Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 422
- 489
Hicho ndicho kichochoro wanachokimbilia wale masheikh na walimu watetezi wa mambo ya ushirikina na uchawi wanapokosa hoja ya kutetea uchawi wao hukimbilia kufananisha uchawi na mambo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.Tuseme tu Mungu mwenyewe ndio mjuzi zaidi ila ukiangalia dunia ilipofika ambapo tunaweza kuwasiliana na mtu ambaye yupo mbali sana na wewe tena pengine pasina hata kumjua wala kumuona, hivyo pengine tatizo baadhi ya hizo njia zitumikazo kuwasiliana na hao viumbe.
Ni WAONGO SANA.
Kuagua na kupiga ramli wanasema ni sawa na X-ray na Ultrasound!
SIO KWELI!
Ushirikina na uchawi vimekuwepo kwa Karne nyingi sana tangu enzi za Nabii Nuhu عليه السلام na mitume na manabii wote walikuja kuwatahadharisha wafuasi wao waepukane na mambo ya Ushirikina kama anavyosema Allaah katika Suurat Annahli Aya ya 36 ya kwamba :
"{ وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّٰغُوتَۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنۡهُم مَّنۡ حَقَّتۡ عَلَيۡهِ ٱلضَّلَٰلَةُۚ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ }
Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: MUABUDUNI ALLAAH, NA MUEPUKENI SHETANI. Basi kati yao wapo alio waongoa ALLAAH. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kakadhibisha".
Na kuhusu wanaadamu kutaka msaada kwa majini , majini wenyewe baada ya kusilimu walibainisha kwamba walikuwa wakiwasaidia baadhi ya watu waliotaka msaada na wao wakawaamrisha kufanya madhambi ikiwa ni sharti la kupata msaada waitakao hao watu kama walivyosema majini katika suuratul jinni Aya ya 6 kwamba :
"{ وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٞ مِّنَ ٱلۡإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٖ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَزَادُوهُمۡ رَهَقٗا }
Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga ( kutaka hifadhi na msaada )
kwa wanaume wa kijini; KWA HIVYO WAKAWAZIDISHIA MADHAMBI."
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Kuna madhambi saba ambayo kayaita kuwa ni yenye kuangamiza na na dhambi ya kwanza kataja ni ushirikina na dhambi ya pili ni uchawi kama ilivyo katika hadithi aliyopokea Imamu Albukhary kutoka kwa swahaba Abuu Huraira kwamba mtume صلى الله عليه وآله وسلم
kasema: اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ ". قَالُوا : يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا هُنَّ ؟ قَالَ : " الشِّرْكُ بِاللَّهِ، وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافِلَاتِ ".
Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza .
Wakasema: Ee mjumbe wa Allaah ni yepi hayo ?
Aksema:
" 1️⃣ kumshirikisha Allaah, na 2️⃣ Uchawi, na 3️⃣ Kuiua nafsi ( kuua mtu ) ambayo Allaah ameharamisha kuiua isipokuwa kwa haki , na 4️⃣ Kula riba , na 5️⃣ Kula mali ya yatima , na 6️⃣ Kukimbia siku ya vita ( kuwasaliti waislamu kwa kukimbia wakati wa mapambano na makafiri ) , na 7️⃣ Kuwasingizia ( dhambi ya uzinifu ) wanawake wenye kujitunza, waislamu, wasiofanya madhambi ya zinaa. Kwahiyo kufananisha uchawi na mambo ya sayansi ya kisiasa ni kutaka kuupotosha uislamu na kuwatoa waislamu kwenye njia ya sawa na kuwapeleka kwenye ushirikina.
Ushirikina na uchawi umekuwepo na umekemewa kwa maelfu ya miaka iliyopita kabla ya kudhihiri maendeleo ya sayansi ambayo imekuja ndani ya miaka 300 tu iliyopita. Na Lau kama mawasiliano kwa njia ya sayansi na teknolojia ingekuwa sawa na uchawi basi wanachuoni wanaotambulika duniani ( achana na hawa wahuni wa hapa TZ wanaohalalisha uchawi ) wangekuwa walishaandika vitabu kuwakataza waislamu kutumia mawasiliano ya sayansi na teknolojia .