DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kaka kwa aina ya ngumi ninazozijua Mimi hasa nilizopitia mpaka kupata medali kadhaa ,Derick asingetumia hata dakika moja baada ya kunigusa kichwani Kama alivyomgusa Julian .

Yaani ningepiga mpaka bastola angesahau Kama iko kiunoni .

Sema ndiyo vile tena old is Gold Sasa nguvu hizo Sina Tena nimekuwa mnyonge Sana kuona huyu bwana Julian anapigwa Kama mtoto mbaya zaidi mbele ya dada yake
Wanasema Derick ana black belt kutoka Okinawa.
 
kwanza kabisa,kwa faida ya wadau ifahamike wazi kwamba BINAFSI sihusiki na maswala ya umbwa na wala nyumbu. Hilo ni muhimu zaid.

Lakini pili,
masuala ya ulevi na mafumanizi ya walevi ni muhimu yakasuluhishwa baada ya hang over kwisha japo kila moja atakua amesahau kilichotokea kwasababu ya ulevi wake.

Hata hivyo mayowe ya haki za binadamu yanatokea wapi tena kwenye ugomvi wa walevi gentleman 🤣

kwamba mahakama ya haki za binadamu ICC waje kwaajili ya uchunguzi na kuingilia kati ugomvi wa walevi kwamba moja wao kadhulumiwa haki zake, right?🤣
Haki ni za binadamu, sio za walio sober tu hata walevi nao ni watu.
 
Wanasema Derick ana black belt kutoka Okinawa.
Black belt ya huko Okinawa ,haiwezi kulingana na black belt ya mtaa wa keko Kaka Tena chini ya mwalimu tukuka komando Matumula ,aisee naweza kuuwa sema Sasa utu uzima nimetulia na ulanzi ushalegeza maguvu yangu ila ingekuwa miaka hiyo angeombwa pambano ili nimuoneshe nguvu ya elimu ya mtaa hasa kwenye ngumi
 
Wote hapo wamelewa, wanywa pombe tunajielewa; kinachoonekana hicho kiwanja hakina walinzi wakutosha ambao kazi yao ni kuangalia usalama wa wanywa pombe wote.
Kwa ujumla hicho kiwanja si salama, kama mtu anapigwa pale na wao hakuna ata mlinzi au ata baunsa mmoja kwenda kusuluhisha, kuna tatizo.
Kutokana na pombe, wote wako kwenye tatizo la magonjwa ya akili; kinachotakiwa kufanyika ni mtuhumiwa kulipa fidia na fedheha alizomfanyia muhusika.
Kumiliki silaa ni kitu cha kawaida, ila kutembea na silaa eneo la starehe pia ni tatizo; kwa kawaida huwa kuna kukaguliwa na kifaa maalumu uingiapo eneo la namna hilo, vinginevyo labda iwe ni club ndogo; lakini mmiliki alitakiwa kuweka huo mfumo.​
Kabisa hicho kiwanja usalama ni mdogo ,inakuwaje waruhusu walevi waingie na mabomba(vyuma)(Mikwaju)(mguu wa kuku)?
 
Black belt ya huko Okinawa ,haiwezi kulingana na black belt ya mtaa wa keko Kaka Tena chini ya mwalimu tukuka komando Matumula ,aisee naweza kuuwa sema Sasa utu uzima nimetulia na ulanzi ushalegeza maguvu yangu ila ingekuwa miaka hiyo angeombwa pambano ili nimuoneshe nguvu ya elimu ya mtaa hasa kwenye ngumi
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ungempiga kipigo cha Keko magulumbasi! Angetapika uji aliokunywa kwa mkewe au sio.
 
Back
Top Bottom