Masikini na wachafu wanateseka na kuaibika sana wanapohama makazi

Masikini na wachafu wanateseka na kuaibika sana wanapohama makazi

Samahani mkuu, kwani umasikini na uchafu vinaingiliana vipi?

Au lengo lako lilikuwa kukashifu watu?

Sijajua kipimo ulichotumia kuthibitisha kuwa umasikini na uchafu vinashabihiana.

Hao matajiri unaowasifu au kuwaona leo, kumbuka nao walikuwa maskini.

Halafu jifunze kumind your own damn business, huo muda wa kufatilia mambo ya watu nao ni uchafu
Kuna uhusiano kati ya uvivu,uchafu na umasikini
 
Tutafika, lakini kumbuka kuna mtu anapanga chumba kimoja uswahili, kumudu hii unayosema ni ngumu sana,

Na ndio wanahama usiku, maana vitu vimechoka na ni vichafu,

Wengine wanakaa vyumba vya giza, yaani hakuna umeme, anaona vitu vyake vipo poa tu,
Siku akivitoa uwanjani kwenye mwanga, lazima avikimbie, nawapa pole wenye virikuu wanaovibebe,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Ni kwamba nchi yetu haina mipangilio; ni rahisi sana kwa mtu mwenye kipato badala ya kupangishwa na mtu akachukua mortgage bank (badala ya kulipa mwenye nyumba analipa benki siku ya siku nyumba inakuwa yake) kwa wale wasio na uwezo wa hayo kunakuwa na flats za watu masikini ambapo na bei inakuwa ya chini sana... (ingawa tulikuwa na national housing kwa ajili ya hilo jambo ingawa sasa imegeuka kuwa ya wenye pesa na sio watu wa kawaida)

Kuhusu vitu hio ni mentality Africa tunathamini sana vitu (sentimentality) ila tunapoelekea hata makochi ni fashion unabadilisha kila mwaka na nyumba nyingi zikiwa furnished hata unapohama kuna vitu itafika wakati labda kuama na vyombo vya kupikia vichache alivyokuachia bibi yako kama kumbukukumbu vingine utavikuta unapoamia.... Na uzuri wa kuwa na mortgage na nyumba kuwa liquid unaweza kuamua kuhama time yoyote kwenda sehemu yoyote na kuuza hii kununua ile wakati wowote (ukizingatia kukiwa na mipangilio hata nyumba nyingi zitakuwa saresare kila mtaa (unless wewe ni Don na serikali inakupiga Tozo ya kufa mtu
 
Samahani mkuu, kwani umasikini na uchafu vinaingiliana vipi?

Au lengo lako lilikuwa kukashifu watu?

Sijajua kipimo ulichotumia kuthibitisha kuwa umasikini na uchafu vinashabihiana.

Hao matajiri unaowasifu au kuwaona leo, kumbuka nao walikuwa maskini.

Halafu jifunze kumind your own damn business, huo muda wa kufatilia mambo ya watu nao ni uchafu

Halafu tambua usafi unahusisha vipengele vingi kijana.
Kumbuka Kuna usafi wa roho,mwili,kiakiii.

Unaeza kuta jitu Kama wewe ni Safi kimwili ila ndani ya moyo limejaza chuki nzito Kama kinyesi.
🤣🤣🤣Duuu we jamaaa umekua mkali sana kwenye huu uzii...

Humu unaweza ugombane mpk na masufuria hapo ulipo ukihisi kila kitu unasemwa wewe..
Relaaaax brother...
 
Nmecheka sana nikakumbuka mwaka jana jirani yangu alikua anahama mchana ,basi bwana wale wanaomuhamisha kwa guta wakawa wana nsaidie kutoa vitu nje, walipotoa godoro mara mmoja wa wale vijana akarudi kinyumenyume huku macho yanemtok akaanza kupiga kelele mtu!,mtu!.Akaja mwenye vitu vyake akauliza nini yule jamaa akajibu kuna mtu kwenye godoro ,yule mama akaingiza mkono kwenye godoro (lilikua limekunjwa) huku anasema sio mtu ni wigi hili ,akalitoa,, aisee jamaa waliishia kucheka tu
 
Mkuu hii imekaaje?
Yani urogwe kisa kuhama/mali au nini hii hoja sijaielewaa...
Yaani maisha ya ushwahilini kama upo vizuri kiuchumi ukihama mchana watu wanaona TV fridge kitanda kizuri makochi safi lazima wakupige zongo

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Kuhama nyumba halijawahi kua jambo rahisii, hasa kama wewe ni mchafu unaweza ukimbie vyombo vyako.

Maskini si shida sana labda km ni mtu wa show-off atajihisi aibu, ila mwingne km maisha yake anayaweka level basi sio shida hasa kama ni msafi, inshu uwe mchafu.

Uwe tajiri au masikini kama ni mchafu hapo kazi unayo, hali ya kiuchumi haiwezi halalisha uchafu,
Wengi wanahama usiku kufunika kombe.

Kwenye kuhama bana! watu macho yanakua juu juu sanaa, tension inaongezekaa kwa unaowapita ×2

Ukiwa zako ndani ukiangalia vyombo vyako unaona mbona viko poa tuuu, jarb kuhama uonee, kila ukiviangalia pale nje unaona kama ni stoo ya nje,

Hujawahi ona Uchafu kwenye godoro, siku hio litoe uone, unakutana na bonge ya Map na visiwa vya kutosha, hujakaa sawa limepigwa na jua hutojua mende katokea wapiii......

Aaaaah ikifika hapo ndio unavikana unajisemea kimoyomoyo hivi siongozani navyoo ng'ooo, Mnagawana njia na mbebaji.

Godoro ndio mtihani mkubwa kuliko yotee, inafika hatua unalazimisha godogo liingie kwenye Safleti.
Umewaza nini wewe hasa ... hatareeee.
 
Hahahaha watu huwa wanasingizia oooh ukihama mchana wezi watakuchora wakat godoro alinunua Babu mpaka mjuu analitumia wataiba Nini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ukiishi msisha yako bla kufuatilia wengne watasema nn juu yako ata kama ni maskini na mchafu wala hautawaza .
 
Ili usijulikane Unaweza umuambie dereva wa sijui kirikuu/guta "Na mimi niwekeni kwenye jaba"

wengi hawapandagi kwenye hio gari, anapanda kwenye boda, tena akiona inamkaribia anaikimbiaa.
Au yupo ndani hathubutu kuangalia nje.

Huku nyuma nako baba wa nyumba unawaza akiona matundu ya misumali kila sehemu na ukungu wa jiko ukutani, unaweza ughaili.

Siku hio hata panya hawaogopi, unashagaa Panya wanadandiana juu ya kirikuu..
We jamaa,hebu nipe break...hahahaa!
 
😂😂😂Mtatuvunja mbavu
 
Kuhama nyumba halijawahi kua jambo rahisii, hasa kama wewe ni mchafu unaweza ukimbie vyombo vyako.

Umaskini km ni msafi si shida labda km ni mtu wa show-off atajihisi aibu, inshu ni uwe mchafu, hapo lazima uwe na timing ya giza na majiranii.

Maana kwenye kuhama bana! watu sikuhio utaona kama wameongezeka halafu kila yule unahisi anakuangalia.

Ukiwa zako ndani ukiangalia vyombo vyako unaona mbona viko poa tuuu, jarb kuhama uonee, kila ukiviangalia pale nje unaona kama ni stoo ya nje,

Hujawahi ona Uchafu kwenye godoro, siku hio litoe uone, unakutana na bonge ya Map na visiwa vya kutosha, hujakaa sawa limepigwa na jua hutojua mende katokea wapiii......

Aaaaah ikifika hapo ndio unavikana unajisemea kimoyomoyo hivi siongozani navyoo ng'ooo, Mnagawana njia na mbebaji.

Godoro ndio mtihani mkubwa kuliko yotee, inafika hatua unalazimisha godogo liingie kwenye Safleti.
🤣🤣🤣🤣 Nmecheka hadi so poa.
Yalaaaaaaaaah
 
Eti kirikuu ikiikaribia boda anakimbia 😆 😆 😆 😆
Hapo unakuelekeza mwenye kirikuu mtaa unaohamia unamwambia akifika ashushe aulize chumba aingize ndani utaenda unamaliza kuwaaga wapangaji wenzio😂😂
 
Uzuri wanahamia walipojenga, wewe endelea kulala nyumba za watu.
 
Back
Top Bottom