Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Hapo malima alikuwa analeta ile unajua mm ni nani, ukiona hadi huyo polisi kamind kiasi hiko, kuna kitu alikuwa kafanyiwa na jamaa. Kumbuka yule traffic alietukanwa na mke wa waziri maiga, hawa watu wenye uwezo kifedha wamekuwa wakiwadharau askari wetu
 
Huyu Polisi mwehu tu, kwaiyo kama ameapa kwa bendera aliambiwa aje atishe watu kwa risasi!? Polisi kama hawa si wa kuachiwa hata kidogo maana ipo siku atawafyatulia watu risasi tumboni , sioni mantiki ya yeye kupiga risasi hewani
 
Ungeisikikiza hiyo clip ndipo ungejibu.Hakuna RAIA aliyetaka kumpuga,hapo walishaamua kuondoka,lakini ili kutaka kuonyesha yeye ni polisi ndipo alipotoa silaha.

Walipo ona wamwchapia ndipo walupirudi Mara ya tatu na kumkamata Malima.Siyo sahihi kabisa alichofanya askari.

Hawa Yono wanapenda sana rushwa na itakuwa amemwamvia akupe elfu 50 au ampeleke kituoni ndiyo zao.

Ukitaka kuona kitambulisho hakupi maana utamjua jina lake.

 
Ukiwa hapa jf kila kazi unaweza kusema unaiweza.
Nakushauri nenda ukawe polisi maana hata wewe ni mtanzania ili uwafundishe huo weledi wako

Hakuna watu wanaopewa training namna ya kukamata wahalifu au kudeal na RAIA kwenye msongamano kama polisi,Ila wanapenda Sana kujionyesha wao ndiyo Serikali. na huyu akifukuzwa kazi wengine watajifunza.
 
Huyu Polisi mwehu tu, kwaiyo kama ameapa kwa bendera aliambiwa aje atishe watu kwa risasi!? Polisi kama hawa si wa kuachiwa hata kidogo maana ipo siku atawafyatulia watu risasi tumboni , sioni mantiki ya yeye kupiga risasi hewani
Yani sijui hata Kama alipitia mafunzo huyu polisi, enzi zileeee kulikuwa na somo pale polisi la jinsi ya kuzuia hasira, na huyu zingekuwa zama zile tayari kazi alikuwa Hana kwa makosa kadhaa niliyoyabaini hapo.....
 
Apige tu risasi hata milioni juu. Kodi ya sisi mafala ndo inaliwa hapo... Na haya mambo sisi wenyewe ndo tunaendekeza ndiyo maana wanasiasa wanaowapa kiburi hawa polisi wanajifanyia watakavyo. Kodi tunazolipa ndo zinawapa kiburi. Hivi kuna haja ya askari wanaosaidia ukamataji wa wrong parking kuwa na bunduki?
 
Unajua mkuu,mimi nadhani huko chuoni wanatakiwa wawe makini kuwapa mtihani wa saikolojia hawa vijana
True. Kama wangekuwa peke yao sehemu iliyojificha au usiku mkali, yule kijana angeweza kabisa kumtandika Adam risasi ya kichwani. IGP anapaswa kumtafuta yule kijana. Ila kwa maajabu ya Tanzania, usishangae kuambiwa ''huyu mtu tunamtafuta na sio askari police''
 
Kwa Matumizi Haya Ya Hovyo Hovyo Ya Silaha
Ni Hatari Sana Kwa Askari Lakini Pia Wananchi Tujitahidi Kujua Nguvu Ya Umma Ni Kubwa Kuliko Silaha.
Utemi Haufai Popote Pale!!!!
Mabina alibondwa kwa mawe hadi kufa japo alikuwa na "kamguu ka kuku"
 
Umeisha sema watu walizingara sehemu Hiyo wakifikiri kuna jambazi, ili kutuliza au kumuokoa Mtu ktk mazingira hayo polisi au Mtu yeyote mwenye kibali cha silaha ana ruhusiwa kupiga risasi hewani Kama warning kwa watu wenye nia ya kutenda uovu. Na sababu za majembe kuivamia hiyo gari huja elezea , hivyo habari inakuwa haija balance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…