DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima mwenye namba za simu 0738133331 alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian. Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya “Matajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.

View attachment 3136877
View attachment 3136878
Nikipata uthibitisho wa kutosha kuwa huyo sijui Derrick ni Usalama wa Taifa 100% naweza nami GENTAMYCINE kama Raia Tukuka wa Afrika Mashariki na Kati naweza kutoa Maoni yangu. Tatizo la Tanzania Siku hizi hata tu Mwendawazimu akiwa na Bastola Feki Kiunoni haraka sana ataitwa ni Usalama wa Taifa.

Ila siwezi kumahitisha Kuandika hii Post bila ya Kuuliza hili Swali hivi kama kweli Wewe unajua una Dada yako tena ni Mrembo na Watu huwa Wanaruka nae (Wanambandua) na Mpenda Starehe unaenda nae wa nini katika hizo Kumbi Kubwa za Starehe zenye Watu wenye Pesa zao zisizo na Kazi na wana Mamlaka au Network kwa Wakubwa Serikalini na tena Serikali yenyewe hii hii ya CCM iliyo ICU sasa?

Matatizo mengine huwa mnajitakia wenyewe.
 
Hivi rais Samia atakuwa anajua haya, kwamba anakumbatia vibaka, wahalifu?!!!
Anajua .

Tangu alipowakingia kifua , wauaji na watekaji kwa hotuba kali ya kuwatisha wale wanaolaani vitendo vya utekaji na uuaji.

Kifupi CCM na watu wake ni genge la wauaji .
Rejea Marehemu Ditopile alivyompiga risasi dereva wa boda boda mchana kweupe na hakuna hatua iliyochukuliwa .

Hata huyo ni wale wanaoua watu halafu Polisi wanalazimishwa kuwabeba kwa lazima na kutoa taarifa za uongo huku wakiwatisha watoa taarifa kwa kutumia sheria ya mitandao .

Mzanzibari hakwepi kabisa vitendo vyote vya uvunjifu wa Sheria vinavyofanywa na machawa wake na wahuni wanaotumia ukatili kuwatia hofu Watanganyika .
Uchaguzi anauharibu makusudi kabisa maana anajua hakuna wa kumfanya chochote yeye ni kama mungu na wetu wake ndio maisrael wa kutoa roho za wetu .

Rais hakemei vitendo vya hivyo kuanzia rushwa ufisadi ,utekaji,wizi ,huduma mbovu kwenye ofisi za umma ,uhuni kwenye uandikishwaji wa wapiga kura na kila aina ya ujinga ,yeye anawaza kushinda tu kwa hila na rushwa .
 
Back
Top Bottom