Masudi Kipanya akemewe kabla hajaleta machafuko kama Lars Vilks

Mtoa mada Kipanya kaongelea Sukuma genge (kikundi) na si kabila la wasukuma
Sukuma gang ni lugha inayotumiwa na Chadema na wanasiasa wengine kumaanisha mtu wa kabila la wasukuma. Masudi kawalenga wasukuma.
 
Mwangaluka Mayo, ulimwola?......
 
Acheni kutengeneza utengano wasukuma wangapi wapo chadema mfano angalia kula alizo pata upendo chato zile walipiga wachaga au
 
Tuache kushambulia kabila fulani kwa sababu zozote zile. Ni hatari kuna kuchoka na kujibu mashambulizi.

Limeshambuliwa genge au kabila?. Maana kasema Hakuna Sukuma genge. Inaonekana hujaelewa kilichobaki andikwa.
 
Bongo kwakweli hiyo sio ishu kabisa maana tunataniana mnoo
Hapana huu si utani, huu ni ubaguzi na muendelezo wa mashambulizi kwa wasukuma. Ni wapole ila kuna siku watachoka watajibu.
 
Sukuma Gange sio?
 
Sukuma ndio kabila kubwa, lenye heshima na wapambanaji. Wape pole Chadema na wanasiasa wengine wanaoangaika kuwachafua maana sioni watachofaulu.

Mkabila mkubwa Sana wewe. Unahangaika na CHADEMA ili kuwagombanisha na wasukumuka. Hutafanikiwa na hiyo roho yako mbaya.
 
Sukuma ni kabila. Hakuna tafsiri mpya. Sioni afya ya kushambulia wasukuma. Masudi ameingia mtego mbaya sana.

Amemshambulia msukuma gani kwa kusema Hakuna Sukuma genge?. Wewe ulitaka usikie lipo Sukuma gang ndio hufurahie maana mnautukuza ukabila utadhani Nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…