Ishu ni hv, huyu ndugu malima jr alienda IOM akamuacha dereva wake kwenye gari, dereva akaegesha gari upande ambao kuna maduka na migahawa na ni upande ambao huwa hawakamati labda wakubabatishe mjinga mjinga, sasa mabwana wakubwa (Majembe) wakaja akawa anataka kukamata gari, dereva anamuuliza kitambulisho jamaa akagoma, sasa dereva akaanza kumfokea ndo wananchi wakajaa kwenye tukio, walipomuomba tena atoe kitambulisho akagoma ndo wakataka kumpiga, bahati walikuja na polisi ambao walikuwa kwenye gari, baada ya kelele polisi wakatoka kutuliza presha za wananchi. Mwenye gari (Malima) alipokuja akauliza kwa nn wanataka kukamata gari na kwa nn hawataki kutoa vitambulisho majibu hayakupatikana, Polisi wakapanda kwenye gari wakawa wanaondoka, sasa cha ajabu baanda ya mwendo waa sekunde 30 wakapaki gari pembeni wakaanza kujibizana upya ndo hapo dereva akapaniki na askari akapaniki jamaa akaamua kufyatua risasi juu watu hawakukimbia. Ikabidi Polisi wamchukue Malima Jr waende nae Kituoni.