Kweli aisee. Ndio maana yule Jaji alisema ameahirisha kesi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Welldone Mama Samia kwa kutokumbatia chuki za watangulizi wako.

'Apandae Chuki huvuna chuki, apandae upendo huvuna upendo'.
Hakika wote walioonewa na Yule mwovu bila kuangalia vyama na udini wawe huru. Tujenge nchi wote Kwa upendo kila mmoja na mchango wake.
 
Wakiachiwa wafungwa wote itapendeza zaidi. Ndani kule kubaya ndugu zangu, au nasema uongo?!!
Ukiwa kiongozi jitahidi kuboresha maslai ya jela Ili kesho ukiingia usilale pa bovu.
 
What next? Nani atavishwa kengele? Cia mossad in Tz?
 
[emoji117]Unakaa jela zaidi ya miaka 9, unateseka weee familia inakosa huduma yako kwa muda wote huo

[emoji117]Baada ya miaka mingi kupita DPP Anafuta kesi yako na kukuruhusu uende nyumbani

[emoji117]Unaenda nyumbani ukiwa umeathirika kisaikolojia, biashara zako/kazi zinakuwa zimekufa na muda mwingine huna pesa kabisa hivi unaishije?

[emoji117]Huwa kuna kesi hazina dhamana mtu anakaa jela wee halafu baadae anashinda kesi au DPP anafuta hiyo kesi huyu nae anaambiwa aende nyumbani tu huko anaenda kuishije?

[emoji117]Wataalamu hebu mnisaidie huwa wanapewa pesa kufidia muda walio kaa gerezani?au wanaachwa tu? Kama wana waachwa tu hili liangaliwe wawe wanapewa fidia

[emoji117]Mtu anakaa gerezani miaka sita mfano kesi ikiwa anaendelea mwaka wa saba anapewa hukumu ya kufungwa miaka 15 jela (mfano).. Je, kuna fidia ya ile miaka sita aliyo kaa kabla ya hukumu?

~Karibuni
 
Masheikh wametoka na madai yao yapo pale pale.

Haki hupatikani tu kikubwa kinachoweza kufanyika ni kucheleweshwa kwa haki hiyo
 
Acha maneno yako maovu. Wewe utakuwa na matatizo yako tu kila tukio saizi kazi yenu ni kumhusisha Magufuli.Mnasema hammpendi sawa, ameshakufa mnataka nini?
 
Hao sasa hivi watakuwa watiifu sana kwa jamhuri miaka 9 wameshakuwa brainwashed kwelikweli hapo ukijichanganya uende na mambo ya tuachwe tupumue ukimaliza tu kuongea nao kabla hujashika kitasa cha mlango utoke tayari utakuwa mikono salama
Si mlisema hawatatoka milele.

P.mbaaaaaaav sana
 
Naulizia hivi;

Je huko gerezani hakuna wengine ambao wamekaa zaidi ya muda huo ?

Je nao wametolewa?


Kama ni haki inapaswa kutolewa kwa watu wote hata wasio amini yani wapagani ilimradi ni binadamu wameumbwa na Mungu.
Masheikh tu wapo zaidi ya mia waliyokamatwa na kesi kama hizi ukiacha na hao wa uamsho, kiujumla wapo watu wengi tu waliyoshikiliwa huko kwa muda mrefu.
 
Kweli aisee. Ndio maana yule Jaji alisema ameahirisha kesi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Welldone Mama Samia kwa kutokumbatia chuki za watangulizi wako.

'Apandae Chuki huvuna chuki, apandae upendo huvuna upendo'.
Tunasisitiza tena na tena na tena kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.

In shaa Allah kwa uwezo wa Mungu mpaka ndugu na jamaa wa Saanane watajua kuhusu ndugu yao.

Give Mama time and everyone will enjoy being Tanzanian again.
 
Acha maneno yako maovu. Wewe utakuwa na matatizo yako tu kila tukio saizi kazi yenu ni kumhusisha Magufuli.Mnasema hammpendi sawa, ameshakufa mnataka nini?
Atujawahi pata mtu dhalimu kama yule thus tunaomba dua Mola aepushe marudio.
Wewe kama ulinufaika zamu yenu kuumia sisi tupo na furaha dua yetu kwa Mola ameipokea.Raha mustarehe hatuna pesa lakini tuna amani tele, Hakuna kutekana tena, kubambikwa kesi,pesa bank zipo salama,viroba baharini Hakuna,bei ya korosho ni kicheko tu mwaka huu, wasiojulikana wapo likizo ya milele.Mola atupe nn tena.
 
Huku kwetu ukiwa incarcerated for a crime you didn't commit na baadae ukawa vindicated....basi tunakulipa USD 400,000 kama kifuta machozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…