Kila nipatapo wasaa nitakua naelezea makundi mabalimbali ya superhero yaliyopo kwenye Marvel Comics. Mengine tulishayaona kwenye film, mengine bado! Leo nitaanza na hili..
Illuminati
Kwenye marvel Universe kuna race mbili ambazo hazipatani kamwe kila muda zinagombana. Race hizo ni Kree na Skrulls, ambapo Kree ndio hua bad guys kama tulivyoona kwenye Guardian of the galaxy Vol 1 na Captain marvel.
Kipindi fulani makundi haya yakiwa yanapigana yalikuja hadi huku duniani, wakasababisha mauaji na uharibufu mkubwa.. Superhero wa duniani walipoona hivyo wakafanya kikao maalumu, kikao kikifanyikia Wakanda.
Iron Man akiwakilisha Avangers, Mister Fantastic akiwakilisha Fantastic Four, Namor akiwakilisha Atlantis, Black Bolt akiwakilisha Inhumans, Professor Xavier akiwakilisha X-Men, Black Panther akiwakilisha Wakanda na Doctor Strange walijadiriana kuunda chombo kama UN ambacho kitakua kinafuatilia matukio ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa dunia.
Kundi hili waliliita Illuminati na lilikua kinafanya kazi na vikao kwa siri, superhero wasiokua members hawapewi taarifa juu ya kinachoendelea.
Ila baadae chombo hichi kilikuja kusababisha matatizo zaidi kama vile Secret Invasion, Civil War nk..
To be continued......
Mnaruhusiwa kuongeza kwa wale mnaofahamu
View attachment 2115001