Kwa muda sasa nimekuwa nikisoma baadhi ya post za baadhi ya watu na ushauri wanaoutoa kwa watu wqlio wahitaji wa incubator au bidhaa zingine.
Jf ni mahali ambapo siku zilizopita tulikuwa tunategemea kupata ufumbuzi au msaada wa baadhi ya mambo ambayo huelewi utapata wapi majibu yake.
Kwa ufupi mimi ndiye mwanzilishi wa kampuni ya MWAKALINGA GENERAL ENTERPRISES,iliyopo mburahati mkoani Dar es salaam.
Kampuni yangu ilianzishwa mwaka 2008,mkoani njombe,kisha kufungua ofisi mtwara 2010,na Dar es salaam,2013.
Kampuni inajishughulisha na kazi zaidi ya 20 za ufundi na ubunifu wa bidhaa rafiki wa mazingira na mwanadamu.
Kutokana na tatizo la umeme ktk nchi yetu,tulibuni incubator rahisi sana ya mafuta ya taa.
Ktk incubator hii,ubageuza mayai kwa mkono kila baada ya masaa nane,unaiwasha saa nne usiku,au saa kumi na mbili asubuhi,au saa nane mchana,ili kurahisisha muda wa ugeuzaji mayai.
Incubator hii hutumia mafuta kati ya lita nne mpaka lita nane kwa siku 21,inategemea ukubwa wa incubator kwani kuna zinazobeba mayai 60-200.
Pia inaruhusiwa kugeuza mayai kwenye incubator hii mara mbili kwa siku,endapo tu huwezi kugeuza ktk masaa nane.
Incubator hii ni rafiki wa mjasiliamali,kwani kazi yake kubwa ni kugeuza mayai,kuongeza maji na mafuta ya taa na usafi.Ikifika siku ya 19,Hugeuzi mayai,hayo kama ni mayai ya kuku.
Tumeunda incubator hii kwa ustadi mkubwa,na bado tunaendelea kuziboresha.
Pia tumeunda incubator ya mafuta ya taa,semi automatic,ambayo inatumia mafuta ya taa ktk kutengeneza joto,lakini inageuza yenyewe kila baada ya masaa manne.Huu ni ubunifu wa pekee ambao hata huwezi kupata incubator hii hata nje ya nchi,labda kwa vishoka wanao kopi na kupesti,lakini hata hivyo tunawatahadharisha kuwa mashine zetu zote tunazounda zina hati miliki,hivyo atakaeiga,atakuwa anatenda kosa kisheria.
Kuna mtu alipost hapa jf kuwa incubator za mafuta ya taa huwezi hata kusafiri,huo ni uongo kabisa tena anawakatisha tamaa wajasiliamali.
Mtu unatakiwa kutoa ushauri mzuri,sio kuwatisha watu eti huwezi hata kusafiri au kufanya kazi nyingine,utakuwa unalala kwenye incubator,nilishangaa sana kwa uongo huo.Nilijiuliza,sasa kufanya kazi za kwa wahindi ambazo hupumziki,na kuwa na incubator unayokuwa free masaa 12 ipi bora?
0784413039.