Sikubaliani na mengi uliyoandika ila honey trap inatumika sana marekani kuwatapeli /kuwadhulumu watu matajiri au waliojipata kimaisha fuatilia case ya TYRES GIBSON yeye alimpenda msichana wakafunga na ndoa kumbe msichana alikuwa na boyfriend wake pia na anampenda kweli kweli so wakakubaliana msichana ataishi na tyres kwa muda fulani kisha atadai talaka ili apate 50% maana tyres ni muigizaji maarufu marekani na ana uwezo pia wa kifedha .
Tyres kosa alilofanya ni kutomsainisha huyo mke wake prenuptial agreement kwa kuamini hakuwa mtu maarufu so asingekuwa na tamaa , kosa! Kesi ikaenda mahakamani na hakimu akaamuru mali zigawanywe mwanamke akaondoka na jumba lenye thamani ya 1M $ na kila mwezi jamaa akaambiwa atakuwa anampatia 10690$ kwa malezi ya mtoto.
Mwanamke alipoulizwa kwanini alifanya maamuzi hayo wala hakuficha ndo akatoa stori (kwa ufupi na ak i twist) kwamba tyres alimlazimisha amuoe na akijua kabisa ana mchumba wake , akaulizwa pia utajiiri alioupata (nyumba ya kifahari , pesa na pesa za kila mwezi ) atazitumia vipi? Jibu ni kwamba atamrudia mchumba wake kwa sababu ndo mwanaume anampenda kwa dhati na wataponda raha kwenye jumba hilo SO SAD.