Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
Kweli aisee. Ndio maana yule Jaji alisema ameahirisha kesi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Welldone Mama Samia kwa kutokumbatia chuki za watangulizi wako.

'Apandae Chuki huvuna chuki, apandae upendo huvuna upendo'.
Hakika wote walioonewa na Yule mwovu bila kuangalia vyama na udini wawe huru. Tujenge nchi wote Kwa upendo kila mmoja na mchango wake.
 
Wakiachiwa wafungwa wote itapendeza zaidi. Ndani kule kubaya ndugu zangu, au nasema uongo?!!
Ukiwa kiongozi jitahidi kuboresha maslai ya jela Ili kesho ukiingia usilale pa bovu.
 
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

SHEIKH MSELEM SHEIKH FARID WAKO NYUMBANI ZANZIBAR

Masheikh zetu wawili wako majumbani kwao na familia. Tutaendelea kukupeni taarifa awamu kwa awamu.

Lengo ni kutoa taarifa za kweli na zilizozingatia mambo yote muhimu.

Aidha viongozi wa Shura Taifa wako angani wakielekea Zanzibar.

Ibrahimu Zuberi Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania
0713118812

=======

Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu ameieleza Mwananchi Digital leo Jumatano Juni 16, 2021 kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Wawili hao ambao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana wameachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021 baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Taarifa za kuachiwa huru kwa viongozi hao zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana jioni zikieleza kuwa viongozi hao wawili ndio wameachiwa huru na mmoja wa mawakili wao, Juma Nassoro amelieleza Mwananchi Digital kuwa wameshapelekwa majumbani mwao.

Katika ufafanuzi wake Mwakitalu amesema, “ni kweli wameachiwa huru. Nimewafutia wote mashtaka yaliyokuwa yanawakabili. Sasa suala la kutoka gerezani kama wameshatoka wote au wangapi hilo ni suala la taratibu za Magereza lakini mimi nimewafutia mashtaka wote.”

Washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kujihusisha na makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002 Januari 2013 na Juni 2014.

Awali walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua za awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa usikilizwaji kamili wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 25.

Lakini Aprili 23, 2021 Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka 14 baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wao, Daimu Halfani, Juma Nassoro, Jeremiah Mtobesya na Abubakar Salum kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo kwa kuwa makosa wanayotuhumiwa yanadaiwa kutendeka Zanzibar.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake huo uliotolewa na Jaji Mustapha Ismail baada ya kusikiliza hoja za pande zote, hoja za pingamizi la utetezi na majibu ya upande wa mashtaka ulioongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga akisaidiwa na wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Paul Kadushi, ilikubaliana na hoja za utetezi.

Jaji Ismail alisema pamoja na mambo mengine kuwa kwa makosa ambayo yanadaiwa kutendeka Zanzibar, jukwaa sahihi la kuwashtaki washtakiwa ni katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji Ismail aliuamuru upande wa mashaka kufafanua marekebisho katika hati ya mashtaka kwa kuyaondoa mashtaka hayo na kubakiza yale ambayo yamedaiwa kutendeka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara ambayo ndio mahakama hiyo ina uwezo wa kuyasikiliza.

Zaidi, soma:
-
Sheikh Ponda ampongeza Mkurugenzi mpya wa mashtaka(DPP) kukutana na Masheikh wa Uamsho Gerezani
- Mufti Abubakari Zuberi ahimiza uharaka kesi ya mashehe wa Uamsho
What next? Nani atavishwa kengele? Cia mossad in Tz?
 
[emoji117]Unakaa jela zaidi ya miaka 9, unateseka weee familia inakosa huduma yako kwa muda wote huo

[emoji117]Baada ya miaka mingi kupita DPP Anafuta kesi yako na kukuruhusu uende nyumbani

[emoji117]Unaenda nyumbani ukiwa umeathirika kisaikolojia, biashara zako/kazi zinakuwa zimekufa na muda mwingine huna pesa kabisa hivi unaishije?

[emoji117]Huwa kuna kesi hazina dhamana mtu anakaa jela wee halafu baadae anashinda kesi au DPP anafuta hiyo kesi huyu nae anaambiwa aende nyumbani tu huko anaenda kuishije?

[emoji117]Wataalamu hebu mnisaidie huwa wanapewa pesa kufidia muda walio kaa gerezani?au wanaachwa tu? Kama wana waachwa tu hili liangaliwe wawe wanapewa fidia

[emoji117]Mtu anakaa gerezani miaka sita mfano kesi ikiwa anaendelea mwaka wa saba anapewa hukumu ya kufungwa miaka 15 jela (mfano).. Je, kuna fidia ya ile miaka sita aliyo kaa kabla ya hukumu?

~Karibuni
 
Hili swala Ni sensitive Sana kwa nchi yetu lakini watu wanalichukulia kisiasa lakini huko mbeleni hawa masheikh wataleta shida sana.kwa Yale mahubili yao ya kuhamadisha vulugu halafu Leo wanaachiwa huli.Tena ikizingatiwa Mambo yaliyopo Msumbiji sijui nini kitatokea.Labda watakua monitored by government nje ya hapo hawa jamaa sio watu wazuri kwa mstakabali wa nchi yetu.N mawazo yangu Wala Sina chili nao.
Masheikh wametoka na madai yao yapo pale pale.

Haki hupatikani tu kikubwa kinachoweza kufanyika ni kucheleweshwa kwa haki hiyo
 
Eee..!.Mungu Baba Mwenyezi twakuomba uliepushe taifa letu lisije tena likapata watawala dhalimu kama jiwe milele na milele sio leo,kesho na hata vizazi vyetu vijavyo.Nafunga katika Jina la YESU jina kuu kuliko majina yote.Nikiomba na kuamini hakika hakuna kiongozi dhalimu tena ataketokea katika taifa hili katika Jina la YESU Kristo ulie hai.! Nateketeza kwa moto ulao ! roho zote chafu za viongozi kama Sabaya bashite zisiinuke tena katika taifa hili milele na milele.Tukiomba na kuamini.Na KILA mmoja na aseme.Amee...ni !
Acha maneno yako maovu. Wewe utakuwa na matatizo yako tu kila tukio saizi kazi yenu ni kumhusisha Magufuli.Mnasema hammpendi sawa, ameshakufa mnataka nini?
 
Hao sasa hivi watakuwa watiifu sana kwa jamhuri miaka 9 wameshakuwa brainwashed kwelikweli hapo ukijichanganya uende na mambo ya tuachwe tupumue ukimaliza tu kuongea nao kabla hujashika kitasa cha mlango utoke tayari utakuwa mikono salama
Si mlisema hawatatoka milele.

P.mbaaaaaaav sana
 
Naulizia hivi;

Je huko gerezani hakuna wengine ambao wamekaa zaidi ya muda huo ?

Je nao wametolewa?


Kama ni haki inapaswa kutolewa kwa watu wote hata wasio amini yani wapagani ilimradi ni binadamu wameumbwa na Mungu.
Masheikh tu wapo zaidi ya mia waliyokamatwa na kesi kama hizi ukiacha na hao wa uamsho, kiujumla wapo watu wengi tu waliyoshikiliwa huko kwa muda mrefu.
 
Kweli aisee. Ndio maana yule Jaji alisema ameahirisha kesi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Welldone Mama Samia kwa kutokumbatia chuki za watangulizi wako.

'Apandae Chuki huvuna chuki, apandae upendo huvuna upendo'.
Tunasisitiza tena na tena na tena kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.

In shaa Allah kwa uwezo wa Mungu mpaka ndugu na jamaa wa Saanane watajua kuhusu ndugu yao.

Give Mama time and everyone will enjoy being Tanzanian again.
 
Acha maneno yako maovu. Wewe utakuwa na matatizo yako tu kila tukio saizi kazi yenu ni kumhusisha Magufuli.Mnasema hammpendi sawa, ameshakufa mnataka nini?
Atujawahi pata mtu dhalimu kama yule thus tunaomba dua Mola aepushe marudio.
Wewe kama ulinufaika zamu yenu kuumia sisi tupo na furaha dua yetu kwa Mola ameipokea.Raha mustarehe hatuna pesa lakini tuna amani tele, Hakuna kutekana tena, kubambikwa kesi,pesa bank zipo salama,viroba baharini Hakuna,bei ya korosho ni kicheko tu mwaka huu, wasiojulikana wapo likizo ya milele.Mola atupe nn tena.
 
Huku kwetu ukiwa incarcerated for a crime you didn't commit na baadae ukawa vindicated....basi tunakulipa USD 400,000 kama kifuta machozi.
 
Back
Top Bottom