Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Mbona dogo kila akiachia wimbo unakuwa hitsong sasa nashangaa mwenzangu unaposema jamaa hajui kuimba cjui unamanisha nn

Anahitaji kujenga utambulisho wake, sio kila jambo amuige tu diamond. From kuvaa, aina ya mademu anaotoka nao, kuongea hadi kuimba. There is no such thing as an original copycat, ndio essence ya sisi kumuona kua hajui kuimba
 
Anahitaji kujenga utambulisho wake, sio kila jambo amuige tu diamond. From kuvaa, aina ya mademu anaotoka nao, kuongea hadi kuimba. There is no such thing as an original copycat, ndio essence ya sisi kumuona kua hajui kuimba
Waja hamukosi cha kusema......watanzani wanavodhani mtu kujua kuimba abane pua kama kina kiba na kina mavoko basi huyo ndo anaejua kuimba lkn tofaut na apo hujui kuimba
 
Siyo kweli. Wewe jaribu kupunguza chuki na wivu kidogo, kisha sikiliza sauti ya huyu dogo. Dogo anastahili pongezi kwa juhudi zake. Diomond anajua biashara, anajua nini wapenzi wa muziki wanahitaji ndiyomaana dogo yupo pale
kwa hiyo wapenzi wa muziki wanahitaji Wasanii wabakwe na makahaba wa bongo movies?!
Tena mwambie awe na heshima kwa hao wazee aliowataja...

Yaani hii mikelele ya hamonaiz ni muziki??? sasa akina maurice kiria wa Uganda tuuitaje??
kanikera kweli huyu...angekuwa karibu ningemzibua makofi
 
Mijitu inachuki humu afu hawatoi point
 
Hivi mtazamo wa anayejua muziki ndiye nani?!! Kazi za sanaa ni bidhaa kama bidhaa nyingine. Kama mtu anatengeneza bidhaa inayokubalika sokoni na haina madhara, basi hiyo no bidhaa nzuri. Uzuri wa bidhaa unahusu Mambo mengi, kama vile ubora, unafuu wa bei,nk. Hivyo soko ndilo linasema Ipi ni bidhaa nzuri. Dogo anakubalika na Mashabikia, sasa huyo mtaalamu wa muziki ana nafasi gani hapa. Na hata hao anaowakubali yeye mbona wanahaha kupenya kwenye soko bila mafanikio. Master J ni mtaalam wa muziki aina ya HIP Hop siyo aina zote. Hivyo aina nyingine zote yeye si shabiki wake.

Umeandika vyema, wapo waimbaji wazuri sana sana, wanafuata ''note'' na kila msingi wa uimbaji na muziki lakini hawana mashabiki wengi wala kazi zao haziuzwi sana.
Wapo ambao wanaimba imba tu lakini wanakusanya washabiki na wanakubalika, yote haya hayabadilishi ukweli. Huwa nawaza inawezekana uweredi katika hizi sanaa, haziamuliwili na hawa ''wataalamu'' wa sanaa husika bali huamuliwa na ''walaji'' wa bidhaa inayotoka kwa msanii.

Hali hii ipo katika sanaa zote, si kila anayejua sana ndiye huwa anakubalika.
 
Back
Top Bottom