Masikini na wachafu wanateseka na kuaibika sana wanapohama makazi

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Masikini atateseka km nje ni mtu wa Show-off,
Mchafu wewe huna pa kuponea, maana hali ya uchumi haihalalishi uchafu hapo sasa lazima uwe na timing ya giza na majiranii.

Maana kwenye kuhama bana! watu sikuhio utaona kama wameongezeka halafu kila yule unahisi anakuangalia.

Ukiwa zako ndani ukiangalia vyombo vyako unaona mbona viko poa tuuu, jarb kuhama uonee, kila ukiviangalia pale nje unaona kama ni stoo ya nje,

Hujawahi ona Uchafu kwenye godoro, siku hio litoe uone, unakutana na bonge ya Map na visiwa vya kutosha, hujakaa sawa limepigwa na jua hutojua mende katokea wapiii......

Aaaaah ikifika hapo ndio unavikana unajisemea kimoyomoyo hivi siongozani navyoo ng'ooo, Mnagawana njia na mbebaji.

Godoro ndio mtihani mkubwa kuliko yotee, inafika hatua unalazimisha godogo liingie kwenye Safleti.
 
Ili usijulikane Unaweza umuambie dereva wa sijui kirikuu/guta "Na mimi niwekeni kwenye jaba"

wengi hawapandagi kwenye hio gari, anapanda kwenye boda, tena akiona inamkaribia anaikimbiaa.
Au yupo ndani hathubutu kuangalia nje.

Huku nyuma nako baba wa nyumba unawaza akiona matundu ya misumali kila sehemu na ukungu wa jiko ukutani, unaweza ughaili

Unafika uendako nako kuna visista duu vimekaa nje, unaweza umuambie dereva rudi reverse twende sheli.
Siku hio hata panya hawaogopi, unashagaa Panya wanadandiana juu ya kirikuu..

Unahama, ukifika kwako unajisemea alhamdulillah.
 
Samahani mkuu, kwani umasikini na uchafu vinaingiliana vipi?

Au lengo lako lilikuwa kukashifu watu?

Sijajua kipimo ulichotumia kuthibitisha kuwa umasikini na uchafu vinashabihiana.

Hao matajiri unaowasifu au kuwaona leo, kumbuka nao walikuwa maskini.

Halafu jifunze kumind your own damn business, huo muda wa kufatilia mambo ya watu nao ni uchafu
 
Halafu tambua usafi unahusisha vipengele vingi kijana.
Kumbuka Kuna usafi wa roho,mwili,kiakiii.

Unaeza kuta jitu Kama wewe ni Safi kimwili ila ndani ya moyo limejaza chuki nzito Kama kinyesi.
 
Au wewe uingie kwenye Saflet! This is JF😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…