Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Hivi ndivyo watu walivyochambua na kupinga uteuzi wa Joshua Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya.

View attachment 1825048

View attachment 1825050
Some of the few hopeless arguments!
Ukishindwa kulima korosho huwezi kuwa mvuvi? Ukishindwa kufuga kuku huwezi kuwa muuza maji. Yaani akishindwa kazi ya ubunge hawezi kuwa mkuu wa wilaya. Is there any synonymity between the two?
Again, hopeless!
 
Kashasema Katiba si kipaumbele chake kwa sasa mkuu.

Ila asinukukuliwe kimakosa. Mama mswahili yule. Alisema hivi:

"Hili la katiba mpya tupeane muda kwanza."

Kauli hii ni tofauti na aliye kwenda zake. Kwani yule ndiyo rasmi alitamka kuwa la katiba yeye hakuahidi.

Hata hivyo Mama asituchukulie poa.
 
Hata akija malaika akatawala kupitia CCM kwa katiba hii bado hatotoshea hicho cheo
 
Dada yangu,
Yaonyesha kuwa bado unayo mapenzi makubwa kwa Mwendazake, kwa upande mmoja hilo laweza lisiwe kosa.
Lakini KOSA ni kuwa wa kushangilia na kushabikia kila kitokacho kwake hata pale ilipokuwa dhahiri kuwa KAKOSEA.
Maadam madhara yake yalikwishaonekana, basi kama twataka kweli kupiga hatua, kama Taifa, itakuwa sio busara kujivunia kuendelea kuyafanya makosa yaleyale.
 
Alivyotelekeza alikuwa ni mbunge kutoka chama gani??

Na hicho chama makini kilimchukulia hatua gani from the first place???
Pole sana
Sijui kama kuna hoja ya msingi hapo.
Hata hivyo kamuulize kwa nini mara baada ya kuvuliwa Ubunge aliamua kuhamia CCM
 
Sidhani kama iliwahi kutokea ulinzi wa Rais wa Tanzania ukawa tatizo,tatizo ni pale tunapomlinda na asitekeleze kile wananchi wanataka akafanye naye akatenda atakayo yeye au chama chake.

Ulinzi huo vipi🙄
 
Sidhani kama mama anajifanyia mwenyewe. Kuna wajinga wanampangia huyu anafaa na huyu hafai, mf huyo nassari. Mama asiwasikilize hao.


Na katiba mpya iliyoachwa na kikwete kwa mwendazake aipitishe.
 
AMEN
 
Well said bro.

Na binaadam sote tuna mioyo na sio malaika. Hata Sisi tunataka katiba mpya na bora, upo uzi wangu humu nimelizungumzia hili. Lakini hatuwezi kudai katiba kwa jeuri na maneno yasiyo staha. Mpaka sasa Mheshimiwa rais amefanya so much already, inapotokea wapumbavu wachache wanakejeli juhudi hizi wanaweza wakamfanya Mama akafikiria tofauti.

Ndio maana nkawaambia, Mama anaweza asilishughulikie na HAKUNA tena HAKUNA chochote tutakachomfanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…