Masanja Mkandamizaji: Watu ooh! Mama anasafiri sana. Ulitaka asafiri babaako?

Masanja Mkandamizaji: Watu ooh! Mama anasafiri sana. Ulitaka asafiri babaako?

Kauli hii ya kifedhuli ameitoa Masanja Mkandamizaji alipopewa nafasi ya kuburudisha leo hii mbele ya mamilioni ya Watanzania na wana-Afirika Mashariki kwa ujumla, waliokuwa wanafuatilia sherehe za Uhuru wa Tanganyika kupitia runinga.

Kauli hii inawabeza Watanzania wenye moyo wa kuipenda nchi yao wanaohoji kwanini Rais Samia anafanya sana safari za nje?

Hii dharau kwa umma wa Watanzania haikubaliki na haivumiliki.
Alinishangaza kwa kauli ya kutest mitambo na nchi jirani kweli huyu jamaa na waliompa hiyo furusa ya kuropoka ni mafyatu si wangemhariri anachota kuongea kabla yani ameboa mpaka rais kakeleka
 
Ccm mnatuzalilisha sana! Hivi wanaachaje kujua nini Masanja ataongea; wakati Ni:

  • Mropokaji
  • Hana busara

Hivi kweli serikal haina chujio la content Kwenye audience serious Kama ile?

Hii nchi imekuwa ya hovyo sana Kwa kweli, kweli mnatuzalilisha! Ila Mbowe sio gaid
Tangu enzi na enzi, wasanii ni watu wa kutumika kuburudisha jamii na hawakutegemewa kwa jambo lolote la kiuongozi au busara. Ni watu wasio na maadili wanakata mauno mbele za watu na kufanya vitendo visivyo na staha.
Hata hivyo, wasanii wana nafasi yao na kosa kubwa sana lililofanywa na linaloendelea kufanywa na uongozi wa chama cha mapinduzi na hata nchi kwa ujumla ni kuwapa wasanii au kuwategemea kwenye nafasi au madaraka ambayo kiasili hayatakiwi.
 
Ange ongea Stive Nyerere mungeshika vichwa yule ndio bingwa wa mashudu
 
Jaman hao cndo wale wanaowatafutia kura au????
Kifupi Masanja na yule mwenzie hawakuwa wamejiandaa kufanya VIP comedy walikuwa wakihutubia na kuvurumisha matusi badala ya kuchekesha hopeless kabisa


Masanja hajui VIP comedy inatakiwa isiguse individuals on any way offensive. Kaniudhi sana aliposema Vifaa vyetu vya Kavita vya kisasa vinapata kutu tu havitumiki kivita akamtaka Mkuu wa Majeshi Mabeyo aongee na Raisi Kagame ili waliamshe waanzishe vita ili vitumike Ile statement ilikuwa offensive kwa Kagame na Mabeyo kwa nchi na ya kichochezi why amtaje Kagame na sio Rais mwingine yeyote aliyeko pale? Why Kagame? Siku ingine waigize kabla vyumbani huko chini ya usimamizi kabla kuonyeshwa public


Huyo mwigiza sauti ya Nyerere naye hopeless ohhhh mke wangu Maria Nyerere yule pale, mWanangu Hussain Mwinyi, kijana wangu Majaliwa ujinga mtupu hakuwa na theme nyingine isiyokuwa offensive?

Kiujumla nobody should be allowed just ku perform chochote Mbele ya VIP mpaka kionwe kwanza

Hana ajili Masanja nadhani atakuwa alivuta bangi
 
Mmojawapo wa watu wa hovyo sana nchi hii
 
Hahaaaa mm ni jiwe kwerkwer
Hatukuwa tunasema ooh hasafiri kajifungia tu ni mshamba. Hapana unakwepa kwepa kwa nini tulichokuaga tunasema? Ni kuwa hakuwa hajui kiingereza ndio hicho tulikuwa tunasemaga halaf unakwepa kusema hapo. Na ni kweli sababu kuu ya Jiwe kuogopa kusafir ni kiingerereza tu baas.

Kama sababu ingekuwa kubana matumizi basi asingeiba rambirambi na matrillion hazina.

KIINGEREREZA NDIO SABABU PEKEE ILIMFANYA FEDHULI KUOGOPA KUSAFIRI BAAS!

Idugunde the witch Magonjwa Mtambuka
 
Siku hizi wamerahisisha kila kitu, teuzi wanapewa vichaa bila kufanyiwa vetting yoyote, sishangai hata huyo nabii uchwara nae wamemuokota jalalani wakampeleka akatoe speech tena ametamka huo upuuzi mbele ya wageni waalikwa, sijui tunaonekana taifa la aina gani mbele za waliostaarabika.
Tatizo nchi haina rais wa kweli tangu 2015
 
Masanja kaongea kihuni lakini ujumbe mpana umeeleweka vyema. Watanzania tunapenda sana kulialia.

JPM alipokuwa hasafiri watu walimnanga wakasema kingereza chake ni not reachable. Amekuja Mama anafanya kinyume na mtangulizi wake bado nongwa ni nyingi tu.

Lugha kali ya matusi lakini ujumbe umefika.
Masanja atakula uteuzi kabla yako.
 
Back
Top Bottom