Maswali 8 ya kuwauliza Bunge la Ulaya

Maswali 8 ya kuwauliza Bunge la Ulaya

Natamani mawasli hayo hayo jiulize kwa nini Tanzania inapeleka watoto wetu (Wanajeshi wetu) SUDAN, CONGO na maeneo mengine............Pia Msiwe mnapokea fedha zao....Maana mojawapo ya masharti ni kuwa na UTAWALA BORA
Ikiwa Bunge la Ulaya wanajiona wanahuruma na wapo tayari kubeba misaba ya mataifa mengine, basi eem, tujiulize yafuatayo:

1. Ni nani hasa wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania? Je, kuna ushahidi wa kisheria au ni maneno ya kisiasa yasiyo na msingi wa kikatiba?

2. Kwa kutumia msingi upi wa kisheria au mkataba gani wa kimataifa, Bunge la Ulaya linajipa mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, taifa huru linalojiongoza kwa mujibu wa katiba yake?

3. Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao?

4. Tokea lini Tanzania, kama taifa huru, imekuwa ikiingilia na kujadili masuala ya ndani ya nchi za Ulaya ndani ya mabaraza yake ya kisheria au ya kisiasa?

5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?

6. Kwa nini Bunge hilo hilo halikai kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jambo ambalo linaendelea kutikisa dunia na kusababisha madhara makubwa kwa raia?

7. Kwa nini pia wasikae kujadili ukandamizaji na unyonyaji wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kampuni nyingi za kimataifa zenye makao yao Ulaya zinatajwa kunufaika?

8. Je, Bunge la Ulaya linaamini katika misingi ya utawala wa sheria? Na iwapo jibu ni ndiyo, je, linaamini kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na hakuna aliye juu ya sheria, ikiwemo wao wenyewe?

Mwisho, naomba wajifungie kuijadili Marekani na Udikteta wa Trump, alafu na sisi walau kidogo tutajua walau wanaouchungu na mataifa ya Afrika.
o
 
Si usome budget estimates za mwaka huu??? Utaiona hiyo aiseee?????? Dunia inaondoka kwenye misaada sasa kwenda kwenye loans... misaada ni pesa kidogo sana
Hivi kukopeshwa si mpaka mkopeshaji akubali?

Nenda wewe leo bamk kakope millioni 100 tu kama unadhani kukopeshwa hakuna conditions zake.
 
Leo zaidi ya miaka 60 tangu mjitawale, unaenda kwa Mchina unamuomba msaada wa kujenga reli, anakupa mkopo wa fedha na kukupa masharti ya kununua chuma kutoka kwao, nawe unakubali na kuchekelea kama zwazwa huku ukiacha kutumia chuma chako, halafu unadai kuwa wanakupora/wanakuibia!!??
Na wao ndio walianza kututapeli tokea wakati kupora mali zetu, alafu wao wanatupatia mawe ya kung'aa, nguo na vyatu kisha wanaondoka na mali zetu. Tuishi hivi, hakuna taifa ambalo linaweza likawa na uchungu dhidi ya Taifa lingine. Ukiona amekomaa sana tambua anahitaji kurudi kututawala hadi kifikra.
 
Umewaza sawa mfano ufaransa yule mpinzani wake yuko rumande kwa kesi ya kukwepa kodi,usa huyo chizi wao alishitakiwa kwa kesi kibao kwakweli nyani hawezi kuona kundule
 
Ikiwa Bunge la Ulaya wanajiona wanahuruma na wapo tayari kubeba misaba ya mataifa mengine, basi eem, tujiulize yafuatayo:

1. Ni nani hasa wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania? Je, kuna ushahidi wa kisheria au ni maneno ya kisiasa yasiyo na msingi wa kikatiba?

2. Kwa kutumia msingi upi wa kisheria au mkataba gani wa kimataifa, Bunge la Ulaya linajipa mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, taifa huru linalojiongoza kwa mujibu wa katiba yake?

3. Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao?

4. Tokea lini Tanzania, kama taifa huru, imekuwa ikiingilia na kujadili masuala ya ndani ya nchi za Ulaya ndani ya mabaraza yake ya kisheria au ya kisiasa?

5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?

6. Kwa nini Bunge hilo hilo halikai kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jambo ambalo linaendelea kutikisa dunia na kusababisha madhara makubwa kwa raia?

7. Kwa nini pia wasikae kujadili ukandamizaji na unyonyaji wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kampuni nyingi za kimataifa zenye makao yao Ulaya zinatajwa kunufaika?

8. Je, Bunge la Ulaya linaamini katika misingi ya utawala wa sheria? Na iwapo jibu ni ndiyo, je, linaamini kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na hakuna aliye juu ya sheria, ikiwemo wao wenyewe?

Mwisho, naomba wajifungie kuijadili Marekani na Udikteta wa Trump, alafu na sisi walau kidogo tutajua walau wanaouchungu na mataifa ya Afrika.
Waandikie kwa kizungu, hiyo lugha ya kichawa hawaielewi
 
Tunachopigania kila siku Afrika kuwa huru ila kuna vichwa wao wanaamini katika kutawaliwa. Ushauri wangu, ambao mnataka kutawaliwa mtengeneze umoja wenu alafu mkawaombe muishi ulaya.
Una Uhuru gani wewe hapa BONGO? Hivi unafikiri UHURU ni GWARIDE siku ya TISA DISEMBA pale Uwanja wa Taifa?....
 
Ikiwa Bunge la Ulaya wanajiona wanahuruma na wapo tayari kubeba misaba ya mataifa mengine, basi eem, tujiulize yafuatayo:

1. Ni nani hasa wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania? Je, kuna ushahidi wa kisheria au ni maneno ya kisiasa yasiyo na msingi wa kikatiba?

2. Kwa kutumia msingi upi wa kisheria au mkataba gani wa kimataifa, Bunge la Ulaya linajipa mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, taifa huru linalojiongoza kwa mujibu wa katiba yake?

3. Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao?

4. Tokea lini Tanzania, kama taifa huru, imekuwa ikiingilia na kujadili masuala ya ndani ya nchi za Ulaya ndani ya mabaraza yake ya kisheria au ya kisiasa?

5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?

6. Kwa nini Bunge hilo hilo halikai kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jambo ambalo linaendelea kutikisa dunia na kusababisha madhara makubwa kwa raia?

7. Kwa nini pia wasikae kujadili ukandamizaji na unyonyaji wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kampuni nyingi za kimataifa zenye makao yao Ulaya zinatajwa kunufaika?

8. Je, Bunge la Ulaya linaamini katika misingi ya utawala wa sheria? Na iwapo jibu ni ndiyo, je, linaamini kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na hakuna aliye juu ya sheria, ikiwemo wao wenyewe?

Mwisho, naomba wajifungie kuijadili Marekani na Udikteta wa Trump, alafu na sisi walau kidogo tutajua walau wanaouchungu na mataifa ya Afrika.
Hujui kitu kuhusu Bunge la Ulaya wala mfumo mzima wa EU ambayo ndiyo mshirika mkuu wa maendeleo kwa Tanzania. Kasome.

EP Hawajajadili vita ya Ukraine, Gaza na DRC? Kasome kazi walizofanya na ratiba yao ya kazi.

Hawajadili udikteta wa Trump Marekani? Unahitaji kwenda shule upya.

Tanzania ikitaka kuwa huru kweli kweli; ikitaka mambo yake yasiguswe na mataifa mengine, basi iache kusaini mikataba/makubaliano mbalimbali ya kimataifa na iache kutafuta misaada na mikopo nafuu toka mataifa mengine na taasisi za kimataifa (multilateral institutions).

Lissu aliwahi kushauri ili Tanzania iwe huru kabisa kufanya mambo yake katika rasilimali zake, basi ijiondoe kwenye mikataba ya inayolinda wawekezaji wa kimataifa kama ule wa MIGA. Watu kama nyinyi, kwa akili finyu, mkafikiri mzaha. Sasa ni mwendo wa kulipa mabilioni kwa kuvunja mikataba bila kuzingatia sheria za kimataifa (sio zetu).
 
Bunge la ulaya halina lolote, Rwanda tu yenyewe wameishindwa, sembuse Tanzania!! Kila mtu ashinde mechi zake!
Ikiwa Bunge la Ulaya wanajiona wanahuruma na wapo tayari kubeba misaba ya mataifa mengine, basi eem, tujiulize yafuatayo:

1. Ni nani hasa wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania? Je, kuna ushahidi wa kisheria au ni maneno ya kisiasa yasiyo na msingi wa kikatiba?

2. Kwa kutumia msingi upi wa kisheria au mkataba gani wa kimataifa, Bunge la Ulaya linajipa mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, taifa huru linalojiongoza kwa mujibu wa katiba yake?

3. Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao?

4. Tokea lini Tanzania, kama taifa huru, imekuwa ikiingilia na kujadili masuala ya ndani ya nchi za Ulaya ndani ya mabaraza yake ya kisheria au ya kisiasa?

5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina?

6. Kwa nini Bunge hilo hilo halikai kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jambo ambalo linaendelea kutikisa dunia na kusababisha madhara makubwa kwa raia?

7. Kwa nini pia wasikae kujadili ukandamizaji na unyonyaji wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kampuni nyingi za kimataifa zenye makao yao Ulaya zinatajwa kunufaika?

8. Je, Bunge la Ulaya linaamini katika misingi ya utawala wa sheria? Na iwapo jibu ni ndiyo, je, linaamini kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na hakuna aliye juu ya sheria, ikiwemo wao wenyewe?

Mwisho, naomba wajifungie kuijadili Marekani na Udikteta wa Trump, alafu na sisi walau kidogo tutajua walau wanaouchungu na mataifa ya Afrika.
Ulivo taburalasa hujui hata kama eu ishajadili sana na kuipa msaada ukraine kwenye vita na urusi, ishajadili sana vita ya Israel na wapalestina sasa kama hivi vitu hujui vishafanyika unaonekana ni kilaza wa aina gani
 
Ukiona malalamiko ujue wameshika pabaya, lakini jibu kuu la maswali yote ni kuwa huwa mnakula vitu vyao mkiahidi kufuata Demokrasia na haki za binadamu na mikataba mmesaini,
 
Hadi hapa wewe kuandika ni uhuru gani umekubana mkuu, kila mmoja anao uhuru wa kufikiri tofauti hapa Tanzania, isipokua matusi, dhihaka dhidi ya wengine n.k.
Kama kuna UHURU Jiulize kwa nini Mama yako Hakutoa Pole Kifo cha Profesa Sarungi....Jiulize pia Kwa nini hakutoa pole kwa baada ya Fr. Kitima kupigwa.......
 
Wakubwa wa MuDunia wameshapima upepo wa yale yanayotokea Barani Afrika na wameshagundua kwamba sasa raia wa Nchi hizo wameshachoka na Intimidations ambazo zimeshakuwa ni kama business as usual kwa Nchi nyingi barani !

Sasa wanataka wao wasipoteze ile credibility yao ya muda mrefu kwamba wao ndio watetezi wa Human rights kwa wale wanaokuwa intimidated katika Nchi zao !

Kwahiyo mambo kama haya watayavalia njuga kweli kweli ili kuirudisha ile credibility yao iliyokuwepo kwa muda mrefu na ambayo ilianza kuporomoka kwa kasi ya 4g kwa siku za hivi karibuni. 😳 !

Muhimu watu wakajua these people are not joking !
Kila hatua wanayo chukua ujue imeshakuwa Calculated kwa ustadi mkubwa.

Sasa watataka kuwaonesha watu wa MuDunia kwamba wanayoyasema akina Traore kuhusu wao kushirikiana na wakubwa kuzinyonya Nchi za Africa sio za kweli !

Jamaa zetu hao huwa ni wepesi wa kusoma alama za nyakati na kutafuta solution wakati huo huo. !

Everything is happening for a reason 😳🙌🤷‍♂️🤩🙏 !

Ngoja Tusubiri tuone. !
 
1. Ni nani hasa wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania? Je, kuna ushahidi wa kisheria au ni maneno ya kisiasa yasiyo na msingi wa kikatiba?- jJIBU- TUME KWA KUWEKA KANUNI ZA HOVYO KAMA VILE WAKALA KUTOKUPEWA NAKALA YA MATOKEO WALA KUPIGA PICHA MATOKEO WALA KUWA NA SIMU KITUONI, AUTOMATICALLY UMEZUIA WENYE AKILI KUINGIA KWENYE UCHAGUZI

2. Kwa kutumia msingi upi wa kisheria au mkataba gani wa kimataifa, Bunge la Ulaya linajipa mamlaka ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, taifa huru linalojiongoza kwa mujibu wa katiba yake? JIBU- TAMKO LA HAKI ZA BINADAMU LA MWAKA 1948 NA MKATAB WA AFRIKA WA HAZI ZA WATU NA BINADAMU (HII WALIINUKUU KABISA)

3. Bunge la Ulaya lina mamlaka gani au dhamana ipi ya kuipigania Tanzania kana kwamba Watanzania hawana uwezo wa kujitetea wala kujiamulia mustakabali wao? JIBU- SWALA LA HAKI ZA BINADAMU SIO LA NCHI NI LA KIMATAIFA KAKA ILIVYO SWALA LA MAZINGIRA

4. Tokea lini Tanzania, kama taifa huru, imekuwa ikiingilia na kujadili masuala ya ndani ya nchi za Ulaya ndani ya mabaraza yake ya kisheria au ya kisiasa? JIBU- KWA SABABU TANZANIA NAYO ILISHAINGILIA KOMORO

5. Kwa nini Bunge la Ulaya halitengi muda kujadili na kuchukua hatua kuhusu mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina? HUNA HAKI YA KUONGEA KWA SABABU HUFANYI UTAFITI- RAIS WA BUNGE LA ULAYA ALISHATEMBELEA HUKO (European Parliament President Metsola visits Israel, Gaza and West Bank | News | European Parliament) PIA BUNGE LA ULAYA LILISHA JADILI SANA NA KUCHUKUA HATUA MBALIMBALI (Ceasefire in Gaza: extracts from the debate - Multimedia Centre)

6. Kwa nini Bunge hilo hilo halikai kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, jambo ambalo linaendelea kutikisa dunia na kusababisha madhara makubwa kwa raia? HII ILIKUWA MOJA YA AGENDA ZA JANA, KAFANYE UTAFITI.

7. Kwa nini pia wasikae kujadili ukandamizaji na unyonyaji wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kampuni nyingi za kimataifa zenye makao yao Ulaya zinatajwa kunufaika? HILI LIMEJADILIWA SANA KAKA HADI KUNA VIKWAZO VILIWEKWA KWA WAHUSIKA

8. Je, Bunge la Ulaya linaamini katika misingi ya utawala wa sheria? Na iwapo jibu ni ndiyo, je, linaamini kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya sheria na hakuna aliye juu ya sheria, ikiwemo wao wenyewe? JIBU - NDIO LINAAMINI KATIKA UTAWALA WA SHERIA
 
Wakiwa huko ulaya wanatamani bado kuitawala Tanzania.
 
Hivi kukopeshwa si mpaka mkopeshaji akubali?

Nenda wewe leo bamk kakope millioni 100 tu kama unadhani kukopeshwa hakuna conditions zake.
Kwani mkopeshaji wa hii mikopo ni Nchi???? Mingi inatoka IMF, World Bank na kwa sasa Mingi tunakopa AfDB, lakini kuna domestic loans pia.... kanuni muhimu zaidi kwenye kukopa ni ability to repay.....zingine stories tu
 
Kwani huwa mnaenda wapi kuomba misaada mnakopa hela kuzirejesha amuwezi sasa deni ni 97 T
 
Bunge la ulaya halina lolote, Rwanda tu yenyewe wameishindwa, sembuse Tanzania!! Kila mtu ashinde mechi zake!
Ona huyu mjinga unafananisha rwanda na tanzania? Mkibanwa sehemu uwa mnakuja na mifano ya kipumbavupumbavu tu

Ngoja wapitishe maazimo alafu mkaze shingo muone
 
Ukiweka uchawa pembeni ukajipa muda kufikiria hata wewe utawaelewa tu bunge la ulaya
Majibu yako haya hapa chini, point by point:

1. Ni nani wameizuia CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu wa Tanzania?
Ni wazi kabisa kwamba si Bunge la Ulaya lililowazuia CHADEMA kushiriki uchaguzi, bali ni vyombo vya ndani vya Tanzania – hasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jeshi la Polisi, na taasisi nyingine zilizotumika kisiasa kuzuia mikutano, kuwakamata viongozi, kuwatishia wafuasi, na kuzuia haki ya kikatiba ya ushiriki wa kisiasa. Ushahidi upo: kuanzia marufuku ya mikutano ya kisiasa, hadi matukio ya polisi kuvamia ofisi za chama na kuzuia wagombea kusajiliwa. Haya siyo maneno ya kisiasa; ni ukiukwaji wa wazi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 20(1) na Ibara ya 21(1).

2. Bunge la Ulaya lina msingi gani wa kuingilia masuala ya Tanzania?
Sheria ya kimataifa, hasa International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR), ambayo Tanzania imeridhia, inawapa haki mashirika na mabunge ya kimataifa kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu. Haki ya kushiriki uchaguzi, uhuru wa kujieleza, na kuendesha shughuli za kisiasa ni haki za msingi za kibinadamu, si “masuala ya ndani.” Ukivunja makubaliano ya kimataifa, huna kinga ya kusema “hii ni nchi huru.” Uhuru wa taifa hauwezi kutumika kama kinga ya uonevu na udikteta.

3. Je, Watanzania hawawezi kujitetea?
Watanzania wamekuwa wakijitetea kwa gharama kubwa sana – wengine wakifungwa, kutekwa, kupigwa risasi, na hata kuuawa. Mifano hai ni Tundu Lissu, Ben Saanane, na wengine wengi. Bunge la Ulaya halichukui nafasi ya Watanzania, bali linatoa msaada wa kimataifa wa mshikamano dhidi ya dhuluma. Huo ndio msingi wa maadili ya haki za binadamu duniani.

4. Je, Tanzania hujadili mambo ya Ulaya?
Tanzania haina nguvu wala ushawishi wa kimataifa kama Bunge la Ulaya. Lakini pia, hata isingekuwa hivyo, haiwezi kuwa kigezo cha kusema “na sisi hatujadili yao, kwa nini wao wajadili yetu?” Haki za binadamu si biashara ya kisasi; ni suala la dhamira na misimamo ya kimaadili.

5. Kwa nini hawajadili Israel na Palestina?
Hili ni hoja ya kupotosha. Bunge la Ulaya limetoa maazimio kadhaa kulaani mauaji ya Wapalestina, kuhimiza usitishaji wa mapigano, na hata kutoa msaada wa kibinadamu. Kusema hawajadili ni kupotosha au kutojua ukweli wa vikao vyao.

6. Je, kuhusu Urusi na Ukraine?
Hili nalo limejadiliwa mara nyingi mno. Bunge la Ulaya limeweka vikwazo kwa Urusi, limetangaza misimamo rasmi ya kulaani uvamizi, na limetoa misaada mikubwa kwa Ukraine. Kwa hiyo, hoja yako haina mashiko wala msingi wa ukweli.

7. Kuhusu rasilimali za Congo?
Bunge hilo hilo umeona hulioni linafanya lolote, lakini kwa taarifa yako, wameshawahi kuitisha mikutano ya dharura kuhusu unyonyaji wa madini ya Congo, wamelaani kampuni zinazohusika, na kuna juhudi za kuweka kanuni mpya za uwajibikaji wa makampuni ya Ulaya. Suala hilo ni changamano, lakini halimaanishi kimya kama unavyodai.

8. Je, wanaamini katika utawala wa sheria?
Ndiyo – na ndiyo maana wanajadili hali ya Tanzania. Kuwa na mamlaka ya kujiongoza haimaanishi kuwa juu ya sheria. Kama taifa linavunja haki za binadamu, halina kinga. Utawala wa sheria ni pamoja na kuhoji kila mamlaka inayokiuka haki za watu, iwe ni ya Ulaya, Afrika, au Marekani.

Kuhusu Marekani na Trump
Huo ni mkengeuko wa mjadala. Udikteta wa Trump ni changamoto ya Marekani, na Marekani hukosolewa na Wamarekani wenyewe, vyombo vya habari, na hata mataifa mengine. Ukiona mataifa ya Ulaya yanamkosoa Trump lakini bado yanakosoa Tanzania, basi hiyo ni dalili kwamba hoja zao si chuki binafsi, bali ni za kiutu na kimaadili.
 
Tunachopigania kila siku Afrika kuwa huru ila kuna vichwa wao wanaamini katika kutawaliwa. Ushauri wangu, ambao mnataka kutawaliwa mtengeneze umoja wenu alafu mkawaombe muishi ulaya.
Kama unategemea michango ya kibajeti ni tofauti gani hapo na kutawaliwa!? Au una maanisha kukaliwa kinabalu?
Unajua chochote kuhusu ukoloni mambo leo?
 
Back
Top Bottom