Masahihisho: Kinachosherehekewa ni Uhuru wa Tanganyika siyo Tanzania Bara. Hatutavumilia upotoshaji

Masahihisho: Kinachosherehekewa ni Uhuru wa Tanganyika siyo Tanzania Bara. Hatutavumilia upotoshaji

Mkuu BANDOKITITA , mtu ukiwa hujui na unajua kuwa hujui, wewe ni mjinga, ukielimishwa, unaelimishika, unajua ujinga unakutoka unakuwa mwerevu.

Mtu ukiwa hujui na hujui kuwa hujui, bali unajidhania unajua, wewe ni mpumba.., hata ukifundishwa hufundishiki!.

Mimi ni mwalimu humu kazi yangu kufundisha. Kabla ya kuungana tulikuwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Baada ya kuungana tumekuwa na nchi moja ya Tanzania, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara, iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Ni Tanganyika ndio ililifuta jina lake na kutumia Tanzania Bara, lakini Zanzibar iliendelea kutumia jina lake la Zanzibar.

P
Tanzania kutoka Tanganyika na Zanzibar ,inazaaje Tanzania zanzibar, na pia Tanzania visiwani? Natafakari cpati uelewa
 
HAKUJAWAHI KUTOKEA TAIFA LOLOTE LA AFRIKA LILILOPATA UHURU ZAIDI YA ETHIOPIA KWANI BADO WAMETAWALIWA KISIASA ,KIUCHUMI,KIJAMII na KIFIKRA.
Hata hiyo Ethiopia inatawaliwa kwa sasa kwa kila kitu kama mataifa mengine ya kiafrika. Wamebaki tu na status ya kwamba hawakutawalia kipindi cha zama za ukoloni. Ila kwa sasa wote ni walewale mwendo wa mateka wa dunia ya kwanza.
 
Masikini mwalimu nyerere ungejua hawa wazanzibari muungano hawautaki. Hawataki kuitwa watanzania, wamekataa Tanzania visiwani, wamerudisha Zanzibar yao.
Watamganyika tumefanyiwa wajinga na ccm yako milele
Mwalimu alijuwa wazanzibari hawautaki muungano. Akaamuwa kuwa muungano utalindwa na dola. Mpaka leo wanaopata matatizo makubwa kutoka kwa watawala ni wanaohoji muungano.
Mtikila
Jumbe
Lissu
Mashehe wa Uamsho
 
Tanganyika iko hai

Sasa kwanini huo uhai wa Tanganyika hauko wazi, kwanini uhai wa Tanganyika utegemee jamhuri ya muungano? Yaan Tanganyika imevaa koti la muungano.
Yaan neno Tanganyika limebaki kwenye hati ya muungano Kati ya Zanzibar na Tanganyika lakini mamlaka ya Tanganyika yamegeuka kuwa ya kimuungano.
 
ILBORU finest.
Asante sana, ukisoma Shule nzuri, kama Ilboru, ukasoma chuo kizuri, kama UDSM, unakuwa na akili nzuri, hata Tundu Lissu, Mwigulu, Lazara, Dr. Ayub Rioba ni Ilboru products!.
P
 
Asante sana, ukisoma Shule nzuri, kama Ilboru, ukasoma chuo kizuri, kama UDSM, unakuwa na akili nzuri, hata Tundu Lissu, Mwigulu, Lazara, Dr. Ayub Rioba ni Ilboru products!.
P

Hakika.

Nilifanikiwa kupita Ilboru ni shule nzuri sana. Nakumbuka kipindi hiko tunafanyia mathematical contexts kule golgotha library kitambo sana.

Maji ya kutosha mto unatiririsha maji muda wote hahaha madaraja matatu yale aisee leo nimekumbuka mbali sana, Ilboru is one of the best government schools in Tanzania.

Hivi kiongozi hii misamiati kama tego, kitei, kayamba uliikuta pia?
 
Hii ni kwa sababu Mwl Nyerere na viongozi wa TANU walikuwa Watanganyika na waliikomboa Tanganyika na wala si nchi nyingine yoyote ile.

Watanganyika hampaswi kuvumilia uongo wowote ule hata kama anayeuongea ni kiongozi mzito, kataeni hadharani ili mheshimike.

View attachment 2837078
Tuliza tako bwanamdogo hiyo nchi Tanganyika we hata huijui we umezaliwa Tanzania.
 
Ilitakiwa mumsapoti sana hayati Mchungaji Mtikila anapopambania upatikanaji wa Tanganyika. Badala yake mkampora UKAWA na kabla ya hapo mlimfukuza uanachama mwaka 1997 alipogombea ubunge Ludewa/Makete.

Alipokua anasema saa ya ukombozi ni sasa, mnasema tulishakombolewa zamani. Alikuwa anapambania uwepo wa Tanganyika kwa faida ya watanganyika na sio kwa faida yake au ya chama. Hakua muumini wa vyama vya siasa.

Majuto ni mjukuu.
We bwege ni zuzu km huyo Mtikila
 
Ukiona watu wanasema mtu hawezi kuwa mkubwa kuliko chama cha siasa basi ujue hapo upo mahali pasipo sahihi.

Yaani watu hawaamini mawazo ya mtu mmoja kuwa yanaweza kuwa sahihi kuliko ya taasisi (chama). Na kwenye kauli hizi za mtu kutokua mkubwa kuliko chama, hapa vyama vya upinzani huungana mkono na CCM, wote huwa na msimamo huo.

Mtu akitoa mawazo tofauti na ya taasisi, piga chini. Hawezi kupata umaarufu kuliko chama
Wanasahau hata huo msimamo wa Chama, Ni wazo la mtu fulani
 
Mkuu BANDOKITITA , mtu ukiwa hujui na unajua kuwa hujui, wewe ni mjinga, ukielimishwa, unaelimishika, unajua ujinga unakutoka unakuwa mwerevu.

Mtu ukiwa hujui na hujui kuwa hujui, bali unajidhania unajua, wewe ni mpumba.., hata ukifundishwa hufundishiki!.

Mimi ni mwalimu humu kazi yangu kufundisha. Kabla ya kuungana tulikuwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.
Baada ya kuungana tumekuwa na nchi moja ya Tanzania, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara, iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Ni Tanganyika ndio ililifuta jina lake na kutumia Tanzania Bara, lakini Zanzibar iliendelea kutumia jina lake la Zanzibar.

P
Unajua ukijiona unajua kwa sababu ya kusoma usichokijua na ukamaliza bila kujua usichokijua maana yake ulipoteza muda kujifunza usichoweza kujua, yani kwa maneno rahisi unakua mpumba.....

Nimekuuliza toka mwanzo kuwa hivi unachokiandika ukikisoma unakielewa? Sikiliza Mayalla mtu mzima mwenzangu, uzuri unajulikana vyema kuanzia elimu yako, na mlengo wako wa kisiasa. Usiwafanye watu werevu kuonekana wajinga, na wajinga kuonekana "geniuses". Unasema Tanganyika ilifuta jina lake, wapi pameandikwa hivyo, na unaweza kueleza kwa nini Zanzibar haikufuta hadi leo? Labda tu nikueleze kuwa Zanzibar ni nchi inayofuata mlengo wa dini ya Kiislam, na km ulivyo utaratibu wa dini hiyo "mume anapofunga ndoa na MKE wake kamwe MKE huwa habadilishi majina ya ubini wake kws sababu tu ndoa. Do you get my point brother.

Tuache simple political reasoning. Unaposema hizi ni sherehe za Uhuru wa Tanzania, ni kitabu gani au museum ipi kuna kumbukumbu hii?

Hivi mtu anaposherehekea siku ya kuzaliwa husherehekea miaka aliyonayo kwa muda huo au tarehe na mwezi aliozaliwa (flashback in memorial)? Kwa hiyo pia unataka kusema Tanzania ilitawaliwa na Mjerumani na Muingereza?

Na nikufundishe tu kitu kidogo kuwa hata Mjerumani hakuitawala Tanganyika bali alitawala eneo lilokuwa linajulikana km "German East Africa". Najua hata hili utapinga kwa hoja dhaifu, fuatilia usije tena ukadanganya watu. Ujue kufahamu na kukubaliana na historia kunataka utashi wa mairifa siyo siasa au porojo.

Kuanzia leo jua kuwa Tanzania haikupata Uhuru bali Tanganyika. Na waziri mkuu wa kwanza Tanganyika alikuwa Mwl Julius Kambarage Nyerere. Full stop.

Nikuambie tu kuwa kila aliesoma shule ya msingi kaisoma vyema historia ya Uhuru wa Tanganyika, aliefika SEKONDARI vile vile kaisoma kuanzia enzi ya URAI later CIVICS na HISTORY. Hadi vyuo vikuu. Labda km wewe ulipita tu hizo sehem ila hukusoma.

Nimemaliza: BANDOKITITA
 
Tanganyika haipo
Zanzibar ipo
Tanzania ipo

Swali, Je Tanzania ni nini?
"Equation" nzuri ya muungano ilipaswa kuwa;
Ta + Zn = Tz

Na wala siyo;
Ta + Zn ~ Tz + Zn

Kwa kuwa endapo ikiwa
Ta + Zn = Tz + Zn

Basi ni dhahiri kuwa;
Ta = Tz
na pia kwamba Zn ina "disappear"

Kwa kuwa ithibati nyuma ya hesabu hii ya kisanii ni dhana ya kwamba:
Ta ~ Tz

Dhana hii kwa vyovyote vile haiwezi kuhakisi ukweli, labda kupitia mantiki za kulazimisha.

Alama za = na ~ ndizo zenye kuweza kuweka maudhui, mantiki na muktadha wenye kuweza kuelezea aina ya muungano tulioingia.

Endapo basi kama;
Ta + Zn = Tz

Na pia
Ta ~ Tz na tena Zn = Zn

Basi "the whole equation is null and void ab initio"
 
Idea ya muungano ilikuwa hivi...

Hapo mwanzo kulikuwa na Ta na Zn, hizi zilipaswa zijumlishwe ili itokee Tz

Ta + Zn = Tz

Kilichotokea ni Ta + Zn = Tz + Zn, huku wenye kutengeneza huu mlinganyo wakisema ya kwamba Ta ≠ Tz

Hawa watakuwa ni wavumbuzi wa algebra 3.0
 
Back
Top Bottom