Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla

Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla


Abdul Juma ‘Baba D’


Erick Evarist na Gladness mallya

DAR ES SALAAM: Maskini wee! Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma ‘Baba D’ anaumwa sana! Ndivyo Risasi Mchanganyiko linavyoweza kukuhabarisha baada ya mzazi huyo kuzidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini kutibiwa kwa msaada kutokana na kukosa fedha, twende hatua kwa hatua.

NI JUMAPILI ILIYOPITA


Tukio hilo la kusikitisha la baba mzazi wa msanii ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha Bongo, lilijiri Jumapili iliyopita ambapo kwa msaada wa Dk. Fadhili Emily wa Kituo cha Tiba cha Fadhaget Sanitarium kilichopo Mbezi Beach-Africana, Dar, baba Diamond alifikishwa kutoka nyumbani kwake Magomeni-Kagera hadi hospitalini hapo na kupatiwa matibabu.



….Akiwa mapokezi.


CHANZO CHAVUJISHA

Awali, Risasi Mchanganyiko lilipokea taarifa za mzee Abdul kuzidiwa nyumbani kwake lakini ikaelezwa kwamba, hakuwa na msaada wowote hadi majirani walipopata mawasiliano ya daktari huyo na kumuomba amsaidie.

“Jamani baba D (baba Diamond) yupo hoi hapa nyumbani kwake Magomeni. Miguu inamuuma, anashindwa kutembea na ukizingatia hana kipato, anashindwa pia kwenda hospitali. Na bahati mbaya kwa muda mrefu hata majirani wamekuwa wakimsaidia lakini bado hajapata tiba sahihi.”

AUNGANISHWA NA DK. FADHILI

“Leo (Jumapili) kuna jirani yake mmoja hapa ndiyo amepata wazo baada ya kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi (ndugu na hili), amepata namba za Dk. Fadhili katika makala anazoandika gazetini kuhusu afya. Akampigia na kumuomba msaada na bahati nzuri dokta huyo ameguswa na tatizo la mzazi huyu, amemtumia nauli ya teksi ili akimbizwe hospitalini kwake, sasa hivi ndiyo wanaelekea huko,” kilisema chanzo hicho.

MAKACHERO WAUNGA TELA

Licha ya kuwa muda huo ulikuwa umeyoyoma (saa 1 usiku), makachero wetu waliingia mzigoni kuelekea moja kwa moja Mbezi kwenye hospitali hiyo na kumkuta baba D akiwa anaingia mapokezi katika kliniki hiyo.



ASAIDIWA NA WAHUDUMU

Akiwa mapokezi, makachero wetu walimshuhudia baba Diamond akisaidiwa na vijana wawili ambao ni wahudumu wa hospitali hiyo, walimkalisha kwenye kochi kisha wakaanza kumpa huduma ya dharura ambapo walimpima presha na kumuita Dk. Fadhili atazame miguu yake.

KUHUSU MIGUU

Dk. Fadhili alipofika, alimvua soksi baba huyo na kuikagua vizuri miguu hiyo kabla ya kuingia naye ndani katika chumba maalumu cha vipimo na matibabu.



VIPIMO VINGINE

Ilibainika kuwa, miongoni mwa vipimo alivyopimwa baba D ni pamoja na kile cha Quantum Magnetic Analyzer ‘QMA’ ambacho kazi yake ni kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu. Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko halikufanikiwa kujua kipimo hicho kilitambua nini!

BABA DIAMOND AFUNGUKA

Baada ya kupimwa na kupatiwa dawa za kutumia, baba Diamond aliliambia gazeti hili kuwa, anamshukuru daktari huyo kwani ameweza kugundua tatizo linalomsumbua na kwamba anaamini dawa alizopewa zitamsaidia.

“Kwa kweli ni Mungu tu, hali yangu ni mbaya, miguu inanisumbua kwa zaidi ya miaka nane sasa. Inauma, imevimba na inabadilika rangi kuwa myeupe. Inakuwa kama inatoka mabakamabaka. Kiuchumi siko vizuri kabisa.”



NGOZI IMEATHIRIKA

“Dk. Fadhili amenipima, amebaini ngozi yangu imeathirika vibaya. Amenitajia tatizo langu kitaalamu na amenipa dawa za kutumia, lakini pia amenielekeza mazoezi maalum ambayo natakiwa kuyafanya,” alisema baba Diamond huku uso wake ukijaa simanzi.



Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond.


AMWAGA SHUKRANI

Baba Diamond alipoulizwa kama alimueleza mwanaye Diamond kuhusu suala hilo wakati alipozidiwa, alisema hakuona na haoni sababu ya kumwambia kwani analijua na hapendi kuendeleza malumbano na mwanaye lakini anamshukuru Dk. Fadhili kwa kujitolea kumsaidia bila malipo yoyote.



“Sipendi kuendeleza malumbano, ninachokiangalia kwa sasa ni miguu yangu. Nitamshukuru Mungu zaidi nitakapopona kabisa maana nimeshahangaika nayo sana. Kipekee, kutoka moyoni nimshukuru Dk. Fadhili kwa kusikia kilio changu na kunisaidia bure.

“Sikutegemea, mtu unaumwa, anakwambia anakutumia fedha ya teksi uende hospitalini kwake akakutibu bure. Ni upendo wa hali ya juu na Mungu amzidishie, pale alipotoa apabariki na apate zaidi,” alisema baba Diamond.

Diamond

DIAMOND ANASEMAJE?

Gazeti hili lilifanya jitihada za kutaka kumsikia Diamond anazungumziaje suala hilo la ugonjwa hadi kufikia mzazi wake kusaidiwa na mtu baki, simu yake haikuwa hewani lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp ulioonesha ameusoma, bado hakujibu chochote.



TUMEFIKAJE HAPA?

Baba Diamond amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa miguu ambapo awali, mzazi huyo alisema anasumbuliwa na kansa ya ngozi lakini hata hivyo, mwanaye Diamond amekuwa mzito kumsaidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mwanaume huyo kumtelekeza mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yeye akiwa mdogo.

MAJIBU YA DK. FADHILI

Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu daktari huyo na kumuuliza kuhusu tatizo la baba Dimaond na namna alivyolishughulikia, ambapo alijibu:

“Ha! Jamani, ugonjwa wa mtu ni siri kati yake na daktari, labda kama ataona sawa aseme yeye mwenyewe.”

chanzo.Maskini Baba Diamond, Azidiwa ghafla!



Si alimkana Diamond kuwa sio mwanawe tangu akiwa mdogo? sitaelewa unataka kumaanisha nini kwa kweli. baba aliambiwa mtoto wake akasema sio wake akasepa. Mama amebaki na mtoto wake labda mtoto aliishia mikononi mwa baba mwingine. sioni sababu ya kumuhitaji Diamond kwa sasa au kulaumiwa Diamond au kutafutwa, huyu mzee ni mtu mstaharabu sana hataki shida.
 
Watoto msipende kuwasikiliza sana mama zenu hamuwezi jua nini kiliwatenganisha.....ni bora tu mondi ajitoe ufahamu amsaidie alafu huyu mzee malipo yake yawe kwa mungu.mwenyewe kwani yeye ndiye anayejua
Mwangalieni kanumba Naye alikuwa na kisasi kama mondi tu
LAKINI hata yeye alikufa na akamwacha baba yake na kinyongo chake moyoni...jiulizeniiii
Nimeipenda sana hii,ni ukweli usio pingika wanawake mara nyingi wana influence kubwa sana kwa watoto (power of a woman),kitu kinachowafanya hata kuwachukia baba zao bila ya kujua ukweli wa tatizo.Najua kuna watakao pingana na mimi kwa kuwa malezi yao sio ya kuunga unga kama ya kina sie ambao tume experience hivi vitu kakatika makuzi yetu.
 
Hata kama mzazi alikutesa kwa namna gani hupaswi kulipiza ubaya kwa ubaya pia ukumbuke Hugo ndiye alikuleta duniani,ni heli ya Hugo diamond akamsaidia baba yake japo Paso na kuonana nae lkn mzee akajua msaada umetoka kwa mwanangu lkn anachokifanya hakipaswi kushabikiwa Leo huyo mzee ktk uhai wake ataona sasa lkn kesho ktk mauti yake yeye(mtoto)atakapokuja kukumbuka ayafanyayo Leo atatamani mzee Huyo aamke japo nusu SAA amsaidie na amshukuru japo apate radhi zake naamini c jambo jema uende kwenye hbdy umwage fedha na bado wanaadam wengine wakiteseka akiwepo mzazi wako hii ni dunia starehe chache ndio zinatupumbaza tufikie hapa,M/Mungu ni kwenye kujua zaidi.

Sijaelewa unachoeleza hapa. Baba alisema mtoto sio wake na akaondoka kabisa. Ina maana huyo diamond sio mtoto wa huyo baba. Diamond hatajutia nini wakati huyo sio baba yake na huyo mzee alisema sio mwanawe.
 
Nimeipenda sana hii,ni ukweli usio pingika wanawake mara nyingi wana influence kubwa sana kwa watoto (power of a woman),kitu kinachowafanya hata kuwachukia baba zao bila ya kujua ukweli wa tatizo.Najua kuna watakao pingana na mimi kwa kuwa malezi yao sio ya kuunga unga kama ya kina sie ambao tume experience hivi vitu kakatika makuzi yetu.
Kama unatambua kuwa ni mwanao na umekosana na mama weka utaratibu wa kulea mtoto. Mtoto unayetelekeza sijui anakuwa na kosa pia? Kama mama ni tatizo inakuwaje kuacha kulea mtoto au unakuwa ni mkwepa majukumu?.
 
Mzee arudi nyuma akumbuke alichokifanya kuwa haya ndiyo mavuno,picha zinaonyesha kuwa hazikupigwa kikachero bali ni dhamira kwakuwa waliopo kwenye picha wote wamejiandaa kuangalia camera.
Aendelee kula ujana wake mbovu,na iwe fundisho kwa VIJANA UCHWARA,mabingwa wa kukataa mimba huku wakiwa mafundi kwenye "KUSIMAMIA"
 
Kama unatambua kuwa ni mwanao na umekosana na mama weka utaratibu wa kulea mtoto. Mtoto unayetelekeza sijui anakuwa na kosa pia? Kama mama ni tatizo inakuwaje kuacha kulea mtoto au unakuwa ni mkwepa majukumu?.
Najua ni ngumu sana kuelewa hii kitu,kweli wapo wanaofanya makosa kwenye maamuzi ya jinsi ya kumlea mtoto,lakini ninachotaka pia ufahamu ni kuwa utamu au ladha ya kuwa na mtoto huwezi kuujua kama huna mtoto,na inapofikia mpaka baba anaamua kuacha kuhudumia mtoto kwa sababu nyingine tu ukiondoa kuwa labda kabanwa na nyumba ndogo and the like ujuwe kuna zaidi ya hayo yanayosemwa na watu ambao hawajui kiundani.
 
Sijaelewa unachoeleza hapa. Baba alisema mtoto sio wake na akaondoka kabisa. Ina maana huyo diamond sio mtoto wa huyo baba. Diamond hatajutia nini wakati huyo sio baba yake na huyo mzee alisema sio mwanawe.
Baba D nae aache kulia lia. Je D aisngekuwa nazo hataishi? Aishi kiume as if mwanae hana kitu. Akiamua kumsaidia ni kwa ridhaa yake na sio lazima. Tunawajibika kuwaendeleza watoto wajitegemee na siyo watutegemeze.
 
Diamond anakosea sana. Yaani anahangaika na Zari halafu anamuacha babake anateseka
sidhani kama unajua unachokiongea. Diamond alishawahi kueleza hadi kutoa machozi maisha yake ya mateso utotoni wakati baba yake akila bata na mke mwingine na hakuwahi kumsaidia, zaidi ya kumfukuza. mwache huyu mzee avune alichopanda. ndio dawa ya wazee wenye kukataa damu zao
 
sidhani kama unajua unachokiongea. Diamond alishawahi kueleza hadi kutoa machozi maisha yake ya mateso utotoni wakati baba yake akila bata na mke mwingine na hakuwahi kumsaidia, zaidi ya kumfukuza. mwache huyu mzee avune alichopanda. ndio dawa ya wazee wenye kukataa damu zao
Lazima tujifunze kuwa na roho ya kusamehe. Hayo mambo yalitokea kipindi cha nyuma na hatuwezi kujua ni nini chanzo chake. Diamond anapaswa kuelewa kuwa duniani kuna baba mmoja na mama mmoja tu.
 
Kama Mungu tunamkosea anatusamehe 7*70 naye ndiye aliyetuumba. Inakuwaje huyu Mondi kuona kosa alilofanya baba yake ni kubwa kiasi kwamba hawezi kumsamehe? Kama mtoto alipaswa kutambua hawezi pata baba mwingine zaidi ya huyo. Na asisubiri afe ndo aende kwenye msiba kwa mbwembwe. Namkubali Mondi ila kwa hili hapana.

Ameridhika na mama yake aliyepigana kufa na kupona kuona maisha ya mwanae yanafanikiwa wakati baba ambaye hakumtambua kipindi hicho akila bata na mke mwingine. acha aonje joto ya jiwe, ndio dawa ya mababa suruali.
 
Lazima tujifunze kuwa na roho ya kusamehe. Hayo mambo yalitokea kipindi cha nyuma na hatuwezi kujua ni nini chanzo chake. Diamond anapaswa kuelewa kuwa duniani kuna baba mmoja na mama mmoja tu.

mama yake ali play part zote mbili na maisha yalienda wakati huyo baba anaishi maisha mazuri. sidhani kama ulisikiliza kipindi cha Diamond maisha aliyoishi na alivyofukuzwa na huyu anayejiita baba wakati alienda kuomba pesa za kaptula ya shule ambayo ilikua imekwisha, ilhali uwezo alikua nao.
achene Diamond ale bata na mama yake ambae hakuwahi kumtupa hata siku moja katika shida zote walizopitia.
 
Dedication kwa wababa wote mnaokimbia wtt,wakifanikiwa mnakuja kifua mbele mkome mnatakiwa mtulie km kipindi kile cha kulea,my dady is one of them cmchukiii na nimemsahame,ila moyoni mwangu hayupo kama mm nicvyokua moyoni .wake
 
mama yake ali play part zote mbili na maisha yalienda wakati huyo baba anaishi maisha mazuri. sidhani kama ulisikiliza kipindi cha Diamond maisha aliyoishi na alivyofukuzwa na huyu anayejiita baba wakati alienda kuomba pesa za kaptula ya shule ambayo ilikua imekwisha, ilhali uwezo alikua nao.
achene Diamond ale bata na mama yake ambae hakuwahi kumtupa hata siku moja katika shida zote walizopitia.
Baba ni baba
 
tumwache Diamond na maisha yake. ni mtu mzima. yaliyo nyuma ya pazia hatuyajui. wababa ndio mpate fundisho hapa, tabia za kukataa watoto wakiwa wadogo muache maana hujui baadae atakua nani na wewe utakua nani. sio muanze kulia lia na waandishi wa habari utadhani una act movie, kisa umetelekezwa, wakati mtoto alipokuhitaji hukuwepo.
 
Back
Top Bottom