Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Nitajie mganga mmoja ambaye una uhakika haijui Quran kiwango cha kuitwa msomi wa Quran.
Mimi naamini wote ni wasomi wazuri kabisa.

mtaje mtu asiye mchawi anayeroga,kuhusu kuagua sina shida,ndio maana nikasema wanakuwa waganga sio wachawi,yeyote anayetibu anakuwa mganga.

bahati mbaya hujui wala huwezi kuhisi unajadili na mkristo wa aina gani,unafikiri ugumu wa kusali novena ungezingatiwa ikiwa kuna verse moja au mbili za kusoma ktk zaburi ili umshtakie mtu kwa Mungu???

ndio maana yake,ukisikia mtu anakwambia nazi inatumika kwenye maandalizi ya chai unajua tu huyu aliona maziwa akadhani ni nazi,matumizi ya kitu sehemu yanatokana na uhitaji wake sio maamuzi tu.

Biblia haijaagiza,hata anayefanya anajua anacheza mluzi anaopiga mwenyewe,lakini Quran inaagiza kabisa,kwanini wanaoisoma wasiwe wataalamu wa field hiyo??
Nimekueleza kwamba mganga anajua tu kusoma Qur'an wala hahitaji kuwa mjuzi wa Qur'an, sasa ukisema wewe unaamini waganga ni wajuzi zaidi wa Qur'an hiyo ni imani yako mie siwezi kufanya kitu, labda ungenisaidia kueleza huo ujuzi zaidi wa Qur'an kwa mganga anautumia kufanya nini? Kwa sababu mganga atasoma quran na kuandika tu basi, ambapo ni elimu ya chini tu.

Mkuu kuroga hata wewe unaweza ukachukua dawa fulani ukamtilia mtu kwenye kinywani na kutia nia zako na huyo mtu akapata athari ya vile ulivyokusudia hivyo teyari umesharoga sio lazima hadi uwe mchawi, ndio maana hicho kitabu kinaelekeza mambo kama hayo kwa kutumia zaburi ila bahati mbaya haujasoma.

Mimi sizungumzii biblia ilivyoagiza bali nazungumzia jinsi watu wanavyohusisha au kutumia biblia katika kuroga na kuagua. Kama utasema ukitumia biblia kuroga huo uchawi hauwezi kufanya kazi hilo ni juu yako maana mie sipo hapa kutetea huo uchawi wa kutumia zaburi, nimeonyesha tu kinachofanyika.
 
ufunuo 12: 7-9 Hii hapo chini sijaona sehemu imetaja majini ni malaika walioasi nisaidie ku-highlight kama ipo.

7 Kisha kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake wakipigana na hilo joka. Joka nalo pamoja na malaika wake likapigana nao.
8 Lakini joka na malaika wake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni.
9 Basi joka hilo kuu likatupwa nje, yule nyoka wa kale aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye watu wote ulimwenguni. Alitupwa chini ardhini, yeye pamoja na malaika wake.

Majini ni malaika walioasi, ambao hapo wanatajwa kama joka na malaika zake. Pia kwenye biblia hakuna mahala utapata neno jini
 
Nimekueleza kwamba mganga anajua tu kusoma Qur'an wala hahitaji kuwa mjuzi wa Qur'an, sasa ukisema wewe unaamini waganga ni wajuzi zaidi wa Qur'an hiyo ni imani yako mie siwezi kufanya kitu,
Embu fafanua mjuzi na msomaji pekee wa Quran tofautu yao ni ipi??wanaotumia kutibia(waganga)ni wajuvi au wasomaji pekee wa Quran??
labda ungenisaidia kueleza huo ujuzi zaidi wa Qur'an kwa mganga anautumia kufanya nini? Kwa sababu mganga atasoma quran na kuandika tu basi, ambapo ni elimu ya chini tu.
IKiwa kusoma andiko,kulielewa,na kujua kazi yake mpaka kuliandika sehemu lilete matokeo unasema ni ujuzi wa kawaida pekee,embu nieleze mtu mwenye elimu ya juu ya Quran ana matokeo yapi??unaweza mtaja mmoja kwa hapa dsm??
Mkuu kuroga hata wewe unaweza ukachukua dawa fulani ukamtilia mtu kwenye kinywani na kutia nia zako na huyo mtu akapata athari ya vile ulivyokusudia hivyo teyari umesharoga sio lazima hadi uwe mchawi,
sahihi kabisa,vipi kuhusu kutibu??unawezakuwa mganga bila kuwa na elimu???
ndio maana hicho kitabu kinaelekeza mambo kama hayo kwa kutumia zaburi ila bahati mbaya haujasoma.
sio sijasoma ni utapeli,kwa ajili ya watu kama wewe.kila jambo unaloliona lina target yake ya watu.
Mimi sizungumzii biblia ilivyoagiza bali nazungumzia jinsi watu wanavyohusisha au kutumia biblia katika kuroga na kuagua.
huu ndio utofauti wa biblia na Quran,yenyewe haijajihusiha kabisa na hayo mambo,ila watu wataitwist iendane na matamanio yao,hata andiko la wapinde utalupata ukitaka.
Kama utasema ukitumia biblia kuroga huo uchawi hauwezi kufanya kazi hilo ni juu yako maana mie sipo hapa kutetea huo uchawi wa kutumia zaburi, nimeonyesha tu kinachofanyika.
What if ukarogeka utasema ni zaburi ndio sababu au mhusika??
 
Kuna mambo ambayo nakubaliana na wewe. Mfano, Mungu anaweza kuruhu/kuachia wachawi wakupige kipapai au azuie.
Swali dogo, Je kuna majini mazuri?? Kama ni mazuri, mazuri kwa nani?
Watu Kuna waumini na waovu

Majini Kuna waumini na waovu (mashetani)

Majini waumini wanafanya ibada zao na hawana mafungamano na binadamu either kuwadhuru au kuwanufaisha.

Majini waovu/mashetani ni ambao wana mafungamano na binadamu, wanatumia binadamu kwa masharti maalumu kuwanufaisha ikiwa pamoja na kuwadhuru binadamu wengine.
 
Embu fafanua mjuzi na msomaji pekee wa Quran tofautu yao ni ipi??wanaotumia kutibia(waganga)ni wajuvi au wasomaji pekee wa Quran??

IKiwa kusoma andiko,kulielewa,na kujua kazi yake mpaka kuliandika sehemu lilete matokeo unasema ni ujuzi wa kawaida pekee,embu nieleze mtu mwenye elimu ya juu ya Quran ana matokeo yapi??unaweza mtaja mmoja kwa hapa dsm??

sahihi kabisa,vipi kuhusu kutibu??unawezakuwa mganga bila kuwa na elimu???

sio sijasoma ni utapeli,kwa ajili ya watu kama wewe.kila jambo unaloliona lina target yake ya watu.

huu ndio utofauti wa biblia na Quran,yenyewe haijajihusiha kabisa na hayo mambo,ila watu wataitwist iendane na matamanio yao,hata andiko la wapinde utalupata ukitaka.

What if ukarogeka utasema ni zaburi ndio sababu au mhusika??
Nikupe mfano mwepesi kama mfano marehemu Sheikh Yahya alikuwa akijulikana kama bingwa wa usomaji wa Qur'an, kwa maana alibobea katika somo la usomaji wa Qur'an. Lakini pia kuna waliyobobea kwenye tafsiri ya Qur'an. Kwahiyo mganga hahitaji kujua sana kusoma Qur'an kwanza wengi hawasomi vizuri au kwa usahihi wanapotumia katika tiba, mganga hahitaji kujua sana tafsiri ya Qur'an na pia wala hahitaji hata kuhifadhi msahafu mzima.

Mkuu hata wewe unaweza ukafundishwa dawa ambazo zinatibu uchawi ukatumia na ukapona, uganga ni elimu japo kuna mengine zaidi maana uganga ni kazi hatari kwa mujibu wao na kiwango cha kwa waganga hutofautiana.

Sasa hilo la utapeli halinihusu mimi sijajua kwanini bado tunabishana katika hili, kama biblia haijajihusisha na hayo mambo sawa mie sitafuti mfanano hapa, wakristo wanajivunia jina la Yesu kuwa linatenda miujiza na kutoa mapepo kiasi hata manabii feki pia hujihusisha na hilo jina.

Nimekwambia uchawi ni maneno na wachawi wanaweza kutumia chochote na kivyovyote vile.
 
Nikupe mfano mwepesi kama mfano marehemu Sheikh Yahya alikuwa akijulikana kama bingwa wa usomaji wa Qur'an, kwa maana alibobea katika somo la usomaji wa Qur'an. Lakini pia kuna waliyobobea kwenye tafsiri ya Qur'an. Kwahiyo mganga hahitaji kujua sana kusoma Qur'an kwanza wengi hawasomi vizuri au kwa usahihi wanapotumia katika tiba, mganga hahitaji kujua sana tafsiri ya Qur'an na pia wala hahitaji hata kuhifadhi msahafu mzima.
Twende na huyu huyu sheikh yahya,huyu ni sheikh(mwaalimu),na alikuwa mtu wa visomo kabisa hata kutabiri nyota,kwanini unafikiri sikujua nilichoandika niliposema wasomi wazuri ndio waganga wa Quran??
Mkuu hata wewe unaweza ukafundishwa dawa ambazo zinatibu uchawi ukatumia na ukapona, uganga ni elimu japo kuna mengine zaidi maana uganga ni kazi hatari kwa mujibu wao na kiwango cha kwa waganga hutofautiana.
Ndio maana nikasema (MGANGA)nikiwa nina maana kabisa lazima awe mtaalam kabisa maana yake ni tabibu wa kutegemewa,sio msomaji tu.
Sasa hilo la utapeli halinihusu mimi sijajua kwanini bado tunabishana katika hili, kama biblia haijajihusisha na hayo mambo sawa mie sitafuti mfanano hapa, wakristo wanajivunia jina la Yesu kuwa linatenda miujiza na kutoa mapepo kiasi hata manabii feki pia hujihusisha na hilo jina.
Manabii feki wewe unawapimaje??una uhakika gani tukiwachambua kwamba hata nabii unayemfuata hatafuatana nao kwenye huo ufeki??tuwaheshimu tu,maana mwenye hukumu ni Mungu tu.
Nimekwambia uchawi ni maneno na wachawi wanaweza kutumia chochote na kivyovyote vile.
Wachawi hupenda kutumia Quran maana ina sura zinazoshabihiana na kazi zao,over.
 
Kwakuwa majini yamejitambulisha kuwa dini yao ni Uislamu:
Ni lazima kiongozi wa Kiislamu ajue wanashirikiana vipi nao katika ibada:
Maana mtume wao ni Muhamadi na yanaswali misikitini:
Kwahiyo Mashehe na Maimamu ni lazima wajue uhusiano wa waislamu watu na Waislamu majini:
Katika kujua huko ndiko kunakowapelekea kuwa wachawi:
Muhamadi alisema Majini ni ndugu wa Waislamu, muislamu ameambiwa ampende Jini Muislamu kuliko mtu asiye Mwislamu:
(Kafiri)Hapo mtakosaje kuwa wachawi ?

Je kama mwislamu umefanya juhudi gani kukutana na ndugu yako wa Kijini?
Kama alivyofanya mtume Muhamadi?
Umesoma wapi hayo kuwa Majini mtume wao ni Muhammad (S.A.W)
 
Kutoka kwa ‘Awf bin Maalik Al-Ashja’iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Tulikuwa tunafanya ruqyah katika zama za jahiliyyah, tukasema: Ee Rasuli wa Allaah, unaonaje katika hayo (ruqyah yetu]? Akasema: ((Nionyesheni ruqyah yenu, hakuna ubaya katika ruqyah madamu tu haitokuwa na shirki)) [Muslim katika Kitaab As-Salaam, Abuu Daawuwd katika Kitaab Atw-Twibb]

Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Tulikuwa katika safari tukateremka mahali, akaja kijakazi akasema: Bwana wetu ametafunwa na nge na wanaume wetu hawapo, je, yupo kati yenu tabibu? Akasimama pamoja naye mtu mmoja ambaye hatukudhania kuwa anajua ruqyah (utabibu). Akamtibu kwa ruqyah akapona. Akampa kondoo thelathini na akatupa maziwa tunywe (kama ni malipo). Aliporudi tukamwambia: Je, ulikuwa kweli unajua kutibu kwa ruqyah, au ulikuwa unabahatisha tu? Akasema: Hapana, bali nimemsomea Ummul-Kitaab (Suwrah Al-Faatihah). Tukasema: Tusiseme kitu hadi tumfikie au tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Tulipofika Madiynah, tulimwelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Alijuaje kuwa (Al-Faatihah) ni ruqyah? Gawaneni na mnitolee sehemu (ya kondoo.” [Al-Bukhaariy]
Hapa sawa haya twende, Mtume kasema nini kuhusu rukya, ni yapi masharti ya Rukya?
 
nakinyume chake ikiwa unaitakidi adhana ndiye inafanya na sio ALLAH basi ni shirki.
Je wanaoenda kufanyiwa uganga wa Adhana wanaitakidi kwa Allah na si kwenye Adhana na mganga mwenyewe?

Ni kweli wote wanaogangwa ni waislamu hakuna wakiristo ambao hawamuamini hata huyo Allah (S.W)?
 
Unatakiwa wewe kutoa aya inayoonesha kuna kinga ya kutovamiwa na jinni
Aya nishaweka huko nyuma labda niirudie
Surat Az-Zukhruf (43:36)
“Na anayegeuka na kujiepusha na kumkumbuka Mwingi wa Rehema, tunamwekea shetani, naye ndiye anakuwa mwandamizi wake.”

Pia imesuniwa unapoingia na kutoka chooni usome dua ili kujikinga na viumbe wabaya

1. Wakati wa kuingia chooni

Imepokewa na Anas bin Malik (RA):

Mtume ﷺ amesema:

“Wakati mmoja wenu anapoingia chooni, na aseme:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخُبُثِ وَالْخَبَائِثِ
(Allahumma inni a‘udhu bika minal-khubuthi wal-khabaa’ith)
‘Ewe Allah! Najikinga kwako na majini wa kiume na wa kike (waovu).’”
— (Hadith: Bukhari na Muslim)

2. Wakati wa kutoka chooni 🚶‍♂️

Imepokewa na Aisha (RA):

Mtume ﷺ alipokuwa akitoka chooni alikuwa akisema:

“غُفْرَانَكَ”
(Ghufraanaka)
“Naomba msamaha Wako (Ee Allah).”
— (Hadith: Abu Dawud, Tirmidhi, Ibn Majah, na Ahmad – imethibitishwa na Al-Albani)
 
Kwenye uganga unakuta mtu anaweza kujua kiarabu kidogo cha kujua kusoma na akaweza kusoma Qur'an basi hahitaji kusoma mambo mengine zaidi wala kuwa mjuzi sana wa Qur'an,
Mtu anasomea falaq tu inamtosha Hana haja na kujua dini na mengine ya ibada masheikh wetu mpo vizuri
 
Mleta mada aje kulizungumzia hili Kazanazo
Ukiona jini muasi kakuingia angalia namna ya ufanyaji ibada zako jinni muasi hawezi kuingia kwa muumini na hawakai sehemu Safi na twahara

Ibada anaijua Mungu muumba kuwa huyo mja anafanya ibada thabiti au anacheza shele sasa mkuu gallow bird una uhakika gani hao masheikh wako wanafanya ibada ya ukweli au kumbe wana mauza uza mengine wewe ni Mungu hadi uje na hilo hitimisho
 
Allah anasema katika Surat- dhaariyat(51)

51:56 - Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.

Kwa maana majini ni viumbe kama tulivyo binadam na wote tumeumbwa tuje tumuabudu Mungu peke ake na sio kitu kingine
Hapa ndipo huwa nahitimishaga kuamini kuwa Allah sio Mungu huyu anaehusudiwa na kuabudiwa na wakristo na watakatifu.

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom