Muda uliosimama mpira wewe unaupimaje?
Ulikuwa una stopwatch pembeni pale mpira ambapo unakuwa umesimama wewe huko kwako ukawa unai stop?
Hukuona matukio ya balls boys kuacha kurusha mipira ndani ili kuchelewesha muda?
Hukuona matukio ya Kocha wa Simba akiokota mipira na kuwapa Mashujaa warushe na wao wakiwa wanajivuta kwenda kupokea mpira kwake?
Hukuona mpaka Kocha akajikuta anakasirika na kuanza kuwafokea hao wachezaji wa Mashujaa kwa ushamba waliokuwa wanamfanyia?
Hukuona kuna time hadi wachezaji wa Simba iliwabidi waende kuokota mipira wenyewe kuwapa Mashujaa ili kuokoa muda?
Hukuona mipira ya kurushwa kuelekea Simba kulikuwa na ucheleweshwaji wa kimakusudi wa muda?
Sometimes unaona mchezaji wa mashujaa anatoka eneo la mbali kwenda kurusha mpira huku akitembea taratibu na akishaufikia mpira anaunyanyua ishara ya kurusha lakini baadae anauweka chini anakuja mwingine kurusha, halafu huyu anayerusha ni mtu ambaye alikuwa karibu?