Maskini Pacome. Kweli kuimba kupokezana. "Kama Simba hawataki Kuguswa wakacheze karata" Pacome leo kaguswa

Sisi waafrika hatuendelei kwa mambo ya kipuuzi kama haya. Sasa kumuumiza hivyo mwenzako kazini unapata faida gani?
Nimeangalia ile tackling kwa makini,yule beki hakuwa na mpango na Mpira kabisaaaa!
 
Ninachojua mimi hawa wanalogana sana...
Tizama walichomfanya Mzize...
Kamekua kama katoto kadogo
 
watu ni either hamjui mpira au mmeweka mahaba ya timu mbele

Hiyo foul ukisema jamaa amekusudia kumuumiza pacome utakuwa mwongo kwa sababu it's clearly alikuwa anataka kucheza mpira or kufanya tackling block ambayo bahati mbaya imekutana na mguu wa pacome ukiwa kwenye movement
Uko sahihi sana,foul ilikua ya kawaida lakini ndio hivyo mazingira ya pacome kuwa kwenye. Movement ndio ikawa changamoto,hata asingepigwa mguuni bado pacome aliangukia goti vibaya sana!
 
Uongo!
 
Hatocheza tena mpirq, labda akacheze dhumna au draft
Hivi wale wanaounga mifupa kienyeji kwanini wanachukuliwa poa poa sana wakati naona kama wana tiba ya uhakika na huchukua muda mfupi kupona. Kuna ndugu yangu aliangukiwa na ngema ya mchanga wakati anachimba mchanga uliopo juu, mguu mmoja ulikatika sehemu mbili lakini leo huyo anaendelea na shughuli zake.
 
Pacome kupona atapona tu. Lakini kumbuka kuwa wachezaji wengi wa Afrika umri uliopo kwenye paspoti ya kusafiria unaongeza tena miaka mitatu mpaka mitano kuupata umri halisi wa mchezaji. Kwa hiyo kurudi tena uwanjani kwa haraka halafu tena kwa kiwango kile kile sio rahisi sana. Na mifano ipo hapa hapa bongo kama Fraga na hata Mzize.

Na kibaya zaidi huyo Pacome alishafika kilele cha ubora wake na alishaanza kushuka kiwango taratibu. Kwa hiyo hata kama asigekutana na dhahama ya hiyo rafu kwa mtizamo wangu Pacome msimu ujao ndio ungekuwa wa mwisho kucheza Yanga. Sasa hili balaa lililomkuta ndio itakuwa mbaya sana kwake labda tu Mingu aingilie kati vinginevyo ile spidi yake huku anawahesabu mabeki wa timu pinzani kila week end tutavimisi sana.

Kikubwa mashabiki wa Simba na Yanga nao waache kushabikia rafu za kijinga hasa pale anapochezewa mchezaji wa timu pinzani na ya kwake kwani ndio inasababisha hao wachezaji wapuuzi kuumiza wenzao. Ni wakati sasa wa kuwazomea na kuwapiga vita hao wachezaji wanaocheza rafu mbaya uwanjani badala ya kuwasifia wanapoumiza wachezaji wa timu pinzani.

Kuna yule mchezaji anacheza rafu mbaya sana wenyewe wanamuita mvunja kuni kama sikosei jina lake halisi ni Albano Mtenje bado yupo ligi kuu kweli sijamsikia siku nyingi. Huyo jamaa alikuwa anaona sifa kabisa kusifiwa kucheza rafu za kijinga. Wachezaji kama hao wanahitaji watafutiwe watu wa kuwashauri waache hiyo michezo yao maana watakuwa wanawaharibia wenzao maisha.

Mchezaji mwingine mvunja kuni alikuwa huyo Kagoma wa Simba. Aisee aliyembadilisha akaacha kucheza rafu za kijinga apewe maua yake. Sasa hivi Kagoma amekomaa kiakili kiasi anakwenda kuchukua mali bila kufanya rafu za kijinga kama zamani wakati siyo kawaida yake.

Ni mtizamo tu
 
Naongezea kidogo. Ikumbukwe kuwa Yanga ni Klabu inayomjali mchezaji ndani ya pitch tu, nje ya uwanja hawana taimu na wewe. Pacome asitegemee kabisa matibabu nje ya Tanzania, anayopitia Clement mzize naye atayapitia, kengele ndiyo imelia hivyo.

Kama amewka akiba basi ajitahidi arudi nyumbani kwao haraka, japo nasikia alikuwa ni mtu wa viwanja sana na kula bata. Umaskini utamtembelea muda si mrefu
 
Kuna matches kadhaa nliona kuna teams zimetumwa kuumiza wachezaji wa Mikia. Zipo wala si suala la kubishana na nlisema tusifurahie. Tusifike huko. Kuna siku itatokea kwetu.

Leo imetokea. Faulo ambayo imempata Pacome. Inaumiza sana. Nahisi huu mguu utakuwa umevunjika. Sijui wataalamu watasemaje. Last week kuna wachezaji walikuwa wanawachezea fouls mbaya sana Mikia.

Nliuliza nikaambiwa ni maandalizi na match ya Azam. Nliuliza nikaambiwa pia kama Simba wanataka wasiguswe wakacheze Karata. Leo yamekuja upande wetu. Kama hili tukio ni kweli si chini ya miezi Mitatu Pacome atakuwa juu ya Mawe.

View attachment 3619125
Hivi huyu mchezaji aliyecheza faulo, ni mzanzibar?
 
Kuna yule Damaro,huwa anagonga rafu sana,ibra bacca nae huwa anachezaga sana rafu kuna wakati mwingine huwa anataka hadi kupiga mtu ngumi,ajabu ni kuwa wadau wa yanga na wachambuzi huwa wanafurahia tu ,leo yamewakuta wanataka kuhurumiwa,
Mechi ya Simba na Singida juzi rafu mbaya wachezaji wamefanyiwa na za makusudi kabisa ila amna chochote wala nn,
Wachezaji walindane wenyewe wakiendelea kusikiliza wanasiasa wa soka kisa ahadi za kipuuzi matokeo yake ndiyo haya
 
Kuna matches kadhaa nliona kuna teams zimetumwa kuumiza wachezaji wa Mikia. Zipo wala si suala la kubishana na nlisema tusifurahie. Tusifike huko. Kuna siku itatokea kwetu.

Leo imetokea. Faulo ambayo imempata Pacome. Inaumiza sana. Nahisi huu mguu utakuwa umevunjika. Sijui wataalamu watasemaje. Last week kuna wachezaji walikuwa wanawachezea fouls mbaya sana Mikia.

Nliuliza nikaambiwa ni maandalizi na match ya Azam. Nliuliza nikaambiwa pia kama Simba wanataka wasiguswe wakacheze Karata. Leo yamekuja upande wetu. Kama hili tukio ni kweli si chini ya miezi Mitatu Pacome atakuwa juu ya Mawe.

View attachment 3619125
Mimi Mchome Mapovu nimefurahi Pacome kuumia
 
Back
Top Bottom