Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kuna viongozi nchi hii wanajiona wapo juu ya sheria, sheria hizi hawakutungiwa maskini tu Bali watu wote..
 
Hizi stun grenades sio lethal na zinatosha kusambaza watu...jamani live ammunition kosa moja wapiga kura watano.
dummy-m84-stun-grenade-olive-green-1.jpg
 
Hayo katendewa mti mbichi imagine kwa mkavu itakuwaje. Mwendo wa kuisoma
 
Kwa maelezo haya, polisi hajafanya kosa kabisa kufyatua risasi hewani.

Kwa sababu, naona maelezo hapo yanasema wananchi walikuwa Karibu kujichukulia sheria mikononi.

Hivyo, polisi kuokoa maisha ya aliyedhaniwa ni jambazi ili asitolewe roho.

Au mi nimeelewa tofauti!?
Hapana , police alifyatua risasi baada ya kukasirika kuwa haheshimiwi.
 
Sikuizi ni mwendo wa kuwalaumu polisi tu.Yan mtu akisoma post inaneno polisi anaanza kuwatukana bila hata kufatilia undani wa habari.
Kwa hiyo video tu unataka undani gani hapo, sitashangaa nikisikia unashangilia baadae wakisema huyo polisi hafahamiki
 
Kaka yake au Mdogo wake na Mh. Adam Malima? Ukoo ule nasikia hadi house boy anamiliki AK47, polisi wanahaki ya kujilinda kwa kurusha risasi hewani maana hai ndugu wana hobi ya kutembe na mibunduki!
polisi alikasirika hadi anataka kulia, ndipo kutoa hasira zake akapiga risasi ovyo juu. tunakwenda kubaya sana kama wenye silaha ndio hawa.
 
Inashangaza sana askari junior kama huyu kufanya mambo ya ajabu yale...kwanza anasema ameapa hivi yeye na Malima nani hasa kala kiapo??? Na viapo vingapi hasa??? Kingine kuna haja gani kutumia risasi kama huna tishio la maisha?? Huku ukisisitiza serikali haiheshimiwi??? Hivi kweli yule askari ana mafunzo sahihi??? Naamini kuna haja ya kuweka sheria na mafunzo mapya na kuondoa kabisa mlolongo wa kikoloni ndani ya majeshi...hakuna alie salama huo ni ukweli.
 
Aliyewahi kuwa Naibu Fedha katika Serikali ya Awamu ya Nne. Adam Malima akijibizana na Askari wa Jeshi la Polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuegesha gari vibaya. - Aidha katika tukio hilo Askari huyo wa Jeshi la Polisi alichukua uamuzi wa kufyatua risasi kadhaa hewani.
 
watanzania wameanza kukomazwa kwa kuzizoea sauti za silaha. wanaoshangilia huu ujinga wa polisi wanajua madhara ya kitakachotokea siku raia wakiacha kuogopa hii milio?
 
Kamanda siro alisema kuonesha silaha ni ushamba
Sasa huyu aliyeifyatua hewani sijui atamwitaje?
Nangoja kauli yake
 
Suala hapa sio nani kafanyiwa suala ni je askari huyu ana adabu ya kazi ( maadili ya kazi)?? Ni wapi anatakiwa kupiga risasi?? Ni wapi hatakiwi???
 
Inashangaza sana askari junior kama huyu kufanya mambo ya ajabu yale...kwanza anasema ameapa hivi yeye na Malima nani hasa kala kiapo??? Na viapo vingapi hasa??? Kingine kuna haja gani kutumia risasi kama huna tishio la maisha?? Huku ukisisitiza serikali haiheshimiwi??? Hivi kweli yule askari ana mafunzo sahihi??? Naamini kuna haja ya kuweka sheria na mafunzo mapya na kuondoa kabisa mlolongo wa kikoloni ndani ya majeshi...hakuna alie salama huo ni ukweli.
nimeangalia ile video, nimeogopa, huyu askali inaonyesha amechoshwa na kazi, ana lalamika anataka kulia kwa jambo dogo kama hili..

cha ajabu utasikia amepandishwa cheo
 
Back
Top Bottom