Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Cisco namskia ila personally simjui, ronaldo ana title kubwa huyu namjuaHumjui Cisco, Ronaldo? Noel yupo group E , alikula goli 5 kwa sisco
Aisee noel alipotea goli 5 kwa Cisco?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cisco namskia ila personally simjui, ronaldo ana title kubwa huyu namjuaHumjui Cisco, Ronaldo? Noel yupo group E , alikula goli 5 kwa sisco
Mkuu kama wote unapicha zao basi ziweke hapa wote tuwajueCisco huyu hapa
Yupo tayari muda wowote kukichafua ,
umedadavua vizur omary john hahahnaomba nikusaidie hapa , wanaposema washiriki watapitishwa na mikoa yao wana maana hii, mfano Iringa wachezaji wazuri wa draft tunawajua , sasa ni sisi wanairinga kuamua kupendekeza ni nani akatuwakilisha baada ya kujadiliana kwenye club zetu au kuamua kuandaa mashindano ambayo yatawakilisha wachezaji wotee wa mkoa afu mshindi atashinda ticket ya kwenda kutuwakilsha Dar es salaam katika mashindano ya kitaifa.
Baadhi ya mikoa kutokuwepo kabisaa , hii inatokana na mikoa hiyo kutokuwa na clubs za mchezo wa draft na kupelekea ugumu fulani katika kuwasiliana na wahusika wa mkoa usika lkn pia baadhi ya mikoa kutokuwa na upenzi na huu mchezo au kutokucheza huu mchezo katika sheria pendekezwa hapo juu. Mwisho ni baadhi ya mikoa (katika historia ) kutoa wachezaji wenye uwezo mdogo mnoo .
Unajua huu mchezo haupo kama wengi wajuavyo . Hawa wenzetu wa dar wametuzidi pakubwa mno ktk huu mchezo, kuna kigezo hapo cha omary john 14 hivi hapo umekielewa hicho kigezo ?
- ngoja nikufahamishe ni hivi, wachezaji wengi wanajiona au wanaitwa mabingwa kwasababu ana namna fulani ya kucheza huu mchezo , lkn katika omary john kila mcheza anatakiwa aanze kete zote 7 za vyumba vya mwanzo yaani anatakiwa aanze
Pasati , nugza , meja , kavimba, taa ya treni , mabano na tege . sasa wachezaji wengi wa mikoani utakuta anajua meja lakini mabano hajua au tege hajui , sasa mikoa iliyotajwa kidogo wanaufahamu juu ya hiyo sheria ya omary- john
Kwanin wanaiita omary- john ni kama njia ya kuwaanzi wachezaji wa wili omary na john ambao walipenda kucheza katika utaratibu huo wa kuanza kete zote za mwanzo na kuzipa majina niliyotaja hapo juu.
- Katika mchezo unaoitwa tege . Kuna sheria imesema watacheza tege 4. kwanini wamesema tege na siyo meja , nugza au pasati ?
ni hivi tege ni mchezo unaotaka mchezaji aanze kete ambayo wachezaji wengi wanaamini ni kete dhaifu kama utaanza na kupelekea ufungwe kirahisi na mpinzani wako. Sasa kwasababu wengi wanajua hii itapelekea sare ziwe nyingi na kupelekea mashindano yawe marefu , hivyo kwa kupendekeza wacheze tege basi tunaweza kuokoa muda kwa kuepusha sare zisiwe nyingi.
Daah..ilinipa muda sana kuja kulizoea hili draft la kwenda mbele tu.Sasa hilo ndio tunacheza sana Kanda ya ziwa .... Hayo madraft yenu mtu anapita nyuma yako kizembe SI tunakula kichwa ....inabidi uzame sana laboratory kupata majibu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti mtu anakatuza nyuma yako na huwezi mfanya kitu daah....
Drafti ambalo king haimuvu kufuata kete iliyoko mbali haina tofauti na kibogoyo a aepambana kutafuna muhogo mbichi. Kunakuwa hakuna maana ya king sasaWapo sahihi , tanzania tuna aina yetu ya mchezo ambayo inaitwa Tanzania draughts (sijui kama nimeandika vizuri ) .
-Hapa tunasheria zetu za namna ya kucheza ambazo kimsingi kwa namna fulani zinafanana na draughts za nchi nyingine kama vile American draughts /british draughts. Ila sasa sifa pekee ya Tanzania draughts ni kuwa king can make very long jumps, and can move back and forth . Wakatika american draughts /british draughts yenyewe inafanana kila kitu katika uanzaji wake na Tanzanian draughts lakini yenyewe king haiwezi kumake long jumps . Na kupelekea vitu kama force king kutokuwepo kirahisi ( wacheza wa draft wananielewa hapa nini nasema kama utacheza draft afu force king ziwe hazipo )
- sasa kwa upande wangu mimi nawapongeza sana waliondaa haya mashindano maana siyo tu wanaupromote huu mchezo wa draft Tanzania bali wanapromote kitu cha nyumbani ambacho dunia inatambua kuwa kwa sheria hizi na hizi zinachezwa Tanzania tu . Tofauti na french style of playing , ambayo kama tungeanzisha mashindano yake tunge promote kitu cha kigeni na siyo cha nyumbani.
Wacheze French Ili washiriki tuwe wengi ?Sasa hilo ndio tunacheza sana Kanda ya ziwa .... Hayo madraft yenu mtu anapita nyuma yako kizembe SI tunakula kichwa ....inabidi uzame sana laboratory kupata majibu 🤣🤣🤣🤣 eti mtu anakatuza nyuma yako na huwezi mfanya kitu daah....
Ko french siyo draft?Hawana rekodi yoyote ya kidraft ,hao wengi wanacheza French