Kama ni taifa huru ni kipi kimefanyika baada ya kupata huo uhuru?
Elimu - shule hazina madawati, walimu hawajui wanachokifundisha bora liende.
Miundombinu - tunajisifu tuna miundombino bora na ya kuigwa, lakini ikitokea mvua utasikia daraja limesombwa, mara barabara hazipitiki, maafa kila kona.
Afya- zahanati, hospitalini hakuna madawa, madaktari na wauguzi wanachojua ni pesa na kama huna utakufa bila kufanyiwa matibabu na maiti yako wataizuia hadi jamaa zako waje kulipa gharama ambazo kimsingi hukupewa.
Ajira - limekuwa janga, aliyehitimu chuo na degree yake hakumbuki alichokisomea zaidi ya kurusha kindege (aviator), kubet, kuchoma chipsi na bodaboda. Utawala unaziita ni ajira. Kina dada nao wameona bora kujiuza huko mitaani na Telegram maana hakuna mwelekeo.
Uchumi - Tunasema uchumi wetu upo imara, huku deni la taifs linazidi kupaa, na hiyo serikali inaongeza kodi na tozo kila siku! Jiulize hizo kodi zinaenda kufanya nini, na wakati huohuo serikali inazidi kukopa? Jibu, ni kuwa hiyo mikopo na kodi zinaishia kwenye kikundi cha watu wachache wanaoamini kuwa hii nchi ni mali yao.
Siasa - unasema tume huru, huku wewe mgombea ndiyo umewateua, hii nchi ina maajabu kweli. Serikali haitaki kukosolewa kabisa na wanaokosoa wanaootezwa au kupewa kesi za ugaidi, uhaini na kuambiwa si Watanzania. Huo uhuru ni upi kama unanyimwa kutoa maoni na kukosoa serikali yako?
AU hicho kikunda cha wachache ndio wanaamini wa ni watanzania na wanahaki ya kufanya kile wanachokitaka huku dunia ikiwaangalia?