DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu wote hatuna facts kamili. But polisi Muliro anasema tukio lilitokea saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Huyo mpiga risasi sio mpuuzi tu ashuke kwenye lift kuchukua dem. Huenda dem alikula beer/ vinywaji the all night long sasa wakati wakwenda kwenye malipo yy na broda wake wakajifanya kuweka kizingiti. Lazima wale shaba tu.
Ehe kisa K ya huyo dem dangaji
😄

Ova
 
Tunawapa wehu silaha jambo dogo tu anatoa silaha.Kila mtu akiamua kutumia nafasi yake vibaya tutaishije!!?Doctor naye akiamua kupiga wasiompenda sindano za malimao,itakuwaje!!?Hebu tutumie nafasi kwa umakini tuache upuuzi
Ndy jamaa yetu yule wa sinza wambura naona polisi ilibidi wamnyanganye...mpaka leo hawajamrudishia 😄
Ilikuwa kdg kaitoa visa vyenyewe vya kipumbav kabisa
Nawaqmbiaga nyie wenye silaha nendeni hata porini huko mkapige ngiri na digidigi

Ova
 
4
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima (maarufu kama Chief Abayomi) alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian.

Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya “Matajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.


UPDATE: Polisi wamemkamata Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
Nikiangalia CIA, FSB, na MOSSAD alafu nikilinganisha na hawa the so called TISS napata jibu kwanini Tanzania ni maskini.
 
Ndy jamaa yetu yule wa sinza wambura naona polisi ilibidi wamnyanganye...mpaka leo hawajamrudishia 😄
Ilikuwa kdg kaitoa visa vyenyewe vya kipumbav kabisa
Nawaqmbiaga nyie wenye silaha nendeni hata porini huko mkapige ngiri na digidigi

Ova
Kwa kweli bora hata wangeua ngiri,maana wanawehuka kwa vitu vya kijinga haswa
 
Back in the days of sanity, it was rare to find a member of security establishment or political class embracing this form of decrepit hooliganism and thuggery. They were disciplined and closely monitored.

I remember instances were Government Ministers who, through brazen and collosal arrogance committed adultery with peoples' wives expecting nothing would happen to them. Unfortunately when the news reached Mzee Mchonga, it was over for them.

A nation with no collective moral conviction is no different from pack of cannibalistic savages. And yes, Tanzania is a potentially failed state, you just don't realize it.​
Hizo siku ndio tunazihitaji

Baada yake hatujawahi kukosa hizo drama
 
Video Iko very clear

Hujitaji kumaliza juzuu kuona uvunjifu wa sheria

usijitoe fahamu
Video ipo clear ka bisa, nimreitazama sana, nimetumiwa hata whatsapp.

Naona wanawake ,wa kichina sijui wale, na anaedai kuporwa dadake, kama ndiyo aliyepigwa, ni Mwafrika.

Na maelezo ni ya upande mmoja, tutaamini vipi huyo ni mtu wa usalama wa taifa?
 
Dah we unafuatilia matukio kweli,wanajeshi kila kukicha wanadunda watu mitaani na kwenye mabar.kumbuka hata tukio la mtoto wa fundikira swetu,tafuta tukio la komandoo aliyeua chalinze sababu ya mapenzi,tafuta tukio la
Kweli washamba bado wanazaliwa yaani unanunulia vinywaji dem the whole night ili ukamle!, si muongee bei tu uzuri madem zetu wa mjini wako straight forward.unasema price unaenda kula mzigo hayo ya kununua drinks kayataka mwenyewe.
Ni habari ngapi umewahi kukutana nazo kuhusu wanajeshi ukaona mojawapo ikimhusisha mwanajeshi akimtishia mtu silaha?
 
Video ipo clear ka bisa, nimreitazama sana, nimetumiwa hata whatsapp.

Naona wanawake ,wa kichina sijui wale, na anaedai kuporwa dadake, kama ndiyo aliyepigwa, ni Mwafrika.

Na maelezo ni ya upande mmoja, tutaamini vipi huyo ni mtu wa usalama wa taifa?
Kwanza kabisa kutumia silaha ni kosa

Mengine yote secondary

Kamanda wa polisi dar kaiweka vizuri sana

Saaa sijui unatetea nini?
 
Video ipo clear ka bisa, nimreitazama sana, nimetumiwa hata whatsapp.

Naona wanawake ,wa kichina sijui wale, na anaedai kuporwa dadake, kama ndiyo aliyepigwa, ni Mwafrika.

Na maelezo ni ya upande mmoja, tutaamini vipi huyo ni mtu wa usalama wa taifa?
Hata kama maelezo ni upande mmoja bado tukio alilofanya ni la kipuz, in short hapo wote ni wapuz
Na wako kwenye maeneo ya kipuzzz

Ova
 
Back
Top Bottom