Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

2 way system......
Muislamu akisoma sana dini anakuwa mganga
Lakini mgalatia akifeli elimu ndio anakuwa Nabii.....
 
Kuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.

Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki

Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim

98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,

98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,

98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka

98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?

Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.

Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama

NB, tujadili kistaarabu
Kheee wenye uchawi wao nao hawataki ku8ngiliwa kama wanasiasa ,mana huku usichangaye dini na siasa huku nako usichanganye dini na uchawi sasa hawa watu wakimbilie wapi?
 
Aya nishaweka huko nyuma labda niirudie
Surat Az-Zukhruf (43:36)
Shetani siyo jini,hata mtu anaweza kuwa shetani, ushetani ni sifa siyo kiumbe,rejea albaqara..'wanapokua na waumini husema tumeani,wanaporejea kwa mashetani wao husema hakika sisi tu pamoja nanyi...'
Pia imesuniwa unapoingia na kutoka chooni usome dua ili kujikinga na viumbe wabaya

1. Wakati wa kuingia chooni

Imepokewa na Anas bin Malik (RA):

Mtume ﷺ amesema:


اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخُبُثِ وَالْخَبَائِثِ
(Allahumma inni a‘udhu bika minal-khubuthi wal-khabaa’ith)
‘Ewe Allah! Najikinga kwako na majini wa kiume na wa kike (waovu).’”
— (Hadith: Bukhari na Muslim)

2. Wakati wa kutoka chooni 🚶‍♂️

Imepokewa na Aisha (RA):

Mtume ﷺ alipokuwa akitoka chooni alikuwa akisema:


(Ghufraanaka)
“Naomba msamaha Wako (Ee Allah).”
— (Hadith: Abu Dawud, Tirmidhi, Ibn Majah, na Ahmad – imethibitishwa na Al-Albani)
Hadithi ni porojo tu,kuna imam alikua akifanya yote hayo lakini bado jini linamsakama hadi leo
 
Ukiona jini muasi kakuingia angalia namna ya ufanyaji ibada zako jinni muasi hawezi kuingia kwa muumini na hawakai sehemu Safi na twahara

Ibada anaijua Mungu muumba kuwa huyo mja anafanya ibada thabiti au anacheza shele sasa mkuu gallow bird una uhakika gani hao masheikh wako wanafanya ibada ya ukweli au kumbe wana mauza uza mengine wewe ni Mungu hadi uje na hilo hitimisho
Wewe elimu ndogo, ndiyo umeanza kuitafuta,bado una jazba na (elimu ya) dini,yaani mtu anaswali hadi kisimamo usiku kila siku unasema swala yake mushkeli..nabii ayyub nae alikua mchafu?
 
Usiwe mwepesi wa kuwagawa watu kisa umepewa hoja kinzani hapa tunajadili Qur'an na Sunnah hatumjadili mtu
Salafi/wahabi huona wao wasafi kuliko wengine, ilhali wanafuata fatwa za wanazuoni wao(ushirikina) na si Quran
 
Twende na huyu huyu sheikh yahya,huyu ni sheikh(mwaalimu),na alikuwa mtu wa visomo kabisa hata kutabiri nyota,kwanini unafikiri sikujua nilichoandika niliposema wasomi wazuri ndio waganga wa Quran??

Ndio maana nikasema (MGANGA)nikiwa nina maana kabisa lazima awe mtaalam kabisa maana yake ni tabibu wa kutegemewa,sio msomaji tu.

Manabii feki wewe unawapimaje??una uhakika gani tukiwachambua kwamba hata nabii unayemfuata hatafuatana nao kwenye huo ufeki??tuwaheshimu tu,maana mwenye hukumu ni Mungu tu.

Wachawi hupenda kutumia Quran maana ina sura zinazoshabihiana na kazi zao,over.
Waganga wako wengi mkuu sasa mbona hawaitwi kuwa ni mabingwa wa usomaji wa Qur'an kama Sheikh Yahya? Nitajie mganga mwengine mbali na sheikh Yahya ambaye ni mjuzi sana wa Qur'an?

Nimekwambia wapo waganga ambao elimu zao ni ndogo sana kwenye utabibu.

Mimi nimesema manabii feki wala sijamnyooshea kidole yeyote na sio nafasi yangu kuwapima katika hao manabii kujua yupi feki na asiye feki hilo nawaachia wenye kuamini hao manabii, labda uniambie hakunaga manabii feki manabii wote ni manabii wa kweli.

Uchawi umekatazwa kwenye Qur'an kwahiyo kama wachawi wanatumia Qur'an basi ni kwa imani zao ni kama tu wachawi hao hao kwa imani zao wanavyotumia maandiko ya Zaburi.
 
Ukiona jini muasi kakuingia angalia namna ya ufanyaji ibada zako jinni muasi hawezi kuingia kwa muumini na hawakai sehemu Safi na twahara

Ibada anaijua Mungu muumba kuwa huyo mja anafanya ibada thabiti au anacheza shele sasa mkuu gallow bird una uhakika gani hao masheikh wako wanafanya ibada ya ukweli au kumbe wana mauza uza mengine wewe ni Mungu hadi uje na hilo hitimisho
Kwahiyo kinga ni kufanya ibada tu ya kweli au kumuomba Mungu akukinge na shetani?
 
Salafi/wahabi huona wao wasafi kuliko wengine, ilhali wanafuata fatwa za wanazuoni wao(ushirikina) na si Quran
Hapa hatujadili madhehebu tunajadili ushirikina katika dini tena hatubishani tunaelimishana
 
Kheee wenye uchawi wao nao hawataki ku8ngiliwa kama wanasiasa ,mana huku usichangaye dini na siasa huku nako usichanganye dini na uchawi sasa hawa watu wakimbilie wapi?
Wenye uchawi wao akina nani
 
Majini ni roho chafu zitokanazo na Licifer na malaika walioasi Mbinguni pamoja nae. Wanamuabudu vipi Mungu waliyemuasi na sio yule muasisi wa uasi waliyeamini anaweza kuwa Mungu wao? Kwa sababu hata sasa baada ya kushindwa vita na ufalme wa Mbinguni, wanaendeleza vita na viumbe wa Mungu ambao ni wanadamu walio upande wa Mungu hapa duniani.

Maandiko yanasema sababu ya yule muasi kupigana vita na wanadamu ni wivu kwa kuwa Mungu alituumba kwa mfano wake na kutupa mamlaka juu ya viumbe vyote vinavyokatiza hapa duniani wakiwemo Lucifer na hao malaika walioasi na majini. Yule muasi akituona ni anaona image ya Mungu aliyeshindwa kumpindua na kuchukua nafasi yake hivyo chuki yake kwetu ni thabiti.

Kinachowapa faraja: muasi na majeshi yake wakiwemo majini ni kuwa, kuna wanadamu wapumbavu wenye kiburi cha kujiona wana maarifa mengi walioamua kumuasi Mungu wao na kushirikiana na majeshi ya muasi Lucifer kumuabudu na kutumika na huyo muasi kama vyombo vya kuleta uharibifu kwa wanadamu ambao hawajaasi kwa Mungu wao.
 
At least umeanza kuleta Aya na hadithi ndio maana nikasema hapo tunaenda pamoja sasa

Japo umetoa hadithi but gallow bird anasema hadithi ni porojo
Kama umekubali kisomo cha ruqya na kwamba inafaa kusomewa au kumsomea mtu mwengine hapo sawa.
 
Back
Top Bottom