Acheni kudanganyana, nimeona komenti nyingi watu humu wakitamba kuwa wangekuwa wao wangemdhibiti huyo jamaa aliyejihami na silaha ( bastola) wangemdhibiti kwa mapigo ya ngumi.
Hiyo siyo movie ni uhalisia mbele ya macho ya wengi, mtu anapojihami na silaha kanuni zifuatazo zifuate Ili uwe Salama:-
1. Kuwa mtulivu na nyanyua mikono juu kuashiria kuwa hauna Nia ya kupigana naye.
2. Epuka kuongea maneno yenye kumfanya aamue kukushambulia kwa silaha.
3. Muombe idhini ya kuondoka kwa unyenyekevu Ili unusuru uhai wako,
4. Kubaliana na matakwa yake wakati huo ( kama mnagombania mwanamke, pesa n.k)
5. Usijaribu kuonesha Nia ya kupigana naye:
MUHIMU: kujaribu kupambana na mtu anayejihami na silaha kama huna ujuzi wa SILAHA ni kuweka dau la kucheza kamari maisha Yako.
Mtu mwenye ujuzi wa SILAHA anatambua aina ya bunduki, uwezo wake, muda ambao silaha imewekwa tayari kwa mapigo na pia ni rahisi kujua kuwa silaha si halisi ( fake)
Ni muhimu kutambua kuwa kumdhibiti mtu mwenye silaha katika umbali mfupi ( close range) inahitaji mafunzo maalumu ya Hali ya juu yanayokupa uhakika wa haraka wa kutekeleza matendo kusudiwa.
Mafunzo hayo asilimia kubwa hutolewa kwa askari wa vikosi maalumu vya kijeshi ( komandoo).
Msijaribu hata siku moja kumvamia mtu aliyejihami na silaha bila kuwa na sanaa za kimapigano, mtakufa kirahisi sana.
"Play safe, a muzzle plays death games"