiyo ndio democrasia.

Mbowe anaendelea kukaa pale kwa ujinga wa wafuasi wake.
 
Well said Mkuu
 
Ajabu sana. Vijana tulipiga kelele sana kwanba wazee waliochoka wanateuliwa vyeo mbalmbal huku vijana wakiachwa. Vijana wameteuliwa tena tunalia tunasema hawana uzoefu wateuliwe wazee.
Wapinzan wamepewa uhuru wa kufanya wakitakacho lkn sasa hawamtak aliewapa uhuru.

Nasema hivi mama fuata Magufuli style hawa watu wapigwe pin mikutano mpaka uchaguzi mkuu. Ukiwachekea hawa watu utajikuta wamekupiga na viatu wakidai ni uhuru wao.

Nilimchukia jiwe kwa kuwanyima uhuru lkn nasema am sorry Jiwe, hawa watu uliwajua sana. Uliwabana p**u na hakuna kitu walikufanya. Ulitumia kodi zao kuwapelekea moto nao wakaufyata mpka sasa ndo wameinua vichwa.

Believe me, wapinzani wakivhukua nchi hakuna kitu watafanya. Hata hilo la katiba mpya wataachana nalo. Na hawa nk wafalme wapendao kutukuzwa wala hawatak kupingwa.
 
Sidhani kama iliwahi kutokea ulinzi wa Rais wa Tanzania ukawa tatizo,tatizo ni pale tunapomlinda na asitekeleze kile wananchi wanataka akafanye naye akatenda atakayo yeye au chama chake.
 
Nakubaliana nawe mkuu.

Hawa watu nina mashaka na agenda zao.
 
Ndugu,
Nyerere aliwahi kumteua na kumtangaza Chediel Mgonja kuwa RC. Waziri Mkuu Sokoine na Waziri wa Sheria Warioba wakamwendea na kumshauri kwani alikuwa amevuliwa ubunge wake na Mahakama kutokana na kutoa rushwa. Pamoja na Nyerere kuonekana kuwa alimpenda sana Mgonja alitengua uteuzi huo ndani ya siku mbili.
Inavyoonekana ni kuwa, Mama yuko peke yake katika juhudi za kufuta nyayo za UDHALIMU. Wengi wa aliyonao hawamsaidii; kwani sio wakweli ILA ni wachumia tumbo waliyokwisha zoea na kunogewa kuishi kwa kujichekesha na kujipendekeza, muda wote kwa lolote. Hawana ujasiri wa kukosoa wala kutoa hoja za kurekebisha penye madosari hata ya wazi.
Hiyo ndio LEGACY aliyoiacha Mwendazake HASA kwa wenye unyonge wa moyo.
Mungu ataendelea kuwalinda wanaothamini HAKI.
AMEN
 
Umeliweka vizuri Sana. Watanzania kuna nyakati hatujijui tunataka nini kwa kweli. Mungu anaipenda nchi yetu, ameonyesha namna ambavyo nchi yetu inaweza kupoteza utulivu kwa kuruhusu yule DIKTETA kututawala kwa miaka 5 na siku 114 kisha akaitoa roho yake. Ametupa Rais mtulivu, msikivu, mfuata utawala wa Sheria na anayemwogopa Mungu kwa matendo na siyo kwa mdomo kama Mwendazake.

Siku ni chini ya 100 toka amechukua nchi na kazi yake tunaiona kuanzia Uhuru wa kujieleza na kukosoa, mikutano ya ndani. ya vyama vya siasa, ajira za waalimi na watumishi wa afya, TRA kuacha dhuluma kwa wafanya biashara, kufutwa kwa kesi za kubambikiza, ujio wa wawekezaji, utayari wa kupambana na COVID 19 na kufunguka kwa dunia ya kidiplomasia.

Hakuna anayejua To Do List ya Rais SSH ina items gani japo mimi naamini la KATIBA MPYA lipo ni suala la wakati. Cha ajabu WAKOSOAJI wa Rais SSH wanamuona hajafanya kitu. Yaani watakapoona Katiba MPYA ndiyo watakubali.

Pengine niwakumbushe, kupata Katiba nzuri ni kitu kimoja na kuheshimu Katiba ni kitu kingine. Katiba hii mbovu ya sasa yule Mwendazake alikuwa anaivunja anavyotaka. Tumpongeze kwanza huyu Samia ambaye anaiheshimu pamoja na mapungufu yake.
 

Bro wangu tumekuwa wote muda mrefu sana hapa JF. Lkn kitu ambacho nimegundua ni kuwa viongozi wote ambao wamepita tukiwa wote hapa JF umekuwa ukiwapinga. Kuanzia Kikwete, JPM mpaka SSH, wote unawapinga. Je umepata kujiuliza nini tatizo? Mfumo au mtu mwenyewe binafsi?
Nionavyo mimi tuangalie uwezo wao, na si mapungufu yao. Kwa maana viongozi wetu hawa ni binadamu kama wewe. Hawatokei MBINGUNI kama malaika. Kwa hiyo tusiwe na mtazamo wa kuwachambua tu, kana kwamba sisi tunaweza kufanya kila jambo bila makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…