Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Jambo jema ukiwa mganga wa kikristo hutumii biblia kutibu.
Kwani waganga wote ambao ni waislamu hutumia kitabu? Navyojua kuna uganga wa majini,tunguli na vitabu. Ila pia mkuu hata maandiko ya biblia hutumika kufanyia uganga hasa Zaburi.
 
Mkuu hauoni kama kutaja shirki ni rahisi kuliko kuelezea ni ipi hasa hiyo shirki na ipi sio shirki?
 
Unawaonea Bure mashehe. Mfumo mzima wa dini hiyo ndivyo ulivyo. Kitendo Cha kukubali kuwa na Imani Moja na majini ambayo ndiyo baba wa ushirikina duniani ndio kosa kubwa. Fanya tafiti Kila nje ya nyumba zao za ibada Kuna waganga wa kienyeji na machupa chupa yaadawa ya kienyeji mengi ni Yale yanayoua figo na moyo eti waongeze nguvu za kuwatosheleza wake 4 na vimada lundo. Mwisho wa siku wanaishia dialysis na moyo kusimama wakiwa guest
 
Kwani waganga wote ambao ni waislamu hutumia kitabu? Navyojua kuna uganga wa majini,tunguli na vitabu. Ila pia mkuu hata maandiko ya biblia hutumika kufanyia uganga hasa Zaburi.
Hakuna hicho kitu,hakuna mganga yeyote utakuta anakusomea bible wala kuihusisha na hayo madude.
 
Mkuu hauoni kama kutaja shirki ni rahisi kuliko kuelezea ni ipi hasa hiyo shirki na ipi sio shirki?
Unatumia nguvu nyingi kuilezea shirk wakati ipo bayana kabisa kama unafanya hivyo vitendo acha utaingia motoni
 
Wagalatia mlio wengi hamna elimu juu ya majini kwenye hili mnahitaji darsa
 
Hivi kwani uganga unatenganishwa na uislam? Maana huku huwa naona wahuni wakiamua kuwa waganga wanaslimu kabisa. Tena baadhi wanajenga na misikiti midogo nyumbani!
Ndy uislam na uganga ni vitu viwili tofauti uganga/uchawi ni shirki
 
Ndivyo utaratibu wenu ulivyo, ama wewe huijui vizuri inachotaka Quran
 
Yaani tukomae na uarabu tuachane na Uafrika wetu? Hapa ndipo tulipopigwa za uso na hawa watu weupe
Mkuu dini hailazimishwi ila ukiamua kuifuata ifuate kama ilivyoelekezwa haitakiwi kuchanganya

Kama umeamua kuwa mganga kuwa mganga roga uwezavyo lakini kama umeamua kuwa mtu wa dini basi acha mila zote zilizokatazwa na Mwenyezi Mungu kupitia dini
 
Nukuu nzuri kiufupi hakuna dini inayoruhusu uchawi na uganga hizo ni mila zetu waafrika ambazo hatukubali kuziacha lakini pia mafundisho ya dini nayo tunayaelewa na pepo tunaitaka na siku zote haki na batili havichangamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…