Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Ni dhambi kubwa sana kumshirikisha Mwenyezi Mungu

4. Surah Az-Zumar (39:65)
Yani nauchukia sana uganga ,nikikujua unaenda kwa waganga wewe kwangu unakula x mkasi sipendi na nauchukia shiriki, sawa naweza nikawa nimemkose Mungu dhambi nyingine ila sio ya kwenda kwa waganga ni mbaya na hovu na haitubiki kirahisi
 
Yani nauchukia sana uganga ,nikikujua unaenda kwa waganga wewe kwangu unakula x mkasi sipendi na nauchukia shiriki, sawa naweza nikawa nimemkose Mungu dhambi nyingine ila sio ya kwenda kwa waganga ni mbaya na hovu na haitubiki kirahisi
Masheikh tunguli na mazingahombwe mengine wanaharibu taswila ya uislamu wale wanaofuata dini kwa usahihi huitwa extremist

Waafrika tumeletewa dini tukazipokea lakini hatupo tayari kufuata maamrisho yaliyomo bali tunachanganya na mila zetu ili kujinufaisha duniani
 
Mbona mnasema yanawasaidia kupata hela?
Kama watu wapo tayari kuua kupata hela watashindwa kutumia majini?

Kitendo cha kufanya jambo ovu kupata pesa haihalalishi jambo hilo kuwa jema hivyo basi kutumia majini kupata pesa ni ushirikina na Mungu ametukataza

1. Surah An-Nisa (4:36)
"Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote..."
 
Wachungaji wenu ndivyo wanavyo wakaririsha hamna mjualo zaidi ya propaganda na hampo tayari kuelimishwa
Muhammad alitokewa na jini pangoni siyo malaika mtakatifu....muhammad kapewa utume na mkewe na yahudi wa kikatoliki ...muhammad kauliwa na sumu kutoka kwa mchepuko wake wa kiyahudi (muisraeli) uliokuwa unamtumikia ...muhammad alifuga jini ....na jini lilikuwa lina msaidia kwenye utume wake .....
 
Mimi ni Mkristo, lakini wewe mleta mada unawafahamu vizuri waKristo unawafahamu vizuri kabisa? Na viongozi wao unawafahamu vizuri?

Ungewafahamu basi ungewajumuisha kwenye bandiko lako...!

Na waKristo ni wabaya kuliko waIslam, usiniulize kwanini...
Ni kweli siku hizi dini zimekuwa chimbo la kufanyia ushirikina hapa nimesema niwakumbushe masheikh zangu wanajisahau sana
 
Muhammad alitokewa na jini pangoni siyo malaika mtakatifu....muhammad kapewa utume na mkewe na yahudi wa kikatoliki ...muhammad kauliwa na sumu kutoka kwa mchepuko wake wa kiyahudi (muisraeli) uliokuwa unamtumikia ...muhammad alifuga jini ....na jini lilikuwa lina msaidia kwenye utume wake .....
Sina muda wa kujadili propaganda hata hivyo andiko langu linawalenga masheikh sasa wewe mgalatia naona unatumia mada yangu kuleta propaganda zako za uongo anzisha mada watakao kuwa tayari watakufuata mjadili
 
Kitabu mahsusi kwa ajili ya Majini, kibafanya nini ndani ya Quran?
Qur'an ni kitabu kimoja ila zipo Aya na Surah zinaelezea kuhusu viumbe majini

Kipindi cha ujahilia/ujinga makafiri walimuuliza Mtume Muhamad (amani iwe juu yake) kuhusu hivyo viumbe na Mwenyezi Mungu akashusha Surat jinni kuelezea hao majini ni viumbe wa namna gani. Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake katika suratul jinni

72:1 - Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!

72:2 - Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.

72:3 - Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.

72:4 - Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.

72:5 - Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.

72:6 - Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.

72:7 - Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.

72:8 - Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.

72:9 - Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!

72:10 - Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.

72:11 - Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.

72:12 - Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.

72:13 - Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.

72:14 - Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.

72:15 - Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.

72:16 - Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi,

72:17 - Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.

72:18 - Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.

72:19 - Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!

72:20 - Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote.

72:21 - Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.

72:22 - Sema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.

72:23 - Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.

72:24 - Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.

72:25 - Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu.

72:26 - Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,

72:27 - Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

72:28 - Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.
 
Wapuuzi hao wanatuharibia dini yetu, sio kwamba ati hawajui. SHIRKI ndio dhambi kubwa zaidi katika Uislam
 
Huo uganga wa kitabu ni shirki ndugu yangu kama unajifunza ili kuwa miongoni mwao acha Mara moja utaingia hasarani siku ya kiyama

Huo uganga wa miti shamba unaruhusiwa ila usihusishwe na maombezi ya kishirikina uwe ni kama dawa za hospital tu kama wale wanaouza dawa za asili

Kuna wengine hutumia Adhana kuagua hizi zote ni shirki tujiepushe nazo
Mkuu nikisema nikuulize maswali ili nielewe vizuri ni kipi hasa ni ushirikina unaniambia natetea ushirikina na kuanza kunipa onyo, hapo unasema mitishamba inaruhusiwa isipokuwa tu yasitumike maombezi ya kishirikina, je vp dawa za mitishamba ambazo hujulikana kutibu hadi uchawi kwa kutumia tu pasina kufanya maombi yeyote nayo ni ushirikina?
 
Mkuu nikisema nikuulize maswali ili nielewe vizuri ni kipi hasa ni ushirikina unaniambia natetea ushirikina na kuanza kunipa onyo, hapo unasema mitishamba inaruhusiwa isipokuwa tu yasitumike maombezi ya kishirikina, je vp dawa za mitishamba ambazo hujulikana kutibu hadi uchawi kwa kutumia tu pasina kufanya maombi yeyote nayo ni ushirikina?
Mfano dawa gani
 
Wazungu wa wapi,taja eneo specific.

Novena hii ni sala isiyohusisha mitishamba,zaidi ya kuisoma na kufunga tu ukiombea jambo.
na huyu dada mmoja hawezi kufanya ukafikia tamati kwamba biblia ni nyenzo ktk field hiyo.

Wala sijakariri nakwambia kitu ninachokijua,soma sana uwe mganga mzuri kama dr sure au sharif majini.
Dini yenu ni nzuri sana imekamilika.
Moja ya kitabu cha wazungu chenye kufundisha uchawi kwa kutumia maandiko ya biblia. Huyo dada ni mfano mmoja tu nimekupa kutokea hapa hapa Tanzania ili kuonyesha kwamba hata biblia inatumika pia.

Kuhusu Novena sijasema inahusishwa na mitishamba bali inaweza kutumika kumuangamiza adui au kulipiza kisasi, kwa kifupi sioni kama inatofauti na Albadir.
 

Attachments

  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    45.7 KB · Views: 18
Kwani nani kawaumba majini?
Kama alivyo mwumba Ibirisi:
Ni hiyari yake kuumba chochote anacho kipenda:

Majini ni koo za Ibirisi:
Hebu niambie Jini kafanya jambo gani jema ?
Yanatumika katika urozi tu na uchawi:
 
Kwakuwa majini yamejitambulisha kuwa dini yao ni Uislamu:
Ni lazima kiongozi wa Kiislamu ajue wanashirikiana vipi nao katika ibada:
Maana mtume wao ni Muhamadi na yanaswali misikitini:
Kwahiyo Mashehe na Maimamu ni lazima wajue uhusiano wa waislamu watu na Waislamu majini:
Katika kujua huko ndiko kunakowapelekea kuwa wachawi:
Muhamadi alisema Majini ni ndugu wa Waislamu, muislamu ameambiwa ampende Jini Muislamu kuliko mtu asiye Mwislamu:
(Kafiri)Hapo mtakosaje kuwa wachawi ?

Je kama mwislamu umefanya juhudi gani kukutana na ndugu yako wa Kijini?
Kama alivyofanya mtume Muhamadi?
 
Tulisema hakuna majini mema:
Mwema ni Mungu peke yake:
Shida ya kusema majini wema inakuwa kama majini wamegawanywa makundi mawili tu kwamba kuna waovu tu moja kwa moja na kuna wachangamungu moja kwa moja kama malaika.
 
Kama alivyo mwumba Ibirisi:
Ni hiyari yake kuumba chochote anacho kipenda:

Majini ni koo za Ibirisi:
Hebu niambie Jini kafanya jambo gani jema ?
Yanatumika katika urozi tu na uchawi:
Ibirisi ni jinn alieasi miongoni mwa majini kuna walioasi ambao hawamuamudu Mungu nao ndio huitwa ibirisi au mashetani

Sawa na binadamu miongoni mwetu wapo makafiri ambao hawamuamudu Mungu mmoja
 
Back
Top Bottom