Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Mkuu unautenganishaje Uslamu na Uchawi? Uchawi katika Uislam ni Elimu dunia,ni ibada.
Malaika wa Allah ndiyo waliokuja kufundisha Uchawi duniani,Q2:102
Mashehe wako sahihi.
 
Tokea mwanzo sikuitaja albadir mimi wewe ndiye umeileta,rejea mada mezani.
Mimi nimetaja neema za uislam na wataalam wanaotokana na elimu za uislam.
Kuhusu albadir kuitwa shirki hiyo ni juu yenu,Unaifananishaje na Novena ikiwa anayeombwa ktk novena sio Allah,novena inahusisha mpaka mfungo wa siku kadhaa albadir mnafunga???
Mwanzo nilikuelewesha kwamba kwenye uislamu kuna utaratibu wa kutumia Qur'an kitiba ambao unakubalika kisheria na kuna njia zengine hazikubaliki kisheria. Ila wewe ukawa unaona matumizi yeyote ya Qur'an kwenye uganga ndio mafundisho ya uislamu na kwamba uganga hutumia Qur'an, nikakwambia hata maandiko ya biblia yanaweza kutumika na ndio nikakuwekea baadhi ya ushahidi wa kitabu chenye kufundisha uchawi/uaguzi kwa kutumia maandiko ya biblia ila unakataa unasema biblia haijaelekeza kutumia maandiko yake kuagua. Ishu ni kwamba watu wanatumia hivyo hilo la kwamba biblia haijaeleza hivyo ndio sawa na wanaotumia Qur'an kitiba kinyume na maelekezo ya Qur'an yenyewe.

Kinachofanya albadir iitwe shirki ni vile inahusisha maombi yake kupitia watu waliyokufa wakipigana vita, kwamba anaombwa Mungu kupitia hao watu.
Sasa utaangalia mwenye kama novena haina mambo yenye kufanana na hayo, na kuhusu kufunga kwenye albadir pia wengine hufunga kabla ya hicho kisomo cha albadir.
 
Kwahiyo unabisha tu kichwa kichwa?
Kipi hicho nilichokubishia kichwa kichwa? Mpaka dakika hii wewe ndio muislamu hapa umekataa kuamini uwepo wa uchawi pamoja na kisomo cha Ruqya, wewe ndio umedai kufanya ibada ni kinga ya mashetani kwamba wenye kufanya ibada hawawezi kuingiwa na jini na kwamba usipofanya ibada Mungu hufanya shetani akuingie.

Hayo yote sijakubishia wala sijakukubalia, nahoji tu kwenye uhalisia wake ndio maana nikauliza una uhakika wenye kufanya ibada hakuna wenye kusumbuliwa na majini? Vp aliyeingiwa na shetani na kupagawa hajitambui ataweza vp kujisomea mwenyewe Qur'an au kufanya ibada ili kujitibu?
 
Mpaka dakika hii wewe ndio muislamu hapa umekataa kuamini uwepo wa uchawi pamoja na kisomo cha Ruqya
Uislamu ni dini inayofuata utaratibu wa Qur'an na Sunnah sio mtu

Jibu hoja acha kufuata mkumbo

Jibu hoja kwa maandiko acha kujadili kichwa kichwa mambo yanayohitaji elimu na quotation kutoka kwenye vitabu

Bado hujajibu maswali yangu niliyokuuliza hapo juu yajibu tafadhali
 
Mwanzo nilikuelewesha kwamba kwenye uislamu kuna utaratibu wa kutumia Qur'an kitiba ambao unakubalika kisheria na kuna njia zengine hazikubaliki kisheria.
kosa langu kusema ukisoma sana unakuwa mganga ni lipi kwa maelezo yako haya??maana kama utaitumia vyema unatibu,uganga sio dhambi kwa mujibu wa uislam ila ramli.
Ila wewe ukawa unaona matumizi yeyote ya Qur'an kwenye uganga ndio mafundisho ya uislamu na kwamba uganga hutumia Qur'an,
bado hili halitengui maelezo yangu kwamba inayotumika ni Quran ktk uganga.
nikakwambia hata maandiko ya biblia yanaweza kutumika na ndio nikakuwekea baadhi ya ushahidi wa kitabu chenye kufundisha uchawi/uaguzi kwa kutumia maandiko ya biblia ila unakataa unasema biblia haijaelekeza kutumia maandiko yake kuagua.
hakuna kitu kama hicho usijifurahishe ndugu,mtandaoni kuna picha za Muhammad na naweza kukwambia ni yeye unaweza kunielewa??
Ishu ni kwamba watu wanatumia hivyo hilo la kwamba biblia haijaeleza hivyo ndio sawa na wanaotumia Qur'an kitiba kinyume na maelekezo ya Qur'an yenyewe.
kwahiyo Quran hakuna popote imeeleza itumike kwa tiba kama ilivyo bible???
Kinachofanya albadir iitwe shirki ni vile inahusisha maombi yake kupitia watu waliyokufa wakipigana vita, kwamba anaombwa Mungu kupitia hao watu.
sasa haifanani na Novena hii haihusishi watu,ni Mungu,wewe na maombi yanawezakuwa mfungo au sadaka.
Sasa utaangalia mwenye kama novena haina mambo yenye kufanana na hayo, na kuhusu kufunga kwenye albadir pia wengine hufunga kabla ya hicho kisomo cha albadir.
NOvena haiko hivyo aise.
 
Lete aya au hadithi kuthibitisha hii hoja yako
Kutoka kwa ‘Awf bin Maalik Al-Ashja’iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Tulikuwa tunafanya ruqyah katika zama za jahiliyyah, tukasema: Ee Rasuli wa Allaah, unaonaje katika hayo (ruqyah yetu]? Akasema: ((Nionyesheni ruqyah yenu, hakuna ubaya katika ruqyah madamu tu haitokuwa na shirki)) [Muslim katika Kitaab As-Salaam, Abuu Daawuwd katika Kitaab Atw-Twibb]

Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Tulikuwa katika safari tukateremka mahali, akaja kijakazi akasema: Bwana wetu ametafunwa na nge na wanaume wetu hawapo, je, yupo kati yenu tabibu? Akasimama pamoja naye mtu mmoja ambaye hatukudhania kuwa anajua ruqyah (utabibu). Akamtibu kwa ruqyah akapona. Akampa kondoo thelathini na akatupa maziwa tunywe (kama ni malipo). Aliporudi tukamwambia: Je, ulikuwa kweli unajua kutibu kwa ruqyah, au ulikuwa unabahatisha tu? Akasema: Hapana, bali nimemsomea Ummul-Kitaab (Suwrah Al-Faatihah). Tukasema: Tusiseme kitu hadi tumfikie au tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Tulipofika Madiynah, tulimwelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Alijuaje kuwa (Al-Faatihah) ni ruqyah? Gawaneni na mnitolee sehemu (ya kondoo.” [Al-Bukhaariy]
 
kosa langu kusema ukisoma sana unakuwa mganga ni lipi kwa maelezo yako haya??maana kama utaitumia vyema unatibu,uganga sio dhambi kwa mujibu wa uislam ila ramli.

bado hili halitengui maelezo yangu kwamba inayotumika ni Quran ktk uganga.

hakuna kitu kama hicho usijifurahishe ndugu,mtandaoni kuna picha za Muhammad na naweza kukwambia ni yeye unaweza kunielewa??

kwahiyo Quran hakuna popote imeeleza itumike kwa tiba kama ilivyo bible???

sasa haifanani na Novena hii haihusishi watu,ni Mungu,wewe na maombi yanawezakuwa mfungo au sadaka.

NOvena haiko hivyo aise.
Elimu ya dini na elimu ya tiba ni elimu mbili tofauti, ukisema kwamba muislamu akisoma sana anakuwa mganga si ya kweli kwa sababu unataka kutuaminisha kwamba waganga wana elimu kubwa ya dini kitu ambacho sio kweli.
Waganga wanajua elimu ya tiba na wengi hawana elimu sana ya dini.

Mkuu hizo picha ni screenshot za kutoka kwenye kitabu na mimi ndio niliyo screenshot maana ninacho hicho kitabu, sasa sijajua mkuu unachokataa ni nini na ulitaka nikupe ushahidi gani? Hebu eleza unataka ushahidi wa vp? Huyo mwenye hiko kitabu alikuwa akijihusisha na uchawi na ana vitabu kadhaa venye kufundisha uchawi, nilikwambia zaburi inatumika sana kwenye uchawi hivyo si huyo tu nishaona kwenye mafundisho mengine ya uchawi ikitumika zaburi.

Sasa nashindwa kuelewa unachokataa ni nini? Labda nikueleweshe kitu ni kwamba uchawi unaambiwa ni maneno hivyo haijarishi yanatumika maneno ya kutoka kwenye biblia wala quran, sasa unakataa tu kisa unaamini biblia ni takatifu hivyo haiwezi kutumika kwenye uchawi.
 
Hapa hatubishani tunaelimishana na safari hii usije ukakimbia hakikisha unaaga na hakikisha umesilimu na kuacha uganga na uchawi hayo mambo ni shirki Mwenyezi Mungu kakataza
Sasa mkuu nikukimbie kwa hoja ipi ya kunikimbiza? Mada ya uchawi ulikiri hujui uchawi ni nini na hujawahi kushuhudia hata tukio moja la uchawi ukawa umeshikilia maneno mawili tu kwamba "hakuna uchawi" " lete uthibitisho". Sasa ulitaka hapo niendelee kujadili nini?
 
Mfano mdogo ni kuomba au kuabudu kiumbe alichokiumba huo ndio ushirikina au shirki

Tunatakiwa tumuombe na kumuabudu Mungu pekee na sio viumbe alivyo viumba

Mbona wanamuomba mudi, inakuwaje hapoo
 
Elimu ya dini na elimu ya tiba ni elimu mbili tofauti, ukisema kwamba muislamu akisoma sana anakuwa mganga si ya kweli kwa sababu unataka kutuaminisha kwamba waganga wana elimu kubwa ya dini kitu ambacho sio kweli.
Waganga wanajua elimu ya tiba na wengi hawana elimu sana ya dini.
elimu kubwa ya dini kiwango chake ni kipi??
Ni kweli nimesema mtu akisoma sana,yaani huwezi kuwa mganga wa kitabu kama hujasoma sana Quran.kwani sana ina kipimo gani??
Mkuu hizo picha ni screenshot za kutoka kwenye kitabu na mimi ndio niliyo screenshot maana ninacho hicho kitabu,
Kwa maana hiyo unawezaleta aya zozote kutetea ushoga kutoka katika bible,kwamba hizi wanatumia wapinde kujitete na kuhalalisha mambo yao.issue si picha tu za maandiko??
sasa sijajua mkuu unachokataa ni nini na ulitaka nikupe ushahidi gani? Hebu eleza unataka ushahidi wa vp? Huyo mwenye hiko kitabu alikuwa akijihusisha na uchawi na ana vitabu kadhaa venye kufundisha uchawi, nilikwambia zaburi inatumika sana kwenye uchawi hivyo si huyo tu nishaona kwenye mafundisho mengine ya uchawi ikitumika zaburi.
Wewe umesomea uchawi kwa level gani??huko kwenye shule ya uchawi wanatumia zaburi gani kufundishia uchawi zaburi zipo nyingi,leta moja specific na useme inachangiaje katika kuroga.
Sasa nashindwa kuelewa unachokataa ni nini? Labda nikueleweshe kitu ni kwamba uchawi unaambiwa ni maneno hivyo haijarishi yanatumika maneno ya kutoka kwenye biblia wala quran, sasa unakataa tu kisa unaamini biblia ni takatifu hivyo haiwezi kutumika kwenye uchawi.
Sijasema takatifu,sisi sio waumini wajinga wa kuamini kwamba mtu akikojolea msaafu boo inafata kitabu inakuwa kama kamba,NO.

Ni kwamba haina maagizo hayo,hata ukitaka kufanya hivyo utakuwa unajitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Kuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.

Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki

Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim

98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,

98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,

98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka

98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?

Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.

Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama

NB, tujadili kistaarabu
Maneno yako ni kweli kabisa lakini Shiriki ni kwa yule anaye amini bila Mganga hafanikiwi mpaa kwa mganga au mwalimu.

Qur'an inathibitisha Uchawi upo lakini hauwezi kukudhuru kama Mungu hataki. Nawanao enda kwa wa waganga na walimu hawawezi kufanikiwa lolote kama Mungu hataki ufanikiwe. Ushiriki unakuja pale mtu anapo amini hawezi kufanikiwa bila mganga anamsahau Mungu
 
Ngoja niwatag hapa maostadh
Malaria 2
Covax
Adiosamigo
Webabu
FaizaFoxy
Et al......
Asante sana kunivuta kwenye mada hi hapa, mimi na amini kitu kimoja tu si mchawi, mganga au mwalimu wanaweza kufanya lolote kama Mungu hataki.

Qur'an inasema wazi uchawi upo lakini huyo mchawi hawezi kufanikiwa lolote kama Mungu hataki. Kuna wakati mwingine wajinga watajiuliza kivipi Mungu aruhusu hayo wengine wadhurike, hapo ni Hekima ya Mungu yeye anajua faida yake na madhara yake. Kwa hio sio kila kitu ukichukiacho kina kudhuru na sio kila ukipendacho kina faida na wewe.

Mungu anasema kwenye Qur'an hata wajikusanye watu wote na majini wote ili wakudhuru hawawezi kukudhuru kama Mungu hutaki.
 
Mwenyezi Mungu kakataza kumshirikisha na kitu chochote ikiwepo hiyo Adhana,

Surah An-Nisa (4:36)


Adhana ni kwaajili ya kuitia watu wakafanye ibada sio kwa ajili ya kuagulia na hoja kuwa inafukuza mashetani haimaanishi kuwa washirikina walioingiwa na mashetani uwaadhinie Adhana hata kama sio muda wa sala ili wapone bali wao wenyewe wanatakiwa watubie kwa Mwenyezi Mungu na kudumisha dhikri ili wasiingiwe na mashetani waasi wa Mwenyezi Mungu
Kwanza surat An - Nisa haisemi Mwenyezimungu kakataza kumshirikisha Allah na chochote ikiwemo adhana... neno ikiwemo adhana halipo.

Ni kweli Mwenyezimungu kakataza shirki na hatutakiwi kufanya shirki( Allah atukinge sote ), Ila ni muhimu kuelewa shirki ni nini, Na Quran ilivyokataza shirki ilikuwa inakataza nini..?
Hili pekee linatupa swali la kiudadisi nakutufanya tufungue akili zetu katika kujifunza zaidi kwani shirki inaweza mtoa mtu katika dini hivyo sio suala la kuliangalia kwa nje bali kwa undani wake.
Twende taratibu sasa sote tupate faida..
Kuna hadithi ya mtume inasema

"Atakayekula tende saba za Ajwa asubuhi, siku hiyo hatadhuriwa na sumu wala uchawi."
(Imesimuliwa na Abu Hurayrah, Bukhari na Muslim)

Katika hadithi hiyo ni nani anayekukinga usidhuriwe na uchawi ? Je ni tende za ajwa au Allah? Ikiwa ni Allah je nikiamini hivyo bila kula hizo tende nitapata hiyo kinga ya kutodhuriwa na uchawi sawa na aliyekula tende ?
Jambo la pili ni kuwa kwani kuna ulazima gani mtu ili apate kinga lazima ale hizo tende ?Kupitia maswali hayo utaona kumbe jambo la shirki ni pana sana ila pamoja na upana wake lina mipaka yake.

Hii ni kusema kuwa aya inavyosema tusimshirikishe mwenyezimungu na chochote ili takiwa tuelewe kwanza shirki nini..? ndio tuje kwenye hiyo chochote...Bila kuelewa maana ya shirki tutajikuta tunayakataa mambo kumbe yana kheri na sisi na tutajikuta tunayakubali mambo kumbe yana shari na sisi.

Hapa utaona kumbe shirki inaanza katika kuamini... Kwamaana kama mimi nitakula tende nakuamini kuwa hizo tende ndio zinanikinga niatakuwa nafanya shirki japo nafanya jambo ambalo mtume ndio kasema, Sijui tupo pamoja? Kwa maana anayekinga ni ALLAH ila tende za ajwa ni asbabu tu sasa kwanini tende ziwe asbabu hapo anajua yeye ALLAH kuna siri gani katika tende za ajwa.
Vivo hivyo ikiwa mtu anapiga adhana kwa imani kwamba maneno ya adhana yanawakumbusha majini waovu(mashetani) juu ya ukubwa wa Allah na hivyo wanakimbia — basi si shirki, nakinyume chake ikiwa unaitakidi adhana ndiye inafanya na sio ALLAH basi ni shirki.
Ndio maana swali linarudi tena anayepiga adhana anakuwa kamshirikisha Allah na nini? wakati hayo ni maneno yenye tashahud,takbir n.k na mtu anaamini Allah ndio anatenda shirki iko wapi hapo?
 
Kuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.

Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki

Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim

98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,

98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,

98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka

98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?

Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.

Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama

NB, tujadili kistaarabu

Ni ngumu sana kutenganisha uislam na ulozi/uchawi. Ndiyo maana wenyewe ibada yao inafungamana na mizungu, nyota, mwezi na majini. Utabaki mdomo wazi wakikwambia kwamba kuna majini wazuri. Sasa katika hali ya kawaida, majini/mashetani ni malaika walioasi mamlaka ya Muumba. Kama wameasi, hamna namna kwamba utapata kizuri kutoka kwa waasi. Labda wasalimu amri mapema sana kabla ya hali kuwa mbaya. Lakini kwa waislam, eti kuna majini mazuri, inastaajabisha sana.
 
Back
Top Bottom