DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni mpumbavu kwakweli...
Na usikute Dada alishafanikiwa connection, na bia kala. Fala anamzuia dada.

Ameipata haki yake.

Naona hapa dada alimshika koo asiendelee kuongea. Huenda alitoa matusi makali kwa huyo mwamba.

Unamtukana mpumbavu kisa kapigwa na Usalama?. Jamaa katokea from nowhere anataka mwanamke ulitaka jamaa akubali tu. Kwanza mwanamke alikuwa hamtaki huyo shoga wa Usalama wa ya Taifa.
 
Unamtukana mpumbavu kisa kapigwa na Usalama?. Jamaa katokea from nowhere anataka mwanamke ulitaka jamaa akubali tu. Kwanza mwanamke alikuwa hamtaki huyo shoga wa Usalama wa ya Taifa.
Mkuu wote hatuna facts kamili. But polisi Muliro anasema tukio lilitokea saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Huyo mpiga risasi sio mpuuzi tu ashuke kwenye lift kuchukua dem. Huenda dem alikula beer/ vinywaji the all night long sasa wakati wakwenda kwenye malipo yy na broda wake wakajifanya kuweka kizingiti. Lazima wale shaba tu.
 
Umekua too political…. Siwezi kujaji wanyakyusa wote because mmoja ni mshenzi au wamasai wote simply because mmoja ni muuaji

Sheria haisemi akapigane bar au atembee na binduki

The boy is just a bad apple
You are super blind.
Basi lililojaa abiria likiendeshwa na dereva wa hovyo asiyezingatia sheria za usalama barabarani, lina asilimia kubwa kupata matatizo yatokanayo na uz3mb3 huo.

Sasa jifanye wewe ndiye abiria unayesimama nankusema wreckness driving ya dereva ni tatizo lake na nyie abiria msijihusishe na uzembe wake. Endapo litapata ajali sidhani kama wahanga watakuwa ni dereva na kondakta pekee.

Tanzania failed state. Huo upuuzi wa kutetea dhambi ni code ya watu wa mfumo. Better use other approach maana hauna remorse hata kwa mhanga wa tukio, upo bize mishipa ya macho imekutoka kutetea mfumo uliohatibiwa na msifanye lolote kurekebisha
 
Kumuacha kunaweza kuwa na faida zaidi kuliko ku react au kujibu mashambulizi. Ukiangalia vizuri hata huyo mtu wa silaha hakutakunguliza nguvu katika hilo jambo la kumtaka huyo mwanamke.
Mwanamke alikuwa na uwezo wa kukataa yeye binafsi na bado naamini hizo fujo zisingetokea. Sema sisi kama wanaume hatupendi kuonekana wanyonge, lakini pamoja na kutotaka kuonekana wanyonge basi ni vyema sana kutanguliza busara huenda ika work out kuliko kuanzisha mapambano, sasa mapambano aliyoanzisha kaka mtu hayajasaidia na badala yake yamemletea yeye matatizo
Wachache sana watakuelewa🙌ila point Yako ni sehem ya mafunzo ya ku retaliate pale Langley HQ za CIA
 
Malalamiko yamekuwa mengi sana.
Mkuu unakumbuka enzi za jakaya?

Unakumbuka za mkapa?

Unakumbuka za magu ilikua ni usikuma kwanza?

Naona tunarudi kulekule na no jambo baya sana

Lakini kuita a failed state siyo sawa…. Malafyale Msanii hapo juu anaitwa a failed state

The bottom line is… we don’t want to go back there and mamlaka lazima zichukue hatua kali sana na kwa haraka sana
 
Tunawapa wehu silaha jambo dogo tu anatoa silaha.Kila mtu akiamua kutumia nafasi yake vibaya tutaishije!!?Doctor naye akiamua kupiga wasiompenda sindano za malimao,itakuwaje!!?Hebu tutumie nafasi kwa umakini tuache upuuzi
 
Hajakutana na watemi,,,kinda tajiri mmoja Arusha alitoa pisto bar anamtisha jamaa,,,zikatolewa nne zikawekwa mexzani,,,,akaambiwa rudisha mfukoni au tukugawane vipande,,,,akarudisha afu akatandikwa kofi moja la kumpa wenge mpaka leo hafanyi tena huo upuuzi huo na huwa anasimulia mwenyewe na wenge alilipata hata alikopark gari hakupakumbuka kwa lile wenge
 
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima (maarufu kama Chief Abayomi) alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian. Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya “Matajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.


UPDATE: Polisi wamemkamata Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
Hii nchi sheria ni kwa ajili yetu wanyonge tu. Sitaki comment yangu iguswe
 
Back
Top Bottom