Ni kweli ikiadhiniwa Adhana muda wa swala mashetani hukasirika kwani huona dhamira yao ya kusambaratisha Imani zao haijafanikiwa
Matini ya hiyo hadithi ni kuonesha umuhimu wa swala kwa muunini na jinsi viumbe wabaya wanavyopambana kuzorotesha Imani za waumini kuitumia hiyo hadithi ili kuagulia watu wenye mashetani sio sahihi hiyo ni kujiingiza kwenye shirki
Unakuta mtu kapata kitengo kabisa na anapokea watu walioingiwa na mashetani kwa uchovu wa Imani zao kazi yake ni kupiga Adhana kuanzia asubui hadi jioni eti anaagua ushirikina mtupu
Kwahiyo ukimtibu mtu kupitia Adhana kilichomtibu ni Adhana au Mwenyezi Mungu?Lakini shirki si ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na viumbe wengine katika ibada, sifa au mamlaka ambazo ni haki ya Allah pekee. Hili likienda sambamba na kuabudu au kumtegemea mwingine pamoja na au badala ya Allah.
Sasa je kupiga adhana ili kufukuza mashetani kunakuwaje shirki ? wakati hapo sijamshirika ALLAH kwa chochote zaidi nimemtegemea yeye kwa kutumia maneno mazuri yenye kumtukuza yeye kama ALLAHU AKBAR (takbira), ASH HADU AN LAA ILAHA ILA LLAH( Tashahudi ya kwanza), ASH HADU ANA MUHAMMADAN RASULULLAH( tashahudi ya pili) NA LAA ILAHA ILA LLAH (Tahlil).
Sasa nifahamishe nikipiga adhana nakuwa nimemshirikisha ALLAH na kiumbe gani, au nakuwa nimempa sifa ya ALLAH kiumbe gani ?
Ni mwenyezimungu.Kwahiyo ukimtibu mtu kupitia Adhana kilichomtibu ni Adhana au Mwenyezi Mungu?
Hapo umesema Allah amesema atakae sema,atakayesema
Je ukimtibu mtu kupitia tunguli utasema Mungu ndio kamtibu au ni tunguli?Ni mwenyezimungu
Uganga siyo uchawi,uchawi ni uchawi siyo ushirikina, Quran inapotaja washirikina inazungumzia waliokua wakiabudu masanamuKitendo cha kutumia uganga kuondoa uchawi hiyo shirki yaani umejiingiza katika shirki kwa sababu uchawi kama uchawi ni shirki na hauwezi kumpata isipokuwa mshirikina
Surat An-Nisa (4:48)
Ukikutana na waganga watakueleza dawa za kiganga na dawa za kichawi,kuna kufundishwa uganga na kufundishwa uchawi,ni vitu viwili tofautiHuo uganga unaozungumzia ni upi yani unatumia njia zipi kutibu ambazo si uchawi wala shirki?
Shirki/ushirikina ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu kwa chochote kwahiyo uchawi ni shirkiUganga siyo uchawi,uchawi ni uchawi siyo ushirikina, Quran inapotaja washirikina inazungumzia waliokua wakiabudu masanamu
"Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote..."
Hata adhana kufukuza mashetani si ni hadithi ya mtume hiyo kama ndio Allah si ndio kasema maana mtume hakuwa mwenye kujisemea tu.Hapo umesema Allah amesema atakae sema,
Kwahiyo kumbe tunapata funzo kuwa suluhisho la matatizo ni kudumu na dhikri na sio kwenda kwa mganga au sheikh kwenda kuaguliwa
Mimi sijazungumzia tunguli hivyo siwezi jibu kitu ambacho sina uelewa nacho, Mimi nazungumzia adhana. Lakini kwakuwa hii ni jamii forum na ni mada za wazi hizi wenye uelewa na maswala ya tunguri wanaweza kulijibu, tubaki katika mambo yanayoshabihiana na uislamu wetu.Je ukimtibu mtu kupitia tunguli utasema Mungu ndio kamtibu au ni tunguli?
Uchawi ni shirki kivipi?Shirki/ushirikina ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu kwa chochote kwahiyo uchawi ni shirki
Surah An-Nisa (4:36)
Tunguli ni nini, mitishamba!?..kama ni mitishamba,kuna tofauti gani kutibu mafua kwa viks kingo na kutibu tumbo kwa majani ya mpera!?Mimi sijazungumzia tunguli hivyo siwezi jibu kitu ambacho sina uelewa nacho, Mimi nazungumzia adhana. Lakini kwakuwa hii ni jamii forum na ni mada za wazi hizi wenye uelewa na maswala ya tunguri wanaweza kulijibu, tubaki katika mambo yanayoshabihiana na uislamu wetu.
Mwenyezi Mungu kakataza kumshirikisha na kitu chochote ikiwepo hiyo Adhana,nikipiga adhana nakuwa nimemshirikisha ALLAH na kiumbe gani, au nakuwa nimempa sifa ya ALLAH kiumbe gani ?
"Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote..."
Mtu yeyote anaweza kuingiwa na jinni,si kosa lake bali la jinniMwenyezi Mungu kakataza kumshirikisha na kitu chochote ikiwepo hiyo Adhana,
Surah An-Nisa (4:36)
Adhana ni kwaajili ya kuitia watu wakafanye ibada sio kwa ajili ya kuagulia na hoja kuwa inafukuza mashetani haimaanishi kuwa washirikina walioingiwa na mashetani uwaadhinie Adhana hata kama sio muda wa sala ili wapone bali wao wenyewe wanatakiwa watubie kwa Mwenyezi Mungu na kudumisha dhikri ili wasiingiwe na mashetani waasi wa Mwenyezi Mungu
Uchawi ni shirki kwakuwa unamshirikisha Mwenyezi Mungu na shetani (Al Bakarah)Uchawi ni shirki kivipi?
Hapa haijatajwa shirki,umetajwa uchawi kama uchawi,na Quran imekataza kujifunza uchawi,uchawi ni dhambi kubwa lakini si ushirikina, ushirikina na uchawi ni vitu viwili tofautiUchawi ni shirki kwakuwa unamshirikisha Mwenyezi Mungu na shetani (Al Bakarah)
2:102 - Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.