Mary Claire: Sikumlazimisha anilipie ada na sikujua kuwa ameoa

Mary Claire: Sikumlazimisha anilipie ada na sikujua kuwa ameoa

Baada ya hapo, Elvis alianza kunitishia kwa hasira, na sasa hali imefikia hatua ya kutaka kuniangamiza, Ningependa kutoa wito kwa wanaume, mwanamke akikataa kuwa na wewe, muache na uendelee na maisha yako hata kama amekula pesa zako unaweza kupata zingine”
Tunaomba huo wito uende kwa wanawake pia, kutopokea zawadi kwa mwanaume usiyempenda au ambaye haumtaki, hii ya kusema eti hata kama amekula hela zako hiyo fairness haipo, ukitaka kula lazima na wewe uliwe
 
Mmesoma mada??

Yeye kasema alivyogindua kaoa akamkataa,sijaona kosa la bi dada.
Wakati wa kulipiwa ada hujui kama kaoa ukimaliza tu shule unagundua.

Jitahidini sana kumchunguza mwanaume kabla hujakubali akugharamikie kwa kiwango kikubwa. Hakunaga pesa za bure. Mtatolewa makafara.

Wanaume, mabinti zetu tuwaambie. Usikubali kugharamikiwa bila kujiridhisha na anayekugharamikia kwamba umempenda na una future naye. Aje kwenu kujitambulisha. Maadili yazingatiwe. Pesa iheshimiwe.
 
Wanaume wa humu huwa na shida gani sijui! Badala ha kujadili kilichowekwa mezani wao ni mihemko tu!
Seran , Mchakato ni funzo ndo maana tumehemka. Tindikali ikishamwagwa imemwagwa hairekebishiki lakini mchakato uliopelekea tindikali kumwagwa unaweza rekebishika kwa wengine.

Msingi wa mada si tukio la tindikali, ni mchakato uliopelekea tukio la tindikali.

Huko nyuma kuna mtu alikuwa analipa ada gizani, halafu kuna mtu alikuwa anakula ada gizani bila kumjua mlipa ada, huo mchakato ndo umezaa tindikali na ndo wa kujadili.
 
Wanakurupuka sana,maana wakiona mada inahusu mwanamke,wanajibu kimihemko tu.
Unadhani tumekurupuka? No, Binafsi nimehemka ndio, sababu na mimi nina mabinti.

Nisingependa kusikia kuna aliyemwagiwa tindikali sababu alilipiwa ada na mwanaume ambaye hajaja nyumbani tukamfahamu.

Aliyemwagiwa tindikali asingekula pesa za wanaume huko gizani kusipoonekana asingelazimika kuja hadharani akiwa kamwagiwa tindikali.
 
Whatever the case.

Je nikuulize jambo?

Unaweza kufungua biashara ili upate hasara
Kama jibu ni hapana.

Basi jua mabaya yote amefanya huyo mwamba ni sababu ya uwekezaji amefanya.

Swali jingine angekua hajamsomesha au kutumia gharama hizo unadhani angepata guts za kufanya alichofanya jibu ni No, ila sisemi hivi ku support ukatili amefanya kwasababu watu weak ndio hufanya mambo ya kipuuzi kama hayo.


Natumai umenielewa
Asande.
Mwanaume ndio alitakiwa achange karata zake vizuri. Unajua umeaoa halafu unaenda kumsomesha binti mwingine, hujiulizi tu kuwa binti akishamaliza akawa na uhitaji wa kuwa na familia yake we msomeshaji utawekwa upande gani??

Hii ni ujinga mnatetea.
 
Mwanaume ndio alitakiwa achange karata zake vizuri. Unajua umeaoa halafu unaenda kumsomesha binti mwingine, hujiulizi tu kuwa binti akishamaliza akawa na uhitaji wa kuwa na familia yake we msomeshaji utawekwa upande gani??

Hii ni ujinga mnatetea.
Mwanaume anajua anachotaka, anajua kwanini anatoa pesa. Iwe kwa nia njema au ovu anajua yeye, Mwanamke ndo anayezila hizo pesa, yeye ndo alitakiwa achange karata zake vizuri. Unakula tu hujui unakula nini? Hujui nia ya anayekulisha? Ukilishwa na jini mnyonya damu?

Haya sasa karata zimechangwa na tindikali.
 
Back
Top Bottom