Maswali 8 ya kuwauliza Bunge la Ulaya

Jua tu, ikiwa kula yako, nyumba unayoishi na pesa ndogo ndogo zinatoka kwa baba/mama mkwe, jua tu huwezi kumpiga mkeo makofi wala kumfokea kizembe zembe.

Ukiona kama taifa unaingiliwa mambo yako jua kuna sehemu mmefeli, hao wenyewe ulaya hawana jeuri ya kumkoromea mmarekani, ila mmarekani anawakoromea wao, umejiuliza kwanini? Tizama mfano wangu wa Kiswahili swahili juu hapo
 
Umenena vyema. Muhimu tukaondoa kwanza kifikra kwamba Afrika haiwezi kujiendesha, pili wanaotumika na hao kuleta uchafuzi washughulikiwe kisheria, tatu, tuwe wasimamizi wa sheria na sheria zitungwe kuilenga jamii ya waafrika yenye lengo la kulinda rasilimali, tamaduni n.k,.
 




Kuliko wanaotukana tu kama manyumbu nawakubari Sana watu ka wewe mze.

Yani ukiwa na hoja toa hoja... Usitukane ili mradi.

Japo natofautiana na msimamo na mtazamo wako Ila nimekukubari sabab hauja jawa na maasira asira na matusi ila unazo hoja.
 
Hivi kukopeshwa si mpaka mkopeshaji akubali?

Nenda wewe leo bamk kakope millioni 100 tu kama unadhani kukopeshwa hakuna conditions zake.
Umenena vyema, je, unajua faida anayopata anayetoa mkopo? Kabla ya kufikiria mkopaji?

Iko hivi, faida kuu na nyingi hujificha katika maslahi ya kisiasa, kiuchumi, na kimkakati, zinazojumuisha, faida ya Riba, Udhibiti wa sera, ushawishi wa Kijeshi au Kiusalama (Geopolitical Influence), fursa kwa makampuni yao, kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wao, na kulinda maslahi yao ya muda mrefu.

Kwa hivyo, kila mmoja ananufaika kwa upande wake na kila mmoja anamhitaji mwingine. Haimaanishi kuwa ukinikopesha sasa uanze kunifundisha namna gani ya kuishi.
 
N
Nilitaka nikuupuuze Ila nimegundua Kuna machawa watarudia huu ujinga
Ñaona ni Aina ile ile ya fikra za kijinga nazozipiga vita

Akili zinazojali tumbo la siku moja ili kufarahisha watu Fulani bila kujali maslahi ya nchi ni hasara kubwa Kwa Taifa letu

Hilo la chadema muulize Mkurugenzi wa uchaguzi maana ni kama hufuatilia habari

Hoja na mbili hadi nane ni hoja moja tu ya mamlaka ya bunge la ulaya ,INGAwa umejaribu kutenganisha Aya zako Kwa namba

Wazazi Wana mamlaka ya asili juu ya watoto wao Ila Wana mipaka , huwezi kuteka kutesa na kuua watoto wako alafu uache kisa uhuru

Haki haina mipaka
Sovernity Ina mipaka yake haswa kwenye Kusimamia haki za msingi za binadamu

Kama mlidhani mtavunja haki za watu kuwatesa kuwateka na kuwaua halafu mnyamaziwe na watu wenye akili timamu
Hilo hapana hata Mungu atakataa

Nilifikiri mtashukuru bunge la ulaya Kusimamia haki kwenye nchi yenu kumbe Nyie mnataka mpewe uhuru wa uhalifu , upuuzi mtupu


Nasikitika kuwa na watu wazima wenye akili Kama za kwako
 
Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao?
Third world country inayopumulia machine na kuomba omba iwe na uwezo WA kujitetea na kujiamulia??? Are you serious!!!


5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?
Israel sio third world country na haiitegemei ulaya dhaifu na ilio na baadhi ya wanafki kama ufaransa na uingereza kusurvive...


Mwisho, naomba wajifungie kuijadili Marekani na Udikteta wa Trump, alafu na sisi walau kidogo tutajua walau wanaouchungu na mataifa ya Afrika.
Trump sio dikteta ni raisi tajiri makini na muadilifu anaelipenda taifa lake...Zaidi umoja WA ulaya ni mtoto WA marekani..Maendeleo walio nayo wameyapata Kwa marekani (ref open door police after second world war)) Umoja WA ulaya utakuwa na viongozi wenye akili ya panya kama watafikiri kushindana na marekani inayowazidi kiuchumi,,kibiashara,,kijeshi na hata kwa neo la kijiografia.
 
Sawa Gift Mzalendo, kwanza naona umetumia wingi kama vile "mnateka" "mnaua" sasa ndio najiuliza hawa ni akina nani? Maana inaonekana umewajumuisha watanzania wote alafu wewe ukajiondoa basi niseme wewe ndie Mbunge wa Bunge la Ulaya ambaye umejitokeza kujibu maswali kwa niaba yao.

Iko hivi, kila Taifa hua inayomisingi kulingana na tamaduni zake iliyojijengea kutimiza malengo yake mfano Taifa kama Korea Kaskazini ambaye kiongozi wake ni Kim Jong Un a.k.a Kiduku hawa ukithubutu hata kunyoa kama yeye umeenda na maji, je kunyoa si haki? Na mataifa mengine na mifano ipo wazi mno. Hapa sitaki kuhalalisha kitu unachokiita mauaji bali nakufungua ubongo utambue mataifa mengine mnayoona yametulia wamekuwa na mipaka kwenye haki namna gani. Je, wewe ulishasikia mmekaa pale bungeni kwenu hapo uingereza kuwajadili? Okay! Labda mtaanza kusingizia makubaliano ya EU members lakini muhimu hapa tujiulize mlishaona wapi kwenye hiyo mikataba inasema "ukimweka tunayempenda jela au kumfungulia kesi basi tutaingilia sheria zenu za ndani pamoja na mamlaka ili kumwachia huyo tunayempenda". Kama upo huo mkataba weka wazi. Msitumie neno haki kwenye makubaliano mkaipachika kana kwamba sasa mnaouwezo wa kuamrisha mamlaka ya nchi nyingine.

Nadhani, mtakua mnapata somo kidogo-kidogo.
 
Kuomba ni mentality ya waafrika wa ajabu flani, nikikuuliza utaje nchi ambayo imeenda kuomba omba sidhani kama utaitaja "zingatia neno kuomba-omba". Ninachojua tunakopa sio kuomba, sasa wewe sijui ukienda kuchukua mkopo benki hua unaenda kuomba au hua una omba-omba? Okay! Unajua Marekani Taifa tajiri duniani anadaiwa kiwango gani? Fuatilia kama hauna takwimu nitakupa ujifunze.
 
Ch Changamoto ya kwanza ni uzalendo, viongozi wetu wamejawa tamaa mnoo, hawajali kabisa kuhusu taifa. Wao maslahi yao kwanza, taifa panapobakia.
 
Kwanini hujazungumzia Zionist na Palestine?
 
Kwanini hujazungumzia Zionist na Palestine?
Sio kweli,

Katika maswali, niliuliza moja kwa moja: "Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?" Hili ni swali la moja kwa moja linalogusa dhima ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.


Kwa hiyo, madai kuwa sikuzungumzia suala la Zionism na Palestina si sahihi.
 
Ndio maana Wasanii wa Bongo wanatutukana na kutuona walio wengi wajinga kwa kusema SA100 mitano tena kumbe wamekopeshwa fedha wanatumia kwenye starehe zao alafu hawataki kulipa!

WATANGANYIKA AMKENI.

GOD BLESS TANGANYIKA

Your browser is not able to display this video.
 
 
 
Unajitahidi kujibu kwa maneno mengi Ila hoja ni ile ile

Kuna haki ambazo ni universal kwa Taifa lolote lazima zisimamiwe

Ndo maana imesaini mikataba mingi Sana ya Kusimamia haki za kimataifa

Huwezi kusema utamaduni wetu ni kuteka kutesa kuonea na kuua raia wangu alafu dunia ikuache tu
Eti ni utamaduni wenu

Hapa unajaribu ni kunifunga ubongo sio kunifungua kuhusu Sheria na haki za kimataifa

Wewe ndo ujifunze juu Sheria na haki za kimataifa Kila Taifa Lina haki za Kusimamia

Huu uhuru wa kupiga watu mbele ya mahakama chombo cha Kusimamia haki ni inaonyesha dhahiri hiyo sovereignty umevuka mipaka

Usiliahe watu ujinga tàfadhali
 
🤣 🤣 🤣
 
Mkuu hakuna mtanzania mjinga anayeweza kufurahia nchi kuingiliwa kimamlaka.
Ila kinachofanyika hapa nikwamba unakifahamu na ukiona wananchi wanasapoti hilo bunge la ulaya baaasi walikuwa na vilio mioyoni mwao.

Kuhusu nchi zingine kujadiliwa hata wew umesikia na unajua kuwa Rwanda, Uganda, Libya na Congo zimejadiliwa sana.

Na hatasis wenyewe tumewahi kushiriki kuwaingilia majirani zetu kijeshi kwa mianvuli ya jumuia za kikanda na kimataifa kuwafundisha ustaarabu. Mfano ni Congo, Comoro na Sudani.
 
Tano, kama wataamua kuitunishia misuli EU kwa kujifariji kwamba tuta imarisha ukarbu na China na Arabs basi wafute vyama vingi kabsaa.

Ili wananchi wajue moja tuu kwamba taifa tumeingia kwenye mabadiliko ya kimfumo kisiasa nadhani hatutajadiliwa kabsaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…