DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama mtu mnyonge hauna konekshen na ikulu sjui, hauna bastola, dawa ni kuroga tu mamaeh, huyo unamfungia safari, chukua jina lake tu, waganga wa uhakika 30 mamaeh, waganga wale wa kutoa roho wale, tuone kama atatoboa hata mwezi tu mamaeh. .wiki tu mtu anaanza kuvimba tumbo, kidonda kikubwa kinachooza kwenye ulimi, anajinyea na kujikojolea
Hakuna haja ya kusumbua waganga wote hao mmoja tu lazima oashwe na kuzikwa.

Ukhanithi wake akafanyie kwa wangese wenzake.
 
Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.
Ile mamlaka ya maadili mtandaoni nayo itawekwa mfukoni mwa Deriki
 
kwahiyo tuhitimishe tu kwa kusema kwamba kaka wa mrembo aliepata kipigo cha mbwa koko hakuzingatia kanuni za ulevi na alisahau kabisa kwamba unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya ya akili na utimamu wa mwili..

Inafaa siku zingine akiwa nzwii,
ni afadhalli awe anapiga biti tu kwa kurusha mikono na kujipiga kifua kwamba wewe huwezi kuifanya kitu, huku akitokomea kwa kufokafoka na kuondoka kabisa kwenye eneo la tukio. Vinginevyo yajayo yanasikitisha zaidi 🐒
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣hiko kitendo kinaweza kumponza kabisa. Bora akaushe tu.
 
Kulimaliza hili kunatakiwa busara itumike, waombane msamaha na kulipana fidia; kisheria hao wote kwa kuwa wamekunywa pombe na wapo mazingira ya pombe, watatambulika walikuwa na magonjwa ya akili.
We unajielewa h
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima (maarufu kama Chief Abayomi) alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian. Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya “Matajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.


UPDATE: Polisi wamemkamata Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
Tukio hili linaonyesha changamoto kubwa katika usimamizi wa nidhamu, maadili, na uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hasa wale wanaofanya kazi katika vyombo vya usalama. Kwanza, kwa mujibu wa maelezo, matumizi ya silaha na vitisho kutoka kwa mtu anayetarajiwa kulinda usalama wa raia ni kinyume na maadili ya kitaaluma na sheria.

Mifumo ya kiusalama inahitaji kuwajibika zaidi kwa matukio yanayohusisha watumishi wake, hasa pale wanapotumia mamlaka vibaya na kujihusisha katika vitendo vya vurugu au uonevu. Tukio kama hili linaweza kupunguza imani ya wananchi kwa vyombo vya usalama ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa. Ili kulinda imani ya umma na kuimarisha uwajibikaji, ni muhimu hatua za wazi na za haraka zichukuliwe.
 
Uliwahi kusikia au kusoma popote afisa wa Jeshi anamtolea mtu bastola? Usifananishe Jeshi na hizo taasisi zilizojaa watumishi wasio na maadili wala nidhamu.

Tanzania watu wanaotakiwa kuogopwa ni wanajeshi maana hakuna chombo chenye nguvu zaidi ya Jeshi lakini ni kwa sababu ya nidhamu na utu walionao wanajeshi kwenye jamii ndio maana huwezi kusikia habari za hovyo kama hivyo vyombo vingine ambavyo huona sifa kufanya uharifu.
We unaongea upuuzi gani ? , Wote ni wale wale tu washenzi , kuna visa kibao vya wanajeshi kugombea malaya bar nà kupigana na raia mitaani na kwenye kumbi za starehe ,kuna tukio la mwaka huu mwanajeshi kamchoma mtu kisu bar kisa kugombania Barmaid kwenda kufanya naye ngono ,kuna tukio la mwaka jana luteni wa jeshi aliuawa na bodaboda kwa kuchomwa kisu kisa ubabe tu wa huyo mjeda , polisi pia , hawa washenzi TIsS ndio kila siku wananyooshea watu bastola bar wakijiita usalama wa Taifa , hili tukio si mara ya kwanza , hata tangia kipindi cha magufoool walikuwa wanafanya hivi na huu ni mwendelezo ,
Kiufupi Tanzania hawa watu wa vyombo vya ulinzi na usalama wao huwa wanajiweka first class .
Upuuzi sana
 
Back
Top Bottom