Mashindano ya kumtafuta bingwa wa draft Tanzania 2022

EXCLUSIVE



Timu: Omary Kiwembe Vs Dogo Shukuru ( Confirmed )




Mdhamini : Mzee Java ( Raisi wa wakongwe wa madanali )




Zawadi: 70,000/= ( Winner 60k na looser 10k )




Lini: Alhamisi, tarehe 7 July 2022 Saa Tisa Kamili




Uwanja: kitunda stadium




Michezo: 24-Omary John + Tege 10 za mzee Ngapu



Mratibu: Masta Mtemi ( 5000)




Photograper:Masta mtemi( 5000 )




Kamisaa: Dogo Hansi (5000)




Note: Hakutakuwa na mshindi wa pili ila tutakuwa na nauli ya Shilingi elf 10 kwa atakaefungwa



Boss Java amefungua turbo vijana washindwe wao na Sasa Fundi Kiwembe anatembe kifua mbele,, Ikumbukwe tu Fundi Kiwembe alilala karibia miezi Sita bila ya kupata mechi njoo kitunda stadium
 
EXCLUSIVE



Timu: Omary Kiwembe Vs Generali Mboma ( Confirmed )




Mdhamini : Mzee Java ( Raisi wa wakongwe wa madanali )




Zawadi: 80,000/= ( Winner 70k na looser 10k )




Lini: Ijumaa, tarehe 8 July 2022 Saa Tisa Kamili




Uwanja: Mbagala Kizuiani




Michezo: 24-Omary John + Tege 10 za mzee Ngapu



Mratibu: Masta Mtemi ( 5000)




Photograper: Fidelisi( 5000 )




Kamisaa: Haji Nguya (5000)




Note: Hakutakuwa na mshindi wa pili ila tutakuwa na nauli ya Shilingi elf 10 kwa atakaefungwa



Boss Java amefungua turbo vijana washindwe wao na Sasa Fundi Kiwembe anatembe kifua mbele,, Ikumbukwe tu Fundi Kiwembe alilala karibia miezi Sita bila ya kupata mechi njoo Mbagala Kizuiani
 
EXCLUSIVE



Timu: Saiya Vs Mtanga ( Confirmed )




Mdhamini : Mzee Java ( Raisi wa wakongwe wa madanali )




Zawadi: 80,000/= ( Winner 70k na looser 10k )




Lini: Jumapili, tarehe 10 July 2022 Saa Nane kamili Mchana




Uwanja:Kitunda Stadium




Michezo: 24-Omary John + Tege 10 za mzee Ngapu



Mratibu: Masta Mtemi ( 5000)




Photograper: Masta Mtemi( 5000 )




Kamisaa: Riro (5000)




Note: Hakutakuwa na mshindi wa pili ila tutakuwa na nauli ya Shilingi elf 10 kwa atakaefungwa



Hii inaitwa mama Mkanye Mwanao Fundi Saiya anakwenda kukutana na Mtanga Uso kwa uso kama Semi trailer na kichwa cha treni Njoo mjini kitunda Stadium
 
EXCLUSIVE



Timu: Noeli Namaloe Vs Kiwembe




Mdhamini : Kamanda Issa ( Raisi wa watu huru )




Zawadi: 120,000/= ( Winner 100k na looser 20k )




Lini: Jumamosi tarehe 9 July 2022 Saa saba kamili mchana




Uwanja: Kinondoni Manyanya




Michezo: 24-Omary John + Tege kumi za Mzee Ngapu



Mratibu: Masta Mtemi




Photograper: Mkorea(5000)




Kamisaa: Beka ( 5000 )




Note: Hakutakuwa na mshindi wa pili ila tutakuwa na nauli ya Shilingi elf 20 kwa atakaefungwa na kama ngoma 24 zitaisha sare basi hawa jamaa watapewa elf 30 kila mmoja kama kifuta jasho
 
umedadavua vizur omary john hahah
 
Daah..ilinipa muda sana kuja kulizoea hili draft la kwenda mbele tu.

Eti kete inapita nyuma yako unaiacha tu daah..

#MaendeleoHayanaChama
 
Drafti ambalo king haimuvu kufuata kete iliyoko mbali haina tofauti na kibogoyo a aepambana kutafuna muhogo mbichi. Kunakuwa hakuna maana ya king sasa
 
Wacheze French Ili washiriki tuwe wengi ?
 
Aisee kuna mapambano makali sana naona round hii watu wameamua kuyaheshimisha hays mashindano kwa kuweka ligi nyingi zenye unafuu wa pesa tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilizoeleka kuwa mchezo wa draft ni mchezo wa watu waliokosa kazi au wahuni tu.

Bigi up kwa huyo java nimemuona akiwa mstari wa mbele sana kujiyolea kudhamini mapambano mengi.

Ipo siku hii michezo itakuwa na mashabiki wengi na itakuwa chanzo tegemezi cha uingizaji kipato kwa watu wengi japo saizi inachukuliwa kama passion tu.
 
Tusaidie na picha za mabingwa tuwajue hata kwa sura tu

Kuna umuhimu wa kuwajua maana wana kawaida ya kutembelea kwenye vijiwe tofauti tofauti na kujifanya matula wanaomba wazuilishwe sare

Wakicheza friend mechi wanacheza kipimbi ili wakuvute, ukiingia kingi kuwapa sare umeumia. Sio kama atakufunga ila atakuwa anakupelekea sare hizo hizo kwa mfumo wa kipimbi ili baadaye ubadirishe mkataba useme mfungane.

Ukisema mfungane hapo ndio umepotea mwisho wa siku ataondoka na jackpot halafu dakika ya mwisho ukajikuta wewe ndio unazulishwa sare moja na hiyo sare moja nayo huipati.
 
Mngeongea na azam wangefanya jambo...kama waliweza kuchezesha PlayStation wasingeshindwa kufanya jambo kwenye draft
 
Kwenye hayo mashindano makubwa naona hapo bingwa wa kijiwe chetu ni dogo hamis anatuwakilisha
 
Ungeandika bingwa wa mashindano ya draft ( british). Hata mwanza kuna wachezaji husafiri hadi Nairobi kucheza draft, sema vimwanaume vya dar kazi kujisifia tu eti vinajua draft wakati binti anakupita nyuma hata humtazami makalio 😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…