Mbona maswali yako mepesi sana, kupanda ndege wote tunaenda airport siyo?
1.Anayekwenda Mtwara na yuko Mbagala ataisubiri gari uko aliko, wa tegeta ataifuata gari stendi mbezi, au kampuni za mabasi yatakayo opt njia ya Bagamoyo yataanzia safari Mbezi wataelekea huko Tegeta alafu Bagamoyo. Kwa mara ya kwanza wakati nakuja Dar mabasi yote kwenda mikoani yalikuwa yanapakia na kushusha abiria KISUTU.
2. Dunia nzima katika miji yote mikubwa kuna vituo vya usafiri wa umma, utatoka nyumbani kwako utaenda ufuata usafiri. Kuna watu wanasafiri kwenda Kigoma, Bukoba, Mwanza, Arusha nk, wanakaa Mbagala, Chanika, Kigamboni mabasi wanapandia wapi kama siyo ubungo? Kuna wale tunaokaa Kiluvya na Kibamba siku za hivi karibuni mabasi yote mazuri kwenda kanda ya kaskazini yanapatia Bagamoyo tulikuwa tunawajibika kuyafuata Ubungo. Kwa hivo bado yeyote atakaye taka kusafiri lazima afuate gari stendi au lah tumia usafiri wako binafsi.
3. Mwisho kabisa kuna vitu ambavyo wakati tunanunua maeneo hatukuviangalia, mfano wewe kwenu ni Musoma, Mwanza, Bukoba, Kigoma nk unanunua kiwanja chanika au kigamboni, kwa nini usifikirie kujenga kimara, kibamba, kiluvya na hata kibaha anzia maili moja mpaka mlandizi?